Hivi kwanini mnamtumia huyo mwenye id ya "anonymous" kuelezea changamoto zenu si mueleze wenyewe tuwape miongozo nini cha kufanya

Hivi kwanini mnamtumia huyo mwenye id ya "anonymous" kuelezea changamoto zenu si mueleze wenyewe tuwape miongozo nini cha kufanya

Ukileta changamoto yako wewe mwenyewe humu jukwaani watu watakuhoji lakini pia watakushauri nini cha kufanya kuliko hilo roboti lenu mnalolituma

Kujeni wenyewe au mnaogopa kuanzisha account jf?
Nimekuwa nikijiuliza sana hiki kitu, hao anonymous ni member wapya au ni wakongwe tu wanaokuja na IDs nyingine kufikisha kero zao?
 
Nimekuwa nikijiuliza sana hiki kitu, hao anonymous ni member wapya au ni wakongwe tu wanaokuja na IDs nyingine kufikisha kero zao?
Huyo ni mtu mmoja anaetumiwa inbox changamoto ili azilete humu nahisi sasa si walete wenyewe tuwashauri
 
Basi labda uelewa wangu ni mdogo

Mimi nilidhani hao ni watu ambao hawajajiunga humu ndiyo maana inatokea anonymous!
 
Hata wewe una uwezo wa kutuma changamoto yako kama Anonymous. Hii ni kulinda identify yako kufahamika na mamlaka unayoilalamikia. Kuomba JF ipaze sauti kwa niaba yako.
Kuliko kuwatumia modes pia naweza nikaileta mwenyewe hapa na bado msinijue kwani wengi sio verified member

Maana yangu ni kuwa nikileta mwenyewe changamoto yangu zingine zinashaurika hivyo mshauri anaweza kunihoji nikajielezea na kunipa muongozo
 
Feature ya Anonymous ni nzuri sana mkuu kuepuka Dm baada ya kupost SPANA.

Kuna watu wana issue nyingi ila kuzitoa kwa kutumia ID ambayo inajulikana wanaweza kuunganisha dots na post za nyuma wakajua ni nani ,ila kwa anonymous ngumu kujua.

Hata Facebook group kuna feature ya Anonymous au Nick Name.
 
1781939577175.png
... mi naitwaga kishimbe 'ata kwenye NIDA!
 
Feature ya Anonymous ni nzuri sana mkuu kuepuka Dm baada ya kupost SPANA.

Kuna watu wana issue nyingi ila kuzitoa kwa kutumia ID ambayo inajulikana wanaweza kuunganisha dots na post za nyuma wakajua ni nani ,ila kwa anonymous ngumu kujua.

Hata Facebook group kuna feature ya Anonymous au Nick Name.
Unabonyeza wapi ili kuwa na feature ya anonymous sio kuwa wanawapostia modes na kutuma izo changamoto

Nahisi ingekuwepo hio feature kusingekuwa na mrudikano wa id nyingi kwa mtu mmoja wasinge anzisha id nyingi lakini pia kwanini ukimuhoji huyo anonymous huwa hajibu comments
 
Back
Top Bottom