Hivi kunywa pombe ni dhambi?

Hivi kunywa pombe ni dhambi?

Wagalatia 5:19-21
Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi, ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi,
husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu.

Kama una mpango wa kuingia Mbinguni au Peponi acha pombe,
inauwezo mkubwa wa kukukwamisha kuingia mbinguni.

1 Wakorintho 6 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
⁹ Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti,
¹⁰ wala wevi, wala watamanio, wala walevi, wala watukanaji, wala wanyang'anyi.

Mbingu ni ya watu safi,sober.
Mfano tu mdogo.
Kama kazini kwako huruhusiwi kwenda umelewa, je Mbinguni si zaidi.
Kati ya Mungu na Mwanadamu wa kuheshimiwa zaidi ni yupi?
Basi pombe haifai kwa mtu mwenye nia ya kwenda Mbinguni.
Muujiza wa kwanza wa kristo ni kubadili maji kuwa pombe katika harusi ya kana,ili watu wafurahie sherehe.
 
Mpe kileo yeye aliye karibu na kupotea; Kampe divai yeye aliye na uchungu nafsini.
 
Muujiza wa kwanza wa kristo ni kubadili maji kuwa pombe katika harusi ya kana,ili watu wafurahie sherehe.
Sasa wewe ni mtu wa Kana?
Au pombe unayoinywa ni ya muujiza wa kristo?
Endelea kujipa ambavyo hukupewa, Ikiwa mganga tu hafanyi uganga akiwa kalewa au mteja wa mganga hapigiwi manyanga akiwa kalewa,
Wee huogopi?
 
Wakuu, jana nimetoka kwenye mishe zangu nikapitia bar flani ya jirani kupooza koo kidogo.

Wakapita walokole flani hivi tunafahamiana nikawapungia mkono,wakaniita pembeni,jambo Lao kubwa likawa wananiambia eti niache kunywa pombe kwani unywaji wa pombe ni dhambi kubwa sana.

Nikawaitikia ila baadae nikafungua Biblia kutafuta mstari wowote unaosema kuwa kunywa bia ni dhambi lakini sijaona popote palipoandikwa hivyo.

So labda na nyie mnisaidie kujua wakuu,je kunywa pombe ni dhambi au sio dhambi?
si hivyo tu bali pia,
kunywa pombe kupita kiasi ni hatari kwa afya, maisha na uhai wako.

kunywa kistaarabu.

hakuna haja ya kubababika sana na wanaodai ni dhambi au si dhambi.

ukishakunywa pombe na kuufakamia kitimoto ya kutosha na kachumbari yenye ndimu na pilipili kwa mbali, usisahau kunywa maji, ni muhimu sana 🐒
 
Majungu, uzembe, mitusi, fitina, chuki, kusemgenya ni dhambi kuliko pombe

Btw pombe haina dhambi…

Dhambi ni matendo yatomanayo na matendo ya aliyezidisha kipimo cha pombe
 
Majungu, uzembe, mitusi, fitina, chuki, kusemgenya ni dhambi kuliko pombe

Btw pombe haina dhambi…

Dhambi ni matendo yatomanayo na matendo ya aliyezidisha kipimo cha pombe
Nimekubali.Waovu wengi hupenda kujificha kwa kuwataja watumia pombe na wao wasitirike kwa maovu yao lukuki.
 
.Nikawaitikia ila baadae nikafungua Biblia kutafuta mstari wowote unaosema kuwa kunywa bia ni dhambi lakini sijaona popote palipoandikwa hivyo.

So labda na nyie mnisaidie kujua wakuu,je kunywa pombe ni dhambi au sio dhambi?
Hii imetufunga kamba, kwamba ukaenda kufunua Biblia yote kwa muda mchache ili kutafuta maandiko, teba ukiwa umetoka kunywa pombe!
 
Back
Top Bottom