Hivi kunywa pombe ni dhambi?

Hivi kunywa pombe ni dhambi?

Wakuu, jana nimetoka kwenye mishe zangu nikapitia bar flani ya jirani kupooza koo kidogo.

Wakapita walokole flani hivi tunafahamiana nikawapungia mkono,wakaniita pembeni,jambo Lao kubwa likawa wananiambia eti niache kunywa pombe kwani unywaji wa pombe ni dhambi kubwa sana.

Nikawaitikia ila baadae nikafungua Biblia kutafuta mstari wowote unaosema kuwa kunywa bia ni dhambi lakini sijaona popote palipoandikwa hivyo.

So labda na nyie mnisaidie kujua wakuu,je kunywa pombe ni dhambi au sio dhambi?
Kunywa pombe sio dhambi ila unywaji wa pombe unaweza kukupelekea ukatenda dhambi kirahisi sana,kwahiyo haishauriwi kama umeamua kuokoka kuendelea kunywa pombe kwani itakutoa nje ya lengo....
 
Wagalatia 5:19-21
Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi, ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi,
husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu.

Kama una mpango wa kuingia Mbinguni au Peponi acha pombe,
inauwezo mkubwa wa kukukwamisha kuingia mbinguni.

1 Wakorintho 6 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
⁹ Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti,
¹⁰ wala wevi, wala watamanio, wala walevi, wala watukanaji, wala wanyang'anyi.

Mbingu ni ya watu safi,sober.
Mfano tu mdogo.
Kama kazini kwako huruhusiwi kwenda umelewa, je Mbinguni si zaidi.
Kati ya Mungu na Mwanadamu wa kuheshimiwa zaidi ni yupi?
Basi pombe haifai kwa mtu mwenye nia ya kwenda Mbinguni.
Ulevi ni kutokuwa na kiasi katika jambo lolote.
Zingatia neno "Jambo lolote"
Iwe michezo,kazi,hata kushika dini kupita kiasi hadi unasahau kufanya kazi unashinda kwenye kwaya au kanisani au msikitini.Utashindwa kutunza familia yako kwa kutofanya kazi.Na mtu asiyewatunza wa kwao ni mbaya kuliko asiyeamini.

Kuhusu pombe labda hoja ingekuwa kwamba inaleta uraibu,hivyo iogopwe.

Lakini kwa sasa simu tanashati ( smart phones) zinaleta uraibu mkubwa kuliko pombe.Watu wengi wamejifunza ushetani mkubwa kupitia mitandao.Hususan watoto wa kike wengi ni waraibu wa mitandao sana.Wengi wanashawishika kufanya ushetani kwa kuwa wameathirika na taarifa ovu za mitandao.
 
Unachozungumzia ww hayo ya watoto wakike,mitandao ,mabadiliko ya tabia n.k kimemezwa na maadili, ingekuwa ni mada tungeiita maadili.
Ww Umejikita katika uraibu wkt aliyekutwa bar hajaelezea kama yy ni mraibu.
Mwenye Hoja kauliza
je kunywa Pombe ni dhambi?

Kabla hujatafsri ulevi ,ungejikita kwanza hp ktk Pombe na ubaya wake.
Mkuu mm naamini hasara za kunywa pombe ni nyingi kuliko faida zake (km zipo).
Hivyo ikisemekana pombe ni dhambi,kwangu mm ni ndiyo.
 
Kunywa kwa kiasi siyo dhambi bali ni afya, hao Walokole ni wanafiki tu hata wao wana dhambi nyingi wakiwa kama Binadamu, hakuna mkamilifu hata mmoja chini ya Jua.
 
Roman Catholic Huwa wako sahihi katika suala la pombe. Hakuna sehemu kwenye biblia inayosisitiza kutogusa pombe bali maandiko yanasisitiza usilewe.
 
Siku mojaa nilikunywa pombe Kisha nikapanda daladalaa,nikakosa siti nikasimama.Nikamwambia konda silipi maana sijakaa kwenye gari lenu nauli yenyewe buku tu,Dah! Kwenye kushuka konda na dereva walitaka kunichangia nimegomaa mpaka wakaniacha sikulipa nauli.

Ziliponiisha pombe kumbukumbu ikanijiaa nilichofanya,Dah! Nikawaza wale wehu wangekua wamevuta bob Marley wangenitia makonzii ningeaubikaa Sanaa.
 
kuna
Wagalatia 5:19-21
Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi, ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi,
husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu.

Kama una mpango wa kuingia Mbinguni au Peponi acha pombe,
inauwezo mkubwa wa kukukwamisha kuingia mbinguni.

1 Wakorintho 6 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
⁹ Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti,
¹⁰ wala wevi, wala watamanio, wala walevi, wala watukanaji, wala wanyang'anyi.

Mbingu ni ya watu safi,sober.
Mfano tu mdogo.
Kama kazini kwako huruhusiwi kwenda umelewa, je Mbinguni si zaidi.
Kati ya Mungu na Mwanadamu wa kuheshimiwa zaidi ni yupi?
Basi pombe haifai kwa mtu mwenye nia ya kwenda Mbinguni.
kuna tofauti kati ya kunywa na kulewa, zipo substance nyingi zinazolevya
 
Wakuu, jana nimetoka kwenye mishe zangu nikapitia bar flani ya jirani kupooza koo kidogo.

Wakapita walokole flani hivi tunafahamiana nikawapungia mkono,wakaniita pembeni,jambo Lao kubwa likawa wananiambia eti niache kunywa pombe kwani unywaji wa pombe ni dhambi kubwa sana.

Nikawaitikia ila baadae nikafungua Biblia kutafuta mstari wowote unaosema kuwa kunywa bia ni dhambi lakini sijaona popote palipoandikwa hivyo.

So labda na nyie mnisaidie kujua wakuu,je kunywa pombe ni dhambi au sio dhambi?
Kwa mujibu wa torati na injili kunywa pombe siyo dhambi ...hata ulevi siyo dhambi bali ulevi ni haramu kwa sababu unazuia kusikiwa na mungu pia ulevi unaweza kusababisha dhambi kamili ...chochote kilicho haramu kipo karibu sana na dhambi kamili...mfano ulafi ni haramu ..kutamani mke wa mtu ni haramu ...kumpenda mzazi au yoyote kuliko mungu ni haramu ...uvivu ni haramu nk mfano kuna hatua chache sana baina ya uvivu na dhambi ...
 
Back
Top Bottom