Hivi kwanini mtu akija huku Dar anapenda lafudhi ya kiswahili chetu?

Saaa hiyo si lafudhi (Accent), hiyo inaitwa "Slang"

Ni kama Kenya, kuna lafudhi ya Wakikuyu au Wakenya na kuna slang ya Nairobi ambayo Mombasa wala Lamu haipo
 
nimekaa bongo 20 years lakini lafudhi yangu haiwezi kuwa ya kizaramo hata siku moja. nitakuwa nimejishusha hadhi sana.
 
Dar hakuna Kiswahili kizuri, watu wanaongea slangs tu
 
Wewe utakua ni mtu mshamba sana, na hapo usikute chimbuko lako umetoka Ludewa huko, au Urambo Tabora, lakini ubishoo wa mjini umekukaa unajifanya we ni wa town... wabongo bhana
Huyu ni dogo wa Kaliua, Tabora. Vijana wa Tabora wakija Dar wanakuwa na ulimbukeni fulani hivi, sawa tu na vijana wa Kigoma.
 
Ninyi ndo wazawa au sio. Wenye dar yenu.
 
I love this post. I showed this post to my family & they also loved this post.we bought a projector & showed this post to the whole neighborhood & they also loved this post. Our lives have changed because of this post. We are grateful to you for this post,Thank you so much for this post..
 
Asilimia tisini umeitoa wapi?....watu wa mikoani wapo lakini sio kiasi hiko.
 
Kubali tu...lafudhi ya kiswahili Cha Dar hakifanani na Cha kwenu mikoani. Hakuna mtu anayeiga lafudhi ya kihaya au ya kichaga Kwa sababu zimejaa kishamba shamba Hilo halipingiki. Hata hao wachaga/wahaya wanaozaliwa Dar wakawa na lafudhi ya Waswahili wa Dar akija huko vijijini kwenu huwa anakuwa na hadhi tofauti. Na wengi hapa mjini kuanzia huko unakosema ofisi za serikali na Kariakoo kiswahili kinachotumika ni lafudhi ya Dar.
 
Kuna baadhi ya lafudhi za makabila fulani fulani kama wahaya, wamasai , wachaga, wahehe, nk ni ngumu sana kutoka na rahisi kuadopt.

Na wengi sio kua anajilazimisha ila inatokea tu nae anaongea kama wenyeji wake.

Kuna mnyakyusa alienda kusoma chuga, akawa anaongea km wa huko. Alipoenda dsm lafudhi ile ikapotea taratibu na sasa haipo tena anaongea kama watu wa dar wengi waongeavyo.
 
Yaani mimi kabisa chalii ya kisimiri niende dar nianze kuiga kiswahili cha huko
Chalii yoyote hawezi fanya uwo uduwanzi wa kiree.
 
Jaribu kuja mbeya alafu jiongeleshe hiyo unayoiita lafudhi yenu.....

Kila mtu ata kudharau....
 
Muha akishakaa mjini zaidi ya mwezi anajiita mtu wa Dar, sawa bwana, basi wewe ni Mzaramu.
 
Muha ni hivi, siku hizi hapa Tanzania watu wengi wameelimika na kuchukia ushoga, wewe jaribu kwenda mikoani na kujifanya wewe ni kijana wa Dar, uone watu watakupeaje huko.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…