Hivi kwanini Nahreel na Aika hawapati sapoti ya kutosha Bongo ili hali wako na sound ya tofauti kuzidi wasanii wengi wa kwenye A list

Hivi kwanini Nahreel na Aika hawapati sapoti ya kutosha Bongo ili hali wako na sound ya tofauti kuzidi wasanii wengi wa kwenye A list

Navy Kenzo wapo katika dunia yao peke yao, mziki wao si wa nchi hii ya waswahili ndo maana jamii kubwa ya waswahili haiwaelewi. Twende mbele turudi nyuma wawili hawa hasa Nahreel ana mikono ya dhahabu kwenye midundo, tunatofautiana namna ya kusikia lakini kwa mimi niliyeanza kufatilia mziki miaka hiyo tena mziki wa Marekani na bongoflavor yetu ya wakati huo ambayo ilikuwa pia inafanya sampling kwenye Hiphop ya Marekani naweza sema Nahreel na Navy Kenzo yake wapo Level yao peke yao, wana audience yao wanayoitarget, hivyo si lazima wabongo wote wawaelewe na kuwaimba, tupo sisi wachache hatutaacha kuruka nao kila watakapotoa ngoma, ni kama mimi ambavyo siruki na Singeli, Amapiano wala Taarab ila si kwamba hizo genre hazina watu wakali la hasha ni masikio yangu tu hayapati radha katika hizo genre.
Ukipata time sikilizeni #Fella# ndo mtaelawa kuwa Navy kenzo wapo hapa Bongo lakini akili ya mziki wao ipo dunia ya kwanza huko.
 
Tatizo sio wewe mkuu tatizo ni "Tanga" nyie huko zenu Taarab,singeli,mchiriku,mnanda na baikoko sio rahisi kusikiliza na kuelewa mziki wa Navy.

Yani watu wenye ngoma kama Company,Morning,Why now,Manzese,Game,Fella useme hawajui? Leta album yoyote unayoiona bora bongo hivi karibuni ikiwezekana hata miaka 10 iliyopita halafu nikuwekee album za Navy Kenzo, watu wajudge nani ni wasanii na nani ni wanamziki!

Navy Kenzo ndio maana halisi ya mziki, na ukija kwenye uproducer Nahreel ni mikono iliyobarikiwa anzia Riz one,Shem lake njoo kwenye ngoma za Weusi ambao tangu waache kutoa mziki kwa Nahreel mara ya mwisho kutoa nyimbo nzuri angalau kwa Luffa!
Wamezoea kucheza nyimbo za udugu wangu
Mbwa kabisa
 
Nahreel ndiyo producer ambaye angeupeleka muziki wetu panapotakiwa sio hawa s2kizzy kazi kidogo Kiki nyingi sana

Fuatilia hata weusi walipoondoka kwa nahreel ndiyo kimoja hivyo wamepotea .

Joh makini tangu aondoke kwa Nahreel ndiyo mpaka leo anahangaika hangaika
Zile beat Nahreel alizowatengenezea Joh na Weusi zilikuwa za kiwango kikubwa sana., nilikuwa ninatamani Nahreel aendelee kusuka beat, ila bahati mbaya Wasanii wengi huwa hawapendi kuwalipa maproducer ndio maana ninaona kama aliacha kutengeneza beats kwa ajili ya Wasanii wenzake.
Kiukweli ukitoa Ma-producer wa zamani, kwenye kizazi hiki ninamwelewa zaidi Nahreel.
 
Zile beat Nahreel alizowatengenezea Joh na Weusi zilikuwa za kiwango kikubwa sana., nilikuwa ninatamani Nahreel aendelee kusuka beat, ila bahati mbaya Wasanii wengi huwa hawapendi kuwalipa maproducer ndio maana ninaona kama aliacha kutengeneza beats kwa ajili ya Wasanii wenzake.
Kiukweli ukitoa Ma-producer wa zamani, kwenye kizazi hiki ninamwelewa zaidi Nahreel.
Nahreel alikuwa anaachia mikwaju sana
Sisi tuliowahi kupitizia hizi kazi ndiyo tunaelewa

Zile beat zilikuwa kama mambele yaani ilikuwa mzuka sana ile nusu nusu ni beat moja ya viwango sana na don't bother na nyingine nyingi hasa za joh makini

Ila joh tamaa ilimponza akaenda switch rec huko akaishia kupuyanga tu mpaka leo anaruka ruka tu
 
Mashabik wengi wa bongo tabia zao ni km za chama fulan hv, hawafatilii mziki km mziki bali nani anatrend ata km anaimb utopolo
 
Mimi huwa niko na kawaida ya kutengeneza playlist tofauti tofauti na kuzisikiliza wakati naendelea na kazi zangu (huwa napata utulivu wa kubaki kwenye jambo moja kwa wakati huo, kwasababu kichwa changu huwa kina shida ya kufungua mafile mengi kwa wakati mmoja hasa kikiwa kwenye utulivu wa kutokupokea mambo mapya kutoka nje, hali hii huwa inanifanya niweze kufanya vitu nusu nusu).

Sasa leo kwenye playlist yangu nimejikuta niko na ngoma kadhaa za hao jamaa wakuitwa navy kenzo, na kilichotokea ni kwamba wakati ngoma inahama kutoka kwa hawa jamaa kwenda kwenye ngoma ya msanii mwingine kuna test tofauti kabisa ambayo inatosha kusema ile ngoma iliyopita haiwezi kuwekwa kwenye mzani sawa na hii iliyoingia kutokana na ubora wa sound yake.

Yaani kuanzia kwenye midundo hadi mixing, na uimbaji wao na midundo ni kama imefungana kiasi cha kuleta test fulani ya tofauti yaani ile test ya ki-Grammy Grammy kabisa.

Kila siku tumekua tukistruggle juu ya wasanii wetu kupenya kwenye soko la kimataifa ili hali tobo la kutupeleka huko ni kama lipo wazi kabisa ila ni vile tu hatujaamua, kwa mfano "Nahreel on the beat" ingekua inaskika kwenye ngoma nyingi za wasanii wetu wanaopambana kwenda kimataifa nadhani wangefika wanapotaka kutokana na sound ya jamaa jinsi ilivyo(au nimefika mbali sana😅).

Anyway, unahisi ni nini shida inayopelekea hawa jamaa wakose support kwa mtaa, ukiachana na sababu ya kuyajenga maisha yao kwenye engo ngumu ya kutokufungamana na mambo mengi ya kijamii ikiwemo ya kisiasa (sijui kama wameshawahi kwenda Dodoma kiuoto wa asili hawa), au sound yao iko mbele ya muda sana?.
Huenda ni wewe hujawapea attention lkn jamaa kila wakitoa single hakun mtz hajui
 
Vanessa anataarifa kwamba Jux kaoa?
Haoni wivu?
Yaan Vee amuonee wivu jux? Km yeye mwenyewe ndo aliamua kutoka, anaumiajee?

Vanessa anakula maisha mambelee, hana muda na mlamba lips.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Tukiongea ule ukweli kabisa hawana uwezo wanafanya mziki kitajiri , kiufupi hata wanachoimba hakisikiki . Mfumo wa mziki wanaoimba ni nchi kama Jamaica ila jamaa hawana mashairi mazuri labda wakaimbie matajiri na watalii .

Unataka kusema nyimbo gani wameimba hata kiitikio kikabamba ? Kiufupi wanachanganya lugha kama sio watanzania , sikiliza ile nyimbo yao kamatia chini 😀...John makini anapiga hizo za Jamaica sana ila anaelekewa sauti inatoka kabisa ila hao wenzetu hata kiswahili hakieleweki.

Uwezo mdogo , angalia beat aliyoipiga Nahrel kwenye nyimba ya weusi ''gere'' ila bado weusi wameimba wakasikika ndani ya beat yenye nguvu ila wao binafsi na mkewe beat ikiwa juu wanatafuna maneno : Mfano kwenye kamatia chini na ile walioimba na Diamond.
Kamatia Chini, hii ilibamba na iliuza vibayaa.
 
Sema mie huwa napenda life style yao, wasanii wengine waliokuwa wanaendana na hawa ni Vanessa na Jux.

Vanessa nae alikuwa na uimbaji fulani wa kuvutia sana.
1. Wet ft Gnako
2. Niroge
3. Me and you
4. Bambino
[emoji91][emoji91][emoji91]
Never ever
Nobody but me Ft KO.

hizi ziko ki international. [emoji91][emoji91][emoji91]
 
Never ever
Nobody but me Ft KO.

hizi ziko ki international. [emoji91][emoji91][emoji91]
Naona wamewatrndisha sana mtandaoni hatimaye juzi wakaalikwa na kutokea kwenye camera. Ila ukiwaangalia ni kama hawako comfortable.
955EAFE2-6323-4282-B4EE-DAAF12FF2553.jpeg
 
wabongo hawapendi nyimbo zenye mbwembe za kiingereza kingi, wanataka kiswahili zaidi.
hiyo style yao ya ki mamtoni ukiiendekeza bongo flevani utakufa njaa. ni vyema wangebadilika kwa baadhi ya nyimbo kama walivyofanya vee money na shaa wakasogea kidogo.
 
wabongo hawapendi nyimbo zenye mbwembe za kiingereza kingi, wanataka kiswahili zaidi.
hiyo style yao ya ki mamtoni ukiiendekeza bongo flevani utakufa njaa. ni vyema wangebadilika kwa baadhi ya nyimbo kama walivyofanya vee money na shaa wakasogea kidogo.
Wanajua wanachokifanya mkuu, ndo maana hawabadiliki. Nadhani toka nimewafahamu wananyimbo nne pekee zilizokaa kiswahili swahili tu kuna ile ngoma yao kwanza kabisa kama Navy Kenzo inaitwa Chelewa aka Bokodo, Moyoni, Cheza kizembe na Usinibwage. Mikwaju mingine yote baada ya hapo ni kule mbele wanakokujua wenyewe na tunaoelewa kazi zao.
 
Nahreel alikuwa anaachia mikwaju sana
Sisi tuliowahi kupitizia hizi kazi ndiyo tunaelewa

Zile beat zilikuwa kama mambele yaani ilikuwa mzuka sana ile nusu nusu ni beat moja ya viwango sana na don't bother na nyingine nyingi hasa za joh makini

Ila joh tamaa ilimponza akaenda switch rec huko akaishia kupuyanga tu mpaka leo anaruka ruka tu
Kuna interview moja niliwahi kumsikia Nahreel akiadmit kuwa audio production hailipi, yaani watu hawalipi wanachukulia poa tu na wakilipa ni kile wanachojisikia, hapo ndipo alipoamua kuweka bei na mkataba wa malipo kuwa ili akutengenezee mdundo sharti ulipe Tsh 1mil. Hapo ndipo wasanii karibu wote aliokuwa anafanya nao kazi walikimbia wakiwemo na hao washkaji wake wa Weusi hasa Joh.
 
Back
Top Bottom