Ingekuwa vizuri ukaanza kwa kufunguka wewe mkuu.
Mimi nimesomea masuala ya kodi kwa ngazi ya chuo, lakini natumia zaidi nilichosomea ngazi ya sekondari.
Kuna watu nawafahamu wamesoma Kiswahili ngazi ya chuo, lakini wanafanya kazi kama bankers.
Tuendelee kuwa encourage watu kupata maarifa.
Kwa kifupi tu mkuu sisi ni miongoni mwa nchi za watu wengi wenye maarifa madogo, ukiweza ingia hata Dar es Salaam randomly watest wakubwa na vijana kwa maswali ya general knowledge katika masuala ya afya,biashara,historia na jiografia.
Utakutana na watu wanakuelezea kazi za ini kwa sifa za mapafu, kazi za utumbo kwa sifa za moyo🙁
Kazi za manispaa na halmashauri kwa sifa za TRA😳
Kauli kama vile "kwao huko mikoa ya kusini kusini Kigoma,Kigoma, Kagera,Kagera huko"🙂
Ukiweza pia mkuu jitahidi upate maoni ya katiba mpya kipindi cha tume ya Warioba yale maoni kabla hayajawekwa sawa kukidhi mahitaji.
Mpaka leo kuna "wajinga" wanaweza sema anataka kufanya kazi fulani halafu anataja vyeo, utaskia nataka kufanya kazi ya Uraisi badala ya kusema siasa, kufanya kazi ya u IGP badala ya kusema Polisi,unakuwa unajiwazi moyoni huyu mtu hata uwezo wake wa kutengeneza mantiki utakuwa na tatizo.
Kibaya zaidi unakuta wanaoongea hivyo miaka yao ni 20-45. Mpaka unakiri kimoyo moyo kuwa kwa kweli kama taifa tunastahili kuwa hapa tulipo.
Tukiri tu wajinga wengi wamewazidi nguvu wenye maarifa, na silaha sahihi ni kusambaza knowledge, overtime vizazi vitajikomboa.