Hivi kwanini Nyerere aliidhinisha kunyongwa Mwamwindi?

Hivi kwanini Nyerere aliidhinisha kunyongwa Mwamwindi?

Mwamwindi alikuwa ni BEBERU..! Hivi leo Mo akihukumiwa kunyongwa kwa kosa la kuua jiwe si atasaini hiyo hati hata saa tisa usiku na atavuta mtego yeye mwenyewe? Mabeberu ni wa kunyonga na kuteka tu..
 
Huyu jamaa kwangu bado ni shujaa sana lakini najiuliza hao wanaotaka kumpa Mwalimu utakatifu wanatumia vigezo gani ilhali mtu alikua ana sign hati za vifo?

Acha kuingilia dini mkuu, Daudi akiwa mfalme alipigana vita na kuua mamia kwa maelfu, lakini ni mtakatifu, Kadhalika wafalme wengi tu waliomfuata, hata Musa aliua watu pale bahari ya shamu, lakini ni mtakatifu. Mifano ipo mingi kwenye Quran na Biblia

Changia mada, acha kuingilia dini za watu mkuu.
 
Kwani hata kama angechelewa kusaini hati si lazima angenyongwa tuuu, tena afadhali alivowahi kuliko angechelewa maana mtu angekuwa anaishi na stress za kusubiri kunyongwa.
 
Mwisho; Nahisi Mtoa maada hana ushahidi na uthibitisho kwa aliyoyaandika!
Raisi na Idara zilizokuwa chini yake zina utaratibu wake wa kufanya kazi.
ASISIKIE STORI ZA VIJIWENI AMBAZO MARA NYINGINE HAZINA UKWELI.
Asante kwa mchango wako mkuu. Haina maana kwamba baada ya hukumu tu Mwamwindi alinyongwa. Bilashaka kuna taratibu nyingine nyiingi zilifuatwa baada ya hapo(sina hakika na suala la rufaa kwa vile alikiri mwenyewe maana kwenye murder rufaa ni automatic)

Inawezekana ilichukua muda hata wa miaka kadhaa kabda ya kutekelezwa hukumu hiyo kutokana na taratibu hizo. Suala ninalouliza na ambalo ni mashuhuri sana katika duru za historia japo sio za kuandikwa ni kwamba katika hati za kunyongwa ambazo Mwalimu alizi sign bila kujiuliza miongoni mwao ni hiyo ya Mwamwindi, hata kama adhabu ilikuja kutekelezwa miaka kadhaa baada ya hukumu

Kusema kwamba nikuletee takwimu za nani alinyongwa lini baada ya hukumu ni kuufifisha mjadala kwa sababu unajua kabisa kwamba siwezi kuwa nazo.

Humu JF hatujuani lakini inawezekana kabisa kuna watu wamo humu waliwahi kuhudumu katika maeneo ambayo wanaweza wakawa source ya kutupa historia ya nini hasa kilichoendelea kitu ambacho huwezi kupata katika kitabu chochote kilichoandikwa. Na wanafanya hivyo bila kutakiwa kutoa majina au utambulisho wao
 
Kwani hata kama angechelewa kusaini hati si lazima angenyongwa tuuu, tena afadhali alivowahi kuliko angechelewa maana mtu angekuwa anaishi na stress za kusubiri kunyongwa.
Kuna watu wengi tu ambao haku sign hati zao za kunyongwa na mwisho wa siku adhabu zao zikabadilishwa na kua vifungo vya maisha, japo kwangu mimi naona kifungo cha maisha ni adhabu ya kikatili sana kuliko watu wengi wanavyofikiria
 
Mahakama ndo ilioamua anyongwe baada ya kumkuta na hatia..Nyerere hausiki hapo
Mahakama ikishatoa hukumu ya kunyongwa ile forn hupelekwa kwa rais akikubali kuisaini tuu ndo hukumu ya kitanzi ni hapo hapo na rais akikataa kuisaini tuu kinyongo cha mnyongwaji hupuga dang'adang'a ila anakuwa ameshikiliwa hadi hapo kesi watakapoamua tena
 
Nenda jukwaa la Historia pale kuna uzi umeelezea vzr sana majibu ya hayo maswali yako yote, kuna sehem inasema mwalimu alimwambia mwammindi ajutie hta kdgo kile alichokitenda ili asiweke sign anyongwe, lkn mwammindi kile kitendo cha kumuua kileruu hakukijutia cku zote mpka ananyongwa
 
Mie bubafsi siioni hoja ya kutuletea humu jf tujadili kwa sababu za msingi zifuatazo;
1. Anaposema nyerere alisaini hukumu ya kifo cha mwamwindi haraka.
- mtoa maada anaposema haraka, ana taarifa Ni siku ngapi Nyerere alisaini toka pale alipohukumiwa. Na anafikiri ingesainiwa siku ngapi baada ya hukumu kutolewa?
- je mtoa maada anajua kipindi ambacho Ni lazima Raisi awe amesaini hukumu ya kifo baada ya hukumu kutoka mahakamani?
- je mtoa maada ana taarifa za wengine ambao raisi aliwahisha au kuchelewesha kusaini hati zao za hukumu za kifo.
Swali kwa mtoa maada!
- Nyerere alisaini hukumu ya mwamwindi ya kifo baada ya siku ngapi tangu kuhukumiwa ili ilinganishwe kama iliwahishwa au kucheleweshwa!
- Mwamwindi alinyingwa siku ngapi baada ya Nyerere kusaini hati yake ya hukumu ili tujilidhishe kuwa aliwahisha!
Mwisho; Nahisi Mtoa maada hana ushahidi na uthibitisho kwa aliyoyaandika!
Raisi na Idara zilizokuwa chini yake zina utaratibu wake wa kufanya kazi.
ASISIKIE STORI ZA VIJIWENI AMBAZO MARA NYINGINE HAZINA UKWELI.

Mkuu mm haoa nakuona umekuja kutuonyesha kwamba ww ni timu kujua....ukiambiwa ilisainiwa haraka inamanisha iliwaishwa pengine kuliko kesi nyingine za wauwaji kama huyo Mwamwindi....Maswala ya siku ngapi Unajua ww.
 
Huyu jamaa kwangu bado ni shujaa sana lakini najiuliza hao wanaotaka kumpa Mwalimu utakatifu wanatumia vigezo gani ilhali mtu alikua ana sign hati za vifo?
Sema kifo sio vifo maana ktk kukaa madarakani zaidi ya miongo mitatu aliasing hati ya kifo moja tu ya huyo mwammwindi. Usiniulize Mzee Ruksa alisaini ngapi kwa kipindi chake cha miaka kumi
 
Kuna suala jingine, kuna kitu kinaitwa extra judicial killings, viongozi wengi wa Kiafrika inawezekana wakawa hawaonekani kwamba wana idhinisha hati za hukumu za vifo kwa waliohukumiwa adhabu hiyo lakini wameua sana katika mauaji yasio ya kisheria, kimyakimya
Sio viongozi wa Kiafrika tu, hivi unadha huko, kwa weupe ni nchi za zote hazina adhabu hii ya kunyonga.

Marekani mpaka leo adhabu hii ipo, na watu wananyongwa sana msione kimya.
 
Back
Top Bottom