Hivi kwanini mtu akija huku Dar anapenda lafudhi ya kiswahili chetu?

Wa Mkoani bhana utawajua tu wakikaa miaka kadhaa wanaona nao wamezaliwa Temeke wakati mtu kufika Daslm kauza Mbuzi mpaka kamba zake baadae akisahau anazungumzia mambo za lafudhi yao...
 
Kila wakiiga wewe unapoteza kiasi gani kwani??
 
Kwani Dar es salaam si mkoa? Mbona Tanga wana kiswahili kizuri kuliko cha Dar na wanaume wa Dar?
Kizuri kwa vigezo gani?
Tangu lini ulisikia lahaja zafanana?
Mwingine atakuja atasema kipemba,kiunguja, kitumbatu au kingazija ndio kizuri zaidi?

Mwingine ataenda mbali na kusema kimwani Cha Mtwara na Kaskazini mwa msumbiji ndio bora, utakuwa na hoja ya kumpinga?

Kwa nini mnajitahidi kupiga lafudhi ya dar? Hilo ndilo swali.
 

Lafudhi ya Dar ndiyo ikoje?
 
Umejiingiza mwenyewe. Hata hao 'wabara' kama wewe wana rahaja zao na unapaswa uzikubali mwanangu vingine untatea kabobo kama siyo uzwazwa.
 
Hiyo ni lafudhi ya uswahilini kwa ajili ya waswahili wa temeke, Manzese, kilawani, vingunguti, kawe, mbagala n.k njoo mikocheni, masaki na obay uone lafudhi za kichaga na kihaya.
 
Lafudhi huwezi kuilazimisha, utskuwa unafanya comedy tu, lafudhi inajengwa kwa muda mrefu, mtoto anapozsliwa sehemu, atachukua uongeaji wa eneo Hilo, mtoto wa kagera, Arusha, Dar hawawezi kuongea lafudhi moja ya kiswahili,nilienda Arusha, wakati naulizia stand ya mabasi ilipo, wale vijana wa stend wakasema njemba ya dar, kwa kukusikiliza tu unavyoongea, ukienda zenj, ukiongea tu, wanajua M Bara huyu!
Ila lafudhi inafundishika, nimeona wa bongo wengi kwenye NGO za nje, wakijifunza kuongea lafudhi ya kimarekani, na British, na ukisikia maongezi Yao, utafikri unaongea na wazungu
 
Sijui wa mikoa mingine ila
Wanaotokea Arusha hawawezi kuiga hata wakitaka
Wakirudi na hiyo lafudhi watu wa huku wanaweza mjengea kanyumba kake pale mpakani KIA Akae hukohuko
 
Sisi wasambaa umetutenga?
 
Kwa kutumia sentensi fupi, naomba mfano mmojawapo wa lafudhi ya Dar
Lafudhi ipo ni kweli ila ya waswahili ukiwa mshua hutaisikia sababu inapeta sana kwenye dala dala, vijiweni, shule za wenyeji mfano jangwani, temeke, kinondoni, msasani. Vijiwe kama karume, magomeni, tandale n.k

Ila kariakoo madukani huwwzi sikia, maofisi ya serikali, binafsi huwezi sikia, mlimani city huikuti, kwa kifupi ni lafudhi ya watu wa uswahilini waswahili OG
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…