Hivi kwanini baadhi ya Maeneo Dar Maji hayajafika na kuna maeneo huko ndanindani wametandaziwa Mabomba km yote? Nini Shida?

Hivi kwanini baadhi ya Maeneo Dar Maji hayajafika na kuna maeneo huko ndanindani wametandaziwa Mabomba km yote? Nini Shida?

Bueno

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2022
Posts
34,600
Reaction score
59,760
Wakuu, kwa wasioijua Dar wakafikiria Dar labda kila sehemu kuna umeme kila sehemu kuna Maji, aisee kuna maeneo mjini Dar-es-Salaam hakuna maji mpaka leo watu wanafukua maji Chini wanachota maji ya tope wanaoga fungus maji ya chumvi maji yasiyo na virutubisho wengine ndio maji yao ya kunywa hayo mpaka leo,

Sijajua shida ni nini na hapo unakuta mgombea wa maeneo hayo Diwani na Mbunge kikifika kipindi hiki cha kujinadi anakuja na hoja ya kuleta maji akishapita kwamba wamchague yeye awamu hii anawaletea maji hawatochota tena maji ya Visima ila balaa akishachaguliwa Mbunge anapotelea Bungeni harudi tena Jimboni kwake kutekeleza kile alichosema mpaka muda uishe anakuja tena na mradi wa kuwachezea wananchi kwamba nitawaletea maji awamu hii lazima mpate maji wakimpa tu anapotelea Bungeni harudi tena,

Hivi haya maeneo ya Dar ambayo maji hayajafika mpaka leo hawa wanasiasa na Serikali wana mpango gani na haya maeneo?

Maana nimepita maeneo mengi watu wanatumia maji ya Visima vya kuchimba chini local Visima kabisa ndio wanapikia hayohayo wanafulia hayohayo tena wakienda kufua wanakaa hapohapo kisimani hayohayo wanamwagilia mbogamboga hayohayo wanatawaza wakienda Msikitini ndio maji wanayoyakuta, hayohayo kukiwa na sherehe ndio wanayopikia na wengine hayohayo ndio maji wanayokunywa,

Watu wa Serikali kuanzia Mkuu wa Mkoa mpaka wengine wanaohusika wana mpango gani na haya maeneo ya Dar ambayo mpaka leo hakuna maji safi na salama kwa kunywa na kupikia?

Mimi nimetembea huko mafichoni na machakani (Mikoani) ambako sikutegemea nitakuta maji nikakuta kuna mabomba safi watu wanapata maji ila nashangaa Dar kuna maeneo maji hayajafika mpaka hii leo, what's wrong you people? Watu wanakunywa maji aliyokunywa Chura na Ng'ombe is this serious? Come on
 
Unaongelea wap. Toa mifano.

Mji unatanuka kwa kasi. Kumbuka Maendeleo hupangwa kulingana na budget.
Iwe Maji barabara na huduma za jamii.

Ukiona uko sehem alaf huduma za jamii ikiwepo maji barabara na umeme uko mbali na ww basi jua uko pembezoni sana na Jiji.
 
Unaongelea wap. Toa mifano.

Mji unatanuka kwa kasi. Kumbuka Maendeleo hupangwa kulingana na budget.
Iwe Maji barabara na huduma za jamii.

Ukiona uko sehem alaf huduma za jamii ikiwepo maji barabara na umeme uko mbali na ww basi jua uko pembezoni sana na Jiji.
Dar hii hii Dar kuna maeneo maji hakuna hayajafika kabisa na haijulikani km yatafika miaka 100 mbele au vipi ila kuna viongozi wapo Bungeni kila wakija kwenye hayo maeneo wanapewa hio kero wanasema wakipewa uongozi wataleta maji wakipewa tu wanaenda kujificha Bungeni jimboni hawaonekani tena
 
Mbezi msakuzi tuu hapo maji hakuna.
Unaona sasa wakati mimi nimeenda Mbwise huko Mkoani nimekuta mabomba yanatandazwa km yote huku Dar kuna maeneo ukienda km upo kijijini kwetu ambako leo kuna maji wametandaziwa mabomba ila huku mjini Dar eti maeneo hayana maji ya bombani wanahangaika na maji ya Visimani
 
Back
Top Bottom