Wagalatia 5:19-21
Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi, ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi,
husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu.
Kama una mpango wa kuingia Mbinguni au Peponi acha pombe,
inauwezo mkubwa wa kukukwamisha kuingia mbinguni.
1 Wakorintho 6 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
⁹ Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti,
¹⁰ wala wevi, wala watamanio, wala walevi, wala watukanaji, wala wanyang'anyi.
Mbingu ni ya watu safi,sober.
Mfano tu mdogo.
Kama kazini kwako huruhusiwi kwenda umelewa, je Mbinguni si zaidi.
Kati ya Mungu na Mwanadamu wa kuheshimiwa zaidi ni yupi?
Basi pombe haifai kwa mtu mwenye nia ya kwenda Mbinguni.