Hivi kuna ulazima kwa waamuzi wa kike kuchezesha mechi za Ligi Kuu ya wanaume nchini, huku na wenyewe wakiwa na Ligi yao?

Tate Mkuu

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2019
Posts
33,092
Reaction score
96,127
Nimeona niulize hili swali kwa sababu muda huu naangalia mubashara mechi ya mtoano kati ya Tabora United vs JKT.

Kilicho nihuzunisha ni maamuzi ya kibabaishaji ya hawa waamuzi wote watatu wa kike wanaochezesha huu mchezo. Imagine JkT inaongoza kwa ushindi wa magoli mawili ugenini; na yote ni ya kuotea!

Mchezaji wa Tabora United anavutwa karibu ya eneo la 18 mpaka anaanguka! Mwamuzi Tatu Malogo akapeta!! Mchezaji wa Tabora United anaambiwa ameotea, huku mbele yake kukiwa na mchezaji wa JKT!!

Nikijumlisha na ile mechi ya Tabora United vs Azam, na ambayo wachezaji wao wengi walizuiliwa kucheza ili wafungwe magoli mengi; kiukweli napata mashaka makubwa.
Hivi kuna uwezekano hii timu inahujumiwa eti ndiyo maana wameamua kuwapangia hawa incompetent referees!!!

Halafu kama kuna uhaba wa waamuzi wa kike, TFF iseme! Maana kwa upande wangu sioni sababu kwa hawa waamuzi wa kike kuchezesha mechi za wanaume, na wakati na wenyewe wana Ligi yao ya akina mama.

Na kama wanataka usawa, basi na waamuzi wa kiume nao waruhusiwe basi kuchezesha kwenye Ligi yao.
 
Hili lisichukuliwe kama ubaguzi wa kijinsia. Nchi hii Hakuna mwamuzi wa kike competent, waliopo wamecheguliwa kubalance gender.
 
Basi wajengewe uwezo zaidi mkuu, tutapataje watu competent bila kuwapa nafasi ya kupractice?

Sielewi sana kuhusu mpira, lakini naomba kuulizwa swali.. hao wanawake wamefanya hayo makosa kwasababu ni wanawake? Kama jibu ni ndiyo, kwanini?

Dunia nzima inapambana na gender stereotypes, Tanzania haiwezi kubaki nyuma.
 
Ni swali la msingi kabisa
Haiwezkan wao ligi yao wanachezesha wao tu,alafu ya wanaume pia wachezeshe,ndio yaleyale ya Muungano,mzenji anamiliki ardhi bara Ila ni vise versé kwa mbara
 
Hao wanawekwa ili kubalance equation.
Nasikia kuna mitihani yao ya kupima kama wamekidhi kuchezesha huwa wanafaulu kule kikeni lakini ndio hivyo wanachezesha hadi kiumeni.

Lakini kumbe refaree wa kuchezesha kiumeni inabidi afuzu mtihani wa kiumeni.
 
Back
Top Bottom