Hivi kwanini kuna watu wakisikia jina la January Makamba wanapatwa na hofu?

Hivi kwanini kuna watu wakisikia jina la January Makamba wanapatwa na hofu?

Tuna kumbukumbu mbaya dhidi ya huyu Kigogo14 wenu.

Kwanza alikopa mahela kupitia mgongo wa wana Bumbuli na akawapiga na hata huko Benki nadhani bado anadaiwa...
Baba yetu wataifa alishatufundisha kuwa kujenga hoja sio kupayuka bila data zozote. makamba ni mtanzania mwenzetu kama ulivyo wewe na famili yako, leta ushahidi hapa aliwapiga vipi ili tukuone kama sio mpika majungu tu kaa wengine, acheni hizo hiziwasaidii lolote
 
Kwa siku kadhaa sasa nikipitia humu JF naona jina la January Makamba linatajwa sana, hasa kwa mabaya. Lakini cha kushangaza watu hao wanaomsema kwa mabaya hawana ushahidi wowote...
Ukweli kuna jingine mkuu, lipo haswaa! Siku zote mtu akizidiwa akili na ujanja basi hukimbilia kwenye chuki kwa aliyebarikiwa. Makamba yuko vizuri sana na hilo ndo tatizo kwa wachawi wengi humu, na nikwambie tu kuwa baadhi ya wachawi hao humu ni vigogo wenzie wenye ndoto fulani hv......anao bungeni, anao kwenye baraza lao la mawaziri.
 
Hata wewe hapa umelipwa ili uje kumtetea hapa.
Ni wapi umeona kamtetea, kasema makamba apewe muda tuone matokeo sio kumuhukumu mapema. Uongozi sio mchezo ndugu yangu mangine huwa nimajungu tu kupakana matope hii hali inapaswa kukemewa kwa kila mtu mwenye mapenzi mema na taifa letu. Chuki zikiendelea hivi kuna siku tutakuja kuuana
 
Kwa siku kadhaa sasa nikipitia humu JF naona jina la January Makamba linatajwa sana, hasa kwa mabaya. Lakini cha kushangaza watu hao wanaomsema kwa mabaya hawana ushahidi wowote.

Kitu kingine ambacho sikielewi ni kwamba huyu kijana amekuwa waziri kwa takribani miezi mitatu sasa lakini watu wanataka mambo yabadilike ki miujiza bila ya kumpa nafasi ya kuleta mabadiliko.

Hii inapelekea mimi kujiuliza, hivi hawa watu ni kweli wanachukia utendaji wake au kuna jingine?
Mti wenye matunda bora ndio hupigwa mawe

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
 
Ukweli kuna jingine mkuu, lipo haswaa! Siku zote mtu akizidiwa akili na ujanja basi hukimbilia kwenye chuki kwa aliyebarikiwa. Makamba yuko vizuri sana na hilo ndo tatizo kwa wachawi wengi humu, na nikwambie tu kuwa baadhi ya wachawi hao humu ni vigogo wenzie wenye ndoto fulani hv......anao bungeni, anao kwenye baraza lao la mawaziri.
Kisafi hakisafishwi ni kichafu ndio huwa kinasafishwa.
 
Acha kuwa mjinga basi ni wapi umeona kamtetea, kasema makamba apewe muda tuone matokeo sio kumuhukumu mapema. Uongozi sio mchezo ndugu yangu mangine huwa nimajungu tu kupakana matope hii hali inapaswa kukemewa kwa kila mtu mwenye mapenzi mema na taifa letu. Chuki zikiendelea hivi kuna siku tutakuja kuuana
Huyo hata apewe miaka mia sita hatabadilisha chochote zaidi ya kufanya ufisadi tu
 
Mti wenye matunda...
P
Wa kukuamini wewe tena baada ya tukio lile wamebaki wachache sana.
 
Tatizo aliingia wizarani kwa kumsulubu Magufuli kuwa hakuwahi kukarabati mitambo ya TANESCO, hili kosa litagharimu sana.
 
Huyo hata apewe miaka mia sita hatabadilisha chochote zaidi ya kufanya ufisadi tu
Kaka usipende ku generalize vitu unakosea tena sana, utendaji wa wizara hautegemei mtu mmoja tena waziri ambae ni msimamia sera tu na utekelezwaji. Makamba hana professional ya mambo ya nishati ila ana moral authority ya kusimamia uwajibikaji.

Kumbuka bro wizara ni taasisi kuba viongozi wengi tu kuanzia katibu mkuu mpaka mameneja. Tuache chuki tukumbushane Watanzania wote kutimiza wajibu wetu kikamilifu ili kuliletea maendeleo Taifa letu tukufu. Narudia acha chuki
 
Tatizo aliingia wizarani kwa kumsulubu Magufuli kuwa hakuwahi kukarabati mitambo ya TANESCO, hili kosa litagharimu sana.
Hapa aliyumba kweli kumsagia kunguni mzee Magu, hawa viongozi kuna haja yakupewa semina elekezi hata na raia wenye maono nje ya mfumo ili wasiendelee kupanda chuki, hapa makamba alitereza kuendeleze chuki za kijinga kutafuta huruma kumbe ndio anajikaanga mwenyewe. Viongozi wajue haya nimaisha ya watu wasibebeshane zigo la mavi panapotokea changamoto
 
Back
Top Bottom