Hivi kwanini Nyerere aliidhinisha kunyongwa Mwamwindi?

Hahaha hii mada kila mara inajadiliwa humu, hata sijui kwanini.
 
Mwamwindi alikuwa ni BEBERU..! Hivi leo Mo akihukumiwa kunyongwa kwa kosa la kuua jiwe si atasaini hiyo hati hata saa tisa usiku na atavuta mtego yeye mwenyewe? Mabeberu ni wa kunyonga na kuteka tu..
 
Huyu jamaa kwangu bado ni shujaa sana lakini najiuliza hao wanaotaka kumpa Mwalimu utakatifu wanatumia vigezo gani ilhali mtu alikua ana sign hati za vifo?

Acha kuingilia dini mkuu, Daudi akiwa mfalme alipigana vita na kuua mamia kwa maelfu, lakini ni mtakatifu, Kadhalika wafalme wengi tu waliomfuata, hata Musa aliua watu pale bahari ya shamu, lakini ni mtakatifu. Mifano ipo mingi kwenye Quran na Biblia

Changia mada, acha kuingilia dini za watu mkuu.
 
Kwani hata kama angechelewa kusaini hati si lazima angenyongwa tuuu, tena afadhali alivowahi kuliko angechelewa maana mtu angekuwa anaishi na stress za kusubiri kunyongwa.
 
Mwisho; Nahisi Mtoa maada hana ushahidi na uthibitisho kwa aliyoyaandika!
Raisi na Idara zilizokuwa chini yake zina utaratibu wake wa kufanya kazi.
ASISIKIE STORI ZA VIJIWENI AMBAZO MARA NYINGINE HAZINA UKWELI.
Asante kwa mchango wako mkuu. Haina maana kwamba baada ya hukumu tu Mwamwindi alinyongwa. Bilashaka kuna taratibu nyingine nyiingi zilifuatwa baada ya hapo(sina hakika na suala la rufaa kwa vile alikiri mwenyewe maana kwenye murder rufaa ni automatic)

Inawezekana ilichukua muda hata wa miaka kadhaa kabda ya kutekelezwa hukumu hiyo kutokana na taratibu hizo. Suala ninalouliza na ambalo ni mashuhuri sana katika duru za historia japo sio za kuandikwa ni kwamba katika hati za kunyongwa ambazo Mwalimu alizi sign bila kujiuliza miongoni mwao ni hiyo ya Mwamwindi, hata kama adhabu ilikuja kutekelezwa miaka kadhaa baada ya hukumu

Kusema kwamba nikuletee takwimu za nani alinyongwa lini baada ya hukumu ni kuufifisha mjadala kwa sababu unajua kabisa kwamba siwezi kuwa nazo.

Humu JF hatujuani lakini inawezekana kabisa kuna watu wamo humu waliwahi kuhudumu katika maeneo ambayo wanaweza wakawa source ya kutupa historia ya nini hasa kilichoendelea kitu ambacho huwezi kupata katika kitabu chochote kilichoandikwa. Na wanafanya hivyo bila kutakiwa kutoa majina au utambulisho wao
 
Kwani hata kama angechelewa kusaini hati si lazima angenyongwa tuuu, tena afadhali alivowahi kuliko angechelewa maana mtu angekuwa anaishi na stress za kusubiri kunyongwa.
Kuna watu wengi tu ambao haku sign hati zao za kunyongwa na mwisho wa siku adhabu zao zikabadilishwa na kua vifungo vya maisha, japo kwangu mimi naona kifungo cha maisha ni adhabu ya kikatili sana kuliko watu wengi wanavyofikiria
 
Mahakama ndo ilioamua anyongwe baada ya kumkuta na hatia..Nyerere hausiki hapo
Mahakama ikishatoa hukumu ya kunyongwa ile forn hupelekwa kwa rais akikubali kuisaini tuu ndo hukumu ya kitanzi ni hapo hapo na rais akikataa kuisaini tuu kinyongo cha mnyongwaji hupuga dang'adang'a ila anakuwa ameshikiliwa hadi hapo kesi watakapoamua tena
 
Nenda jukwaa la Historia pale kuna uzi umeelezea vzr sana majibu ya hayo maswali yako yote, kuna sehem inasema mwalimu alimwambia mwammindi ajutie hta kdgo kile alichokitenda ili asiweke sign anyongwe, lkn mwammindi kile kitendo cha kumuua kileruu hakukijutia cku zote mpka ananyongwa
 

Mkuu mm haoa nakuona umekuja kutuonyesha kwamba ww ni timu kujua....ukiambiwa ilisainiwa haraka inamanisha iliwaishwa pengine kuliko kesi nyingine za wauwaji kama huyo Mwamwindi....Maswala ya siku ngapi Unajua ww.
 
Huyu jamaa kwangu bado ni shujaa sana lakini najiuliza hao wanaotaka kumpa Mwalimu utakatifu wanatumia vigezo gani ilhali mtu alikua ana sign hati za vifo?
Sema kifo sio vifo maana ktk kukaa madarakani zaidi ya miongo mitatu aliasing hati ya kifo moja tu ya huyo mwammwindi. Usiniulize Mzee Ruksa alisaini ngapi kwa kipindi chake cha miaka kumi
 
Sio viongozi wa Kiafrika tu, hivi unadha huko, kwa weupe ni nchi za zote hazina adhabu hii ya kunyonga.

Marekani mpaka leo adhabu hii ipo, na watu wananyongwa sana msione kimya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…