Hivi kuna uhusiano wa kwenda Ulaya na kufeli maisha?

Ina maana ile siku huyo Sabaya ameenda kwenye ile hotel na kuhitaji aitiwe msanii alielala pale walikuja kufanikiwa kumla?[emoji848]
 
Ewaaa umenena vyema mkuu kila pahala wapo waloshindwa hvyo kwa hao wachache hatuwezi sema wengi wameshindwa hapana aiseeee!!
 
I swear, wala sio chai.....yani nimeona hiyo comment ya begi nikaanza tu kucheka mwenyewe
Joannah , Joline Kato , cariha na wengineo, si kweli kwamba ukipita katika mkoa wa Tabora ukiwa kwenye garimoshi na ukachungulia dirishani ukamuona ng'ombe mweusi, basi ng'ombe wote katika mkoa wa Tabora ni weusi!!

Mimi mbona nimekaa Miami (tamka 'Mayami') miaka mitatu tu nikarudi niko vizuri balaa, hadi leo napeta tu hapa mjini. Kama kuna mwana Jf anaijua Miami nimuelekeze nilipokuwa nakaa.
 
The diaspora is not monolithic.

If you associate with people who failed economically, that is a reflection of your poor judgement, small network and its poor reach.

We are out here making big moves.

Na siku hizi hata likizo tunaishia Turks and Caicos, au tukija Bongo ni kifamilia zaidi, kwa sababu ya umbeya wa wabongo.

Kama kuna lawama, laumu watu wako specifically, usipakazie diaspora.
 
Legend! Wamekuibua mzee Baba.

Mwenyewe nimewaambia miaka mitatu ilinitosha sana kujijenga, tatizo wanapenda kugeneralize..
 
Uko sahihi...Kuna mpuuzi hapa amekaa South Africa miaka nane. Alichorudi nacho ni cheni ya Silver na simu na sasa anataka nimkopeshe nauli eti akifika Dizonga' atanitumia double ya kiasi nitakachompa.
Hahahaahahahahahah

Muepuke fastaaaa
 
Hahahahahahah Miraj hana akili au
Yule mchizi alikuwa msela wa kitaa

Mtoto wq waziri ila mikato ya Gangstar au ganstar wannabe[emoji2]

Clique zake hawa bongo fleva akija AY na FA yaani ile east coast team na watoto wa kino.[emoji2]

Sijui ana mishe gani mjini ila sidhani kama ana njaa kiivyo the shadow of msoga empire is vast!!

Anakula kuku kwa mrija
 
Hebu fikiria mzee wa miaka 50 na zaidi yupo kwenye magenge ya kufanyia mitungo wajukuu zake...Halafu kwani binti alimlia Nani pesa mpaka asulubiwe kiasi hicho?
Ina maana yule binti aliliwa mtungo!!? ..acha utani
 
Bora hata wanao tokaga mashariki ya mbali ndio naonaga wanatoboa....Kuna wale wanaoenda Japan na Korea huko Wana afadhali
Nina washkaji zangu kama 11 hivi, Mmoja yuko JAPAN, Kyoto, Mmoja yuko UK, Brmingham, Mmoja yuko CANADA, Toronto, Mmoja yuko Denmark, Oslo, m1 yuko Namibia, Windhoek, Wa3 wako USA, Texas, California na Las Vegas Nevada, mwingine yuko zake South Africa, Cape town na mwingine anaishi TURKEY, Instanbul na wa Mwisho yuko Sehemu matata sana ARGENTINA, Iruya (Andes). Wote wana maisha mazuri tena sana wanasaidia sana ndugu zao. Ikumbukwe hawa wametokea maisha magumu tu, walikwenda huko kimasomo lkn wakabahatika kupata kazi.
Nilipata bahati ya kufika nchi 7 kati ya hizo, na niseme wazi anayeishi ARGENTINA yuko njema zaidi, yeye anafanya kazi kwenye hotel za hapo IRUYA, ana mke na watoto wa3 wazungu as You know Argentina haina wazawa weusi.

Wengi wanaotoka maisha safi kwenda nje kusoma wakirudi home wanakuwa tegemezi mifano iko mingi sana JUX ni mfano hai kabisa.

Wengi hawajitumi kwakuwa wanajua home kwao kuko njema.

Kuna jamaa tulikuwa nae Chuoni yeye Degree alichukulia Copenhagen Norway yaan hajielewi na sijui shida nini, na mwingine alitokaga kitambo ni kama bro kwangu alienda URUSI kusoma Udaktari ni mlevi sana, na ajabu anaijua dini (Muslim) ambapo aliwahi tuambia kuwa Russia kuna waislam wengi kuliko wakristo RC.

Kikubwa ni kujitambua tu. Mimi ni familia tu ila niliwahi kukaa Brazil miezi 6, nchi iko njema sana kazi nyingi nk sema changamoto ni kwamba mimi ni Muislam hivyo nililazimika kuhamia mji wa Rio de Janeiro ambako kidogo kuna misikiti angalua niweze kula chakula halali kwangu.

Vijana mupatapo fursa nje ya nchi ni muhimu sana kukumbuka shida za nyumbani na kujisevia kihela kidogo. Trick nzuri ni kutafuta demu wa kizungu afu unakuwa mwaminifu kwake maisha utayaona mtelezooooooo. Ref, MAD ICE yuko zake FINLAND, RAMA DEE Australia wanakula shushu kisa mbunye za kizungu.

Kuwa na maisha mabovu ni kujitakia.
 
Polee Inaonekana ww una deal na wanadiaspora zaid [emoji38][emoji38] ila ss wa kwa mtogole hatuna nafasi kwako
 
Ni wehu ni wachache sanaa wanakumbuka kujiwekeza wengi wao ni wehu blaza wangu wa pili anaishi UK mwaka wa 12 sasa hana nyumba wala mke wala mtoto japo yeye ni artist anijiweza kidogo huwa anakuja na kuondoka lakini abachofanya bongo hakuna hata kibanda
 
Mtu yoyote ambae amekwenda Marekani, UK au kwingine madhali ni ughaibuni na akasoma uzuri na kupata kazi za maana hukuhuko, hawezi kuwa na maisha ambayo umeyaeleza ya hao jamaa watatu.

Pili, kama ulikwenda huko kati ya 1995-2010 basi wewe utakuwa umetulia kimaisha yaani una nyumba hukohuko na una nyumba Tanzania lakini huiishi bali waipangisha na nyumba nyingine ndo wazazi wanaishi.

Tatu yaunga mkono namba 2 kwamba pia kama wazazi walikupeleka kule na wakahakikisha warejea bongo na wapata kazi nzuri, nyumba na baadae waanza familia, basi weye Ughaibuni ni kwa vekesheni tu.

Nne, yote niloeleza hapo juu yanataka plan, msaada wa wa wazazi kama walikuwa wajiweza uzuri ma kisawasawa.

Kwa mfano wapo vijana ambao wengi wapo nafasi za juu sasa hivi serikalini na nawafahamu wengine walikwenda huko na wakasoma uzuri na kisha wakarudi na sasa wapo wadunda.

Sasa ukitoka familia maskini au ya kipato cha kati lakini ikajikamua kukutafutia angalau nauli uende kule, lakini wakasahau kuwa wewe kichwani una yako na ukifika kule waanza vurugu basi utaishia kama hao ulowataja.

Hivyo uhusiano wa kwenda Ulaya na kufeli maisha kunategemea zaidi na business plan, strategy yako na mwono.

Kama huna hivyo basi weye ni failure.
 
Duuu! Sasa tutafanyaje mbona Mie nipo Ulaya Saizi. Ila connection na wadau kibao bongo, wameniaidi Kuwa siku nikirudi tu,watanipa Dili ya maama.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…