Hivi kuna ulazima kwa waamuzi wa kike kuchezesha mechi za Ligi Kuu ya wanaume nchini, huku na wenyewe wakiwa na Ligi yao?

Wale waamuzi ni VILAZA
 
Matokeo yakoje?
Tabora United amefungwa goli 4-0 kwenye uwanja wake wa nyumbani. Kati ya hayo magoli 4, magoli 2 ya mwanzo yote yalikuwa ni ya kuotea! Ila mshika kibendera akashindwa kuitafsiri sheria ya kuotea.
 
Vipi kwani kuna baya lolote wakichezesha ligi ya wanaume? Au kuna jambo limetokea.
Mimi naona wengi wao wana mapungufu kwenye kuchezesha mechi za wanaume. Hivyo nadhani wangechezesha mechi za Ligi ya wanawake wenzao.
 
Wakidanga, mnawasema., Wakipambana mnawasema..
Anyway tatu amezingua
Uzuri kuna Ligi ya wanawake. Sasa ndiyo nimeuliza kama kuna uhaba wa waamuzi wa kiume, mpaka ligi ya wanaume kuendelea kuchezeshwa na waamuzi wa kike?

Mbona hatuwaoni waamuzi wa kiume wakichezesha mechi za wanawake kama tunataka kujenga mazingira ya usawa?
 
Tabora united inashushwa kifigisu kama ilivyopanda kifigisu. Ilichukua nafasi ya Pamba mwaka jana.
 
Ulisoma comment yangu iko Wazi. Tunalazimisha kuwa na Waamuzi wanawake lakini dunia nzima vyama vya soka vinawachukua Kwa tahadhari kubwa Sana waamuzi wanawake kuchezesha Mechi za wanaume. Mifano ipo Kwa England, Spain, Italy, South Africa nk. Lakini Sisi tumeingia mkenge kisiasa kwenye soka nako tunatafuta gender balance. Binafsi naamini Kwa Sasa tunaongoza Afrika Kwa kuwa na Waamuzi wengi wa kike bila kujali ubora wao. Kama haiwezekani Wachezaji wa kike kusajiliwa timu za wanaume kutokana na kigezo cha nguvu na Kasi, Kwa nini tulazimishe waamuzi wa kike kuchezesha Mechi zenye Kasi kuliko uwezo wao?
 
Halafu katika hali ya kushangaza na wenyewe wana Ligi yao ya wanawake! Na imekuwa ikifanya vizuri tu. Sasa kwa nini wasibakie huko kwenye Ligi yao?

Ingekuwa kipindi kile hakuna Ligi ya wanawake, tungesema labda waendelee kupewa nafasi ya kuchezesha ili kuwapa hamasa wanawake wengine kuupenda mchezo wa soka! Ila kwa bahati mbaya tumeshatoka huko!

Sasa ni kwa nini waamuzi wanawake waendelee kuchezesha mpira wa wanaume, na wakati huo huo wana ligi yao ya wanawake! Na kama tunataka usawa, ni kwa nini waamuzi wa kiume nao hawaruhusiwi kuchezesha Ligi ya wanawake?
 
Kama hiyo mechi kmeonyeshwa live mbona hamna haja ya kupiga makelele sana kinachotakiwa ni hao Tabora United kuandika barua na kuituma bodi ya ligi na tff ili hatua zichukuliwe, wanaotakiwa kulaumiwa ni hao tff na bodi ya ligi maana ndio wanalea ujinga.
 
Makes sense...
 
Sasa kuandika barua huko Bodi ya Ligi na TFF ndiyo kutabadilisha yale matokeo ya kupangwa? Yaani kesi ya nyani apelekewe Ngedere kuamua!!

Hapa wadau wa michezo tunahoji sababu ya TFF kuendeea kuwatumia waamuzi wa kike kwenye michezo ya wanaume.

Kama ni kufungiwa, hawa waamuzi wameshafungiwa mara nyingi tu kwa sababu ya huko kuvurunda kwao; lakini bado mpaka leo wanaendelea tu kulindwa.
 
Kwahiyo kwa kupiga kwako makele humu ndio kunaenda kubadilisha hayo matokeo? Mwanamke kuchezesha mechi ya wanaume sio kesi ili mradi awe anaujua na kuzitumia sheria za mpira wa miguu.
 
Kwahiyo kwa kupiga kwako makele humu ndio kunaenda kubadilisha hayo matokeo? Mwanamke kuchezesha mechi ya wanaume sio kesi ili mradi awe anaujua na kuzitumia sheria za mpira wa miguu.
Unapata maumivu gani nikipiga hayo makelee humu jukwaani kulalamikia mambo ya kipuuzi yanayofanywa na TFF/Bodi ya ligi?
 
Mimi naona wengi wao wana mapungufu kwenye kuchezesha mechi za wanaume. Hivyo nadhani wangechezesha mechi za Ligi ya wanawake wenzao.
Ok, sasa hapo sio kwamba wawezeshwe zaidi. Huko nako si wataharibu tena ligi ya wamama.
 
Waamuzi wa kike hawafai kuamua mechi za wanaume wapo slow kufanya maamuzi,mara nyingi huwa wanafanya maamuzi ya ovyo,kuna ile mechi ya simba lakred kapigwa goli kauwahi mpira kaanzisha haraka simba ikaenda kushinda,ulikuwa ni uzembe wa refa wa kati na linesmen wake ambao wote walikuwa wanawake,
 
Imarisheni ligi ya wanawake ili watumike huko. NADHANI BADO KIDOGO MTATULETEA KOCHA MWANAMKE TIMU YA TAIFA
Wajengewe uwezo, itawasaidia sana kwavile uzoefu wanao tena wa maamuzi, (mabovu), pia wawakumbushe pia madhara ya maamuzi mabovu na adhabu zake kama zipo
 
Hii Womanization of everything inakera sana. Watu uwezo hawana ila Viongozi wa Dunia wanaforce tu kuwabeba hao viumbe. Inakera sana!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…