Usikate tamaa jombaa, kuna sehemu Bado wanahitaji ujuzi wa mikono yako, ni Swala la muda tu, huo umri Bado sana. Kuna boss wangu mmoja mzungu wa SA, ana miaka, 68!
Alipofukuzwa kazi kwenye kampuni yetu, akarudi kwao, akaendelea kutafuta ajira, maana na Cha msingi ujuzi anao, kampuni moja ya Ulaya ikamuona ikamchukua, sasa hivi ana 70+na ni country manager East Afrika nzima, anakula bata tu na anachapa kazi ni energitic kama balobalo wa miaka 30!! Usikate tamaa mangi endelea kuwa na ndoto, tukate tamaa pale tu tutakapo nyamaza milele.