Sensei Tai
Senior Member
- May 26, 2022
- 168
- 466
Nakumbuka miaka ya nyuma niliwahi kuwa na mpenzi ambae nilimpenda sana na nadhani alijua kwamba nampenda hivyo akawa anautumia upendo wangu kwake kama udhaifu na fimbo ya kunichapia.
Nilijitahidi kadri ya uwezo wangu kumvumilia mana hata ningesema nimuache haraka haraka nitaacha wangapi, siku zilikwenda na bibie alikua anaendelea na drama za hapa na pale mana anajua hata tukigombana haipiti hata wiki nitajirudi.
Kuna wakati ulifika ambapo moyo bado unataka kuendelea nae lakini akili inaniambia nifanye maamuzi ya kiume, nilianza kupunguza mawasiliano nae ambapo mwanzoni nilikua siwezi pitisha wiki bila kuwasiliana nae lakini ilifika point nikaona nakua na amani zaidi nikiwa siwasiliani nae kuliko nikiendelea kuwasiliana nae.
Hii mbinu yangu ya kumpunguza kwenye mawasiliano ili work out ambapo nilikua na uwezo wa kukaa hata mwezi au miezi mitatu bila kuwasiliana nae.
Huyu binti alikua akiona kimya sana ananitafuta yeye mwenyewe lakini nilikua simzingatii tena kama ni sehemu ya maisha yangu na nadhani aligundua kabisa kwamba nishachoka drama zake hivyo sihitaji tena kuendelea nae.
Siku hizi sina tena moyo wa namna ile na mtoto wa kike akianza kunionesha drama huwa naona kama ana matatizo ya akili mana nilishatoka kwenye hizo mambo za kuleteana drama na mwanamke akitaka kuondoka kwenye maisha yangu huwa namfungulia mlango kiroho safi mana hakuna kitu special sana ako nacho ambapo wengine hawana.
Kwanini uendelee kumbembeleza mtoto wa mtu ambae mmekutana ukubwana wote mkiwa na meno 32 halafu kibaya zaidi ukiangalia hana kitu special sana ambacho huwezi pata kwa mwanamke mwingine au mwanaume mwingine.
Bado unateswa na mapenzi? karibu na wewe utupe uzoefu wako