Ford Range
JF-Expert Member
- Oct 13, 2016
- 344
- 525
Navy Kenzo wapo katika dunia yao peke yao, mziki wao si wa nchi hii ya waswahili ndo maana jamii kubwa ya waswahili haiwaelewi. Twende mbele turudi nyuma wawili hawa hasa Nahreel ana mikono ya dhahabu kwenye midundo, tunatofautiana namna ya kusikia lakini kwa mimi niliyeanza kufatilia mziki miaka hiyo tena mziki wa Marekani na bongoflavor yetu ya wakati huo ambayo ilikuwa pia inafanya sampling kwenye Hiphop ya Marekani naweza sema Nahreel na Navy Kenzo yake wapo Level yao peke yao, wana audience yao wanayoitarget, hivyo si lazima wabongo wote wawaelewe na kuwaimba, tupo sisi wachache hatutaacha kuruka nao kila watakapotoa ngoma, ni kama mimi ambavyo siruki na Singeli, Amapiano wala Taarab ila si kwamba hizo genre hazina watu wakali la hasha ni masikio yangu tu hayapati radha katika hizo genre.
Ukipata time sikilizeni #Fella# ndo mtaelawa kuwa Navy kenzo wapo hapa Bongo lakini akili ya mziki wao ipo dunia ya kwanza huko.
Ukipata time sikilizeni #Fella# ndo mtaelawa kuwa Navy kenzo wapo hapa Bongo lakini akili ya mziki wao ipo dunia ya kwanza huko.