Hivi kwanini Nahreel na Aika hawapati sapoti ya kutosha Bongo ili hali wako na sound ya tofauti kuzidi wasanii wengi wa kwenye A list

Navy Kenzo wapo katika dunia yao peke yao, mziki wao si wa nchi hii ya waswahili ndo maana jamii kubwa ya waswahili haiwaelewi. Twende mbele turudi nyuma wawili hawa hasa Nahreel ana mikono ya dhahabu kwenye midundo, tunatofautiana namna ya kusikia lakini kwa mimi niliyeanza kufatilia mziki miaka hiyo tena mziki wa Marekani na bongoflavor yetu ya wakati huo ambayo ilikuwa pia inafanya sampling kwenye Hiphop ya Marekani naweza sema Nahreel na Navy Kenzo yake wapo Level yao peke yao, wana audience yao wanayoitarget, hivyo si lazima wabongo wote wawaelewe na kuwaimba, tupo sisi wachache hatutaacha kuruka nao kila watakapotoa ngoma, ni kama mimi ambavyo siruki na Singeli, Amapiano wala Taarab ila si kwamba hizo genre hazina watu wakali la hasha ni masikio yangu tu hayapati radha katika hizo genre.
Ukipata time sikilizeni #Fella# ndo mtaelawa kuwa Navy kenzo wapo hapa Bongo lakini akili ya mziki wao ipo dunia ya kwanza huko.
 
Wamezoea kucheza nyimbo za udugu wangu
Mbwa kabisa
 
Zile beat Nahreel alizowatengenezea Joh na Weusi zilikuwa za kiwango kikubwa sana., nilikuwa ninatamani Nahreel aendelee kusuka beat, ila bahati mbaya Wasanii wengi huwa hawapendi kuwalipa maproducer ndio maana ninaona kama aliacha kutengeneza beats kwa ajili ya Wasanii wenzake.
Kiukweli ukitoa Ma-producer wa zamani, kwenye kizazi hiki ninamwelewa zaidi Nahreel.
 
Nahreel alikuwa anaachia mikwaju sana
Sisi tuliowahi kupitizia hizi kazi ndiyo tunaelewa

Zile beat zilikuwa kama mambele yaani ilikuwa mzuka sana ile nusu nusu ni beat moja ya viwango sana na don't bother na nyingine nyingi hasa za joh makini

Ila joh tamaa ilimponza akaenda switch rec huko akaishia kupuyanga tu mpaka leo anaruka ruka tu
 
Mashabik wengi wa bongo tabia zao ni km za chama fulan hv, hawafatilii mziki km mziki bali nani anatrend ata km anaimb utopolo
 
Huenda ni wewe hujawapea attention lkn jamaa kila wakitoa single hakun mtz hajui
 
Vanessa anataarifa kwamba Jux kaoa?
Haoni wivu?
Yaan Vee amuonee wivu jux? Km yeye mwenyewe ndo aliamua kutoka, anaumiajee?

Vanessa anakula maisha mambelee, hana muda na mlamba lips.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kamatia Chini, hii ilibamba na iliuza vibayaa.
 
Sema mie huwa napenda life style yao, wasanii wengine waliokuwa wanaendana na hawa ni Vanessa na Jux.

Vanessa nae alikuwa na uimbaji fulani wa kuvutia sana.
1. Wet ft Gnako
2. Niroge
3. Me and you
4. Bambino
[emoji91][emoji91][emoji91]
Never ever
Nobody but me Ft KO.

hizi ziko ki international. [emoji91][emoji91][emoji91]
 
Never ever
Nobody but me Ft KO.

hizi ziko ki international. [emoji91][emoji91][emoji91]
Naona wamewatrndisha sana mtandaoni hatimaye juzi wakaalikwa na kutokea kwenye camera. Ila ukiwaangalia ni kama hawako comfortable.
 
wabongo hawapendi nyimbo zenye mbwembe za kiingereza kingi, wanataka kiswahili zaidi.
hiyo style yao ya ki mamtoni ukiiendekeza bongo flevani utakufa njaa. ni vyema wangebadilika kwa baadhi ya nyimbo kama walivyofanya vee money na shaa wakasogea kidogo.
 
Wanajua wanachokifanya mkuu, ndo maana hawabadiliki. Nadhani toka nimewafahamu wananyimbo nne pekee zilizokaa kiswahili swahili tu kuna ile ngoma yao kwanza kabisa kama Navy Kenzo inaitwa Chelewa aka Bokodo, Moyoni, Cheza kizembe na Usinibwage. Mikwaju mingine yote baada ya hapo ni kule mbele wanakokujua wenyewe na tunaoelewa kazi zao.
 
Kuna interview moja niliwahi kumsikia Nahreel akiadmit kuwa audio production hailipi, yaani watu hawalipi wanachukulia poa tu na wakilipa ni kile wanachojisikia, hapo ndipo alipoamua kuweka bei na mkataba wa malipo kuwa ili akutengenezee mdundo sharti ulipe Tsh 1mil. Hapo ndipo wasanii karibu wote aliokuwa anafanya nao kazi walikimbia wakiwemo na hao washkaji wake wa Weusi hasa Joh.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…