Hivi kuna uhusiano wa kwenda Ulaya na kufeli maisha?

Hivi kuna uhusiano wa kwenda Ulaya na kufeli maisha?

Yaani Hilo ni TATIZO kiukweli..Wanaondoka wakiwa na ndoto kubwa sana Ila wanaishia kupoteza hata uwezo mdogo waliokuwa nao...SAD
Ishu ni kwamba maisha kule yapo juu sana na ujira ni wa kawaida..ni mkubwa ila sio kivile..na kaz nying ni vibarua(kwa hiz ngoz nyeus)...weng ni kubangaiza tu...ulaya ndo kabisaa..bora america wanahis wew ni afro american..ila ulaya plus ubaguz..halaf barid kal inakua ngum kupambana..halaf kule hamna vitu visivyo rasm..kama huku unaweza fungua genge tu maisha yakaenda....kule ni ishu..ukizingatia weng makaratas hawana.so wanabak kubangaiza na kupiga picha kwenye snow.....nna mwenzangu mmoja alibak ...sasa hiv anavuta mabangi na heroin huko..kinachomsaidia nikwamba jmaaa ni genius...so wazungu wanamkubal saana ila sasa ni kama kawehuka...macho mekundu muda wote yuko tipsy...
 
Na sisi tuna brother wetu amekaa nje miaka 4, yeye alirudi na begi la nguo tu baada ya kutumiwa nauli.
Saivi yupo yupo tu hana mbele wala nyuma!
Sijui huko ulaya kuna nini yaani?
mmmh same same here, ndugu yangu 7 years huko alirudi na begi pia lina track suit moja na viatu vitatu kila kimoja hakina mwenzie 🤔
 
Of course nilikuwa na mahesabu...Hivi Kuna binaadamu anaingia tu kwenye mahusiano bila kufanya mahesabu?utakuwa mwehu......sijui labda nyie wanaume

Apo nakuelewa Sasa[emoji4]

Sema jamaa nae mjanja Sana, alitumia mbinu Safi Sana kukunasa mwana mahesabu na ukajaa ukaliwa kimasihara

Otherwise Kama yeye alikupenda sana, alkua na long plans na wewe.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hii komenti ya DeepPond kama vile mashairi.. nimevua kofia.
 
Wasalaam wanajamvi.

Jamani Kuna jambo linanifikirisha kwa muda sasa, hivi kuna uhusiano wowote kwa vijana wa makamo wanaorudi toka ughaibuni na kufeli maisha?nimekutana na case Kama tatu hivi ambazo zimenivuruga kichwa.nitazielezea kufupi

1. Katika hekaheka za humu duniani nilikaribishwa kwenye house party moja maeneo ya Salasala,ilisheheni mbwembwe za kila aina, nilikuwa na wadada warembo na wakaka wamotoo, kila mtu alijifanyia ni mmarekani, Siku hiyo nilijiona nimeokota dodo chini ya mchongoma kwani Kuna jamaa very presentable aliyetambulishwa Kama ndio fresh karudi zake kutoka ughaibuni alitokea kunitunuku.hapo ndio ulikuwa mwanzo wa penzi tamu nikiwa na matarajio kibao.

Picha linaanzia huyu Bwana hana hata nyumba, kapewa nyumba na wazazi wake maeneo ya Tangi bovu ndio anaishi hapo,Huyu Bwana sifa ya umalaya hakubarikiwa, yeye ni mlevi hujapata ona,akiamka asubuhi anaoga,anawasha zake muziki anaanza kunywa whiskey jamani Ni asubuhi ya saa tatu, hiyo Ni mpera mpera mpaka atavyolala Sasa sita, Alikuwa anapenda kupika mwenyewe anapika anakula kidogooo vyote najilia mie yeye anatwanga mipombe yake..baada ya miezi kadhaa nikaanza muuliza ana mpango gani wa maisha?kazi au biashara hana jibu sahihi..Nina search zoom namuonyesha nafasi za kazi jibu lake sawa nita apply, miezi inayoyoma yule bwana hastuki wala nini.Imagine mtu ana 41 anapewa pocket money na mama..

Nikaanza lalamika kwa ndugu zake wa karibu ,mtoto wa baba yake mdogo akaniita faragha"Kama kweli una ndoto na maisha yako hapo unapoteza muda wako buree huyo hajarudi na kitu chochote zaidi ya begi lake na picha za kwenye barafu,,,huko Germany hajasoma chochote na wala huku nyumbani hajainvest kitu chochote kufupi Ni kwamba"Kaenda KUZURURA miaka Saba halafu karudi hoi..nikachoka na penzi likafa..Ila penzi lake lilikuwa tamu sana hana kero,muelewa, romantic kwa kweli abarikiwe Sana na atolewe tozo kwenye kila muamala ataofanya.

2. Huyu ni kaka wa best friend wangu, siku anaondoka hadi airport tumemsindikiza akielekea UK akiahidi ahadi kedekede lazima apambane atoke kimaisha kwamba nafasi aliyoipata hawezi chezea.....Jamani Kaenda huko miaka sita baadae hata nauli ya kurudi ilibidi atumiwe, karudi hana hata mia yupo tu amekuwa mwamba wa kupiga virungu.

3. Huyu wa tatu nahisi ndio kamaliza Ulaya yoteee kikubwa anachomiliki Ni saa aina Seiko anadai Ni original alinunua Milan,simu yake ya smartphone ,kiingereza kilichonyooka na album yake ya Google photos ukiwa imesheheni picha pambe kabisa zenye madhali ya kuvutia sana.Nae kwa virungu na uchawa hajambo.

Sasa Hawa Ni mfano tu wa wengi wanaokwenda huko ughaibuni na kurudi tee. hebu tuwaulize nyie mnaojiita Diaspora huko huwa mnafanya nini?wenzenu huku nyumbani Mambo yetu Ni bambam tumeoana,tuna watoto,tunaishi vizuri.Sasa huko jamani mbona Kama mnapoteza muda Ila mkitupia picha mnatuvimbia kwelikweli ilihali si uhalisia. My Take Kama huko Mambo meusi rudini nyumbani tujenge nchi..Nyie vijana wenye ndoto za kwenda kusaka tonge huko ughaibuni nawashauri mpambane tu hapa nyumbani mtatoboa unless mkachukue elimu mrudii.
Nina mchiz wangu anazaidi ya 10 yrs UK ye life lake anasemaga na single mothers wenye hela zao anaingia nao serious relationship wanamlea akija bongo. Sema anazali nao balaa sijui kachanjia. Saiz kashaoa mdada mmoja mme wake alifariki miaka ya nyuma na huyo dada yupo kitengo . Jamaa alizaaga na mzungu akiwaoneshaga madem mapicha wanapagawa. Saizi anakuja bongo mara mbili kwa mwaka na akija shughuli ni moja tu...lodge za sinza kazimaliza. Mchizi anakismart sana maana kabla ya hapo alikuaga na dem mwingine wa kitengo flani bank akala life balaa. Kiufupi ndo lifestyle yake na hawezi rudi bongo maana kukaa kule kunampa hiyo heshima. Angekuaga anaplan angekua level zingine maana kuna kipindi nilishikaga hela ndefu nikawa namsisitiza tufanye ishu ambayo tutakua tunaleta mzigo toka UK ila jamaa wala hajali,ye stori zake milupo tu na yupo above 40
 
Back
Top Bottom