Hivi kuna uhusiano wa kwenda Ulaya na kufeli maisha?

Hivi kuna uhusiano wa kwenda Ulaya na kufeli maisha?

Kwenye maisha yoyote, popote ogopa kitu Ulimbukeni.

Kujitia mtu wa mjini kumbe umetoka Makanya Kwa kina Taikon.

Kujifanya Mzungu wakati wewe ni Muafrika.

Kujifaraguza unapesa au umetoka familia bomba wakati wewe ni fukara.

Ulimbukeni wa kupapukia na kurukia vitu vipya, ogopa sana
Watu wanajisahulisha uhalisia wao Kaka.
 
Kwenye maisha yoyote, popote ogopa kitu Ulimbukeni.

Kujitia mtu wa mjini kumbe umetoka Makanya Kwa kina Taikon.

Kujifanya Mzungu wakati wewe ni Muafrika.

Kujifaraguza unapesa au umetoka familia bomba wakati wewe ni fukara.

Ulimbukeni wa kupapukia na kurukia vitu vipya, ogopa sana
Kumbe tatizo ni u much knows
 
Hahaa ila Watz mnachekesha sana. Wengi wenu hamzifahamu vizuri nchi zilizoendelea.
Jamani huwezi kwenda kwenye hizo nchi ukatajirika tu kirahisi, lasivyo wananchi waliopo huko wasingekuwa wanalia kila kukicha inequality.
Maisha ya kule ni magumu mnoo, kila kitu kimeshajiset na matabaka yamekomaa. Sio rahisi uanzie from zero to hero. Ndio maana wengi wanaishia kwenye madawa wanakuwa disillusioned.
Mnashangaa mtu kakaa ulaya miaka kumi anarudi na begi mlitegemeaje labda? Atarudi akiwa na pesa kama Bill Gates? Ukitaka upate pesa haswa your best bet ni kujitahidi hapa hapa Tanzania. Huku bado mambo hayajiset na fursa nyingi hazijatendewa haki vizuri.
Waliokwenda hizo nchi wakafanikiwa ni wanafunzi walisoma kwa bidii na walijua watarudi kuendelea na maisha Tz; walioenda kule na very specific skill set wakaajiriwa kama vile wahadhiri wa vyuo (wanafundisha sana sana Kiswahili) au tech science etc au watu wenye idea au products zinazotafuta investors etc.
ASANTE kwa mchango mzuri.
 
Hahahaha eti viwandani. Hahahahaaa.
Unaujua ujira wa watu wanaofanya kazi viwandani relative to the living expenses za hizo nchi?
Unajua working conditions kwenye hivyo viwanda? Unajua hali ya migrant workers kwenye hivyo viwanda?
Nikajua utataja fursa ya maana eti viwandani. Hahahaaaa.
Nyie mnadanganya sana watu hapa Tz kwamba maisha ni bwerere kwenye nchi zilizoendelea, wanaishia kuwa frustrated na kuangukia kwenye uraibu.
Wanaorudi hoi bin taaban
 
Mimi nashangaa kwa nini mnajua Diaspora maisha yetu magumu lakini mnatuonea wivu, yaani nimeona humu topics za watu kuomba uraia pacha unaona kabisa watu mna chuki na wanaoishi nje! Sasa how unakua na jealous na mtu ambae maisha yake tayari ni magumu? Lol
Miaka ya Sasa sio miaka ya 1900s ambapo mtu akienda nje anaonekana Kama kawin Sana maisha,miaka ya Sasa Mambo yamebadilika Sana Dada watu wanaona kawaida Sana mtu kwenda huko,hii ni kutokana na baadhi yenu mnaorudi mkiwa hoi bila chochote na uraibu juu,wakati uliowaacha unawakuta wamefika mbali.Kama wewe umefanikiwa mshukuru Mungu Ila wengi wao Hali sio shwari,tunawaona tunaishi nao....Hakuna mtu wa kukuonea wivu eti kisa Ni Diaspora hakuna
 
My take---hili lina ukweli kwa kiasi fulani kwa upande ya wanaoenda kusoma nje ya nchi.
1.Kuna wanaoenda kusoma---wanajisahau hali ya maisha walioacha huku nyumbani--wao ni bata tu.Marafiki wanaokutana nao huko na ni kutoka hali na kipato tofauti---ULIMBUKENI unawapoteza--wanaacha walichokifuata.
2.Connections wanazozipata huko chuoni huwa zinapotea baada ya kuhitimu tu---na kila mtu anatawanyika kwenda kwao---ukirudi bongo huna hata mtu mmoja wa kukuonyesha mchongo au kukushika mkono kwenye soko la ajira---pia elimu ya nje haifanyi kazi kibongo bongo---very few waliosoma nje undergraduate wanaweza pambana na mishe za kibongobongo---I repeat---very few---Wachache sana!
3.Utamaduni wetu sio wa huko--vise versa is also true----kwenda nje ukasomea degree ya mambo ya fashion sijui interior design sijui upholstery---ulaya ni kazi zenye hela---unaenda UK kusomea kushona masofa---kazi ambayo bongo haihitaji degree---ni nyundo yako na kigodoro baas....wanaoendaga kufanya hizo courses tayari wana connections(either wanamiliki viwanda au wana uwezo wa kuendeleza kipaji.

Umenena vyema

Kitu wengi hawatambui michongo ya ajira unapata kwa connection Za uliosoma nao/wanaokufahamu ukipata chuo

Nakumbuka nilibahatika ajira mara baada ya kuhitimu na alienipa huo mchongo alikuwa ni Lecturer/mhadhiri wangu wa chuo kwakuwa aliona namna ninavyojituma na discipline niliokuwa nayo.

Baada ya kulamba ajira nikaongeza elimu and the rest is now History

Life is 90% luck 10% struggle
 
Back
Top Bottom