Hivi kwanini Tanzania hakuna programmers

Usiseme hawapo ni wewe ndiyo hujakutana nao. It seems cycle yako nzima hakuna competent programmer ndo ukafikia hiyo conclusion. Once nilikuwa na mawazo kama yako but niliwahi kushiriki kwenye uzi mmoja humu ndo nikajuwa asee tuna watu hapa Tanzania wako vizuri kinoma kwenye programming.
Keep an open mind brother.
 
Kulingana na ubongo wa mtu, mtoto anaweza kujifunza akashindwa kwa ugumu wake lakini mtu mzima akaweza... Au ikawa vise versa yake...
Kitu kikianzia utotoni huwa kinakaa vizuri. Programmers wengi walioleta mapinduzi kama kina Mark Zuckerberg walianzia chini kabla ya kuingia chuo.
 
Kitu kikianzia utotoni huwa kinakaa vizuri. Programmers wengi walioleta mapinduzi kama kina Mark Zuckerberg walianzia chini kabla ya kuingia chuo.
Kwa sisi huku ni ngumu... Labda kwa sasa hivi kidogo afadhali tumeendelea ukilinganisha na wao... Imagine wao mtoto mwenye miaka 7 anamiliki simu janja na wengine kwenda nazo shule... Sasa ukitaka iwe hivyo kwetu itakuwa sio
 
Kwa sisi huku ni ngumu... Labda kwa sasa hivi kidogo afadhali tumeendelea ukilinganisha na wao... Imagine wao mtoto mwenye miaka 7 anamiliki simu janja na wengine kwenda nazo shule... Sasa ukitaka iwe hivyo kwetu itakuwa sio
Kuna sehemu niliwahi kuona kwenye mitandao wanawafundisha watoto CODING hapa hapa Bongo sema ni sehemu za kishua sio kwa wavunja kuni.
 
Kwasababu hawapo.
 
Utofauti wa programmer, developer,software engineer ni nini?
Programmer ni mtu anaeandika seti ya maelezo yanayoiambia computer nini ifanye kwa kutumia programming language (au mtu anayeandika program),

developer ni mtu ambaye anauelewa na fani fulani katika teknolojia aidha kwa maendeleo ya wavuti, systems, software designing etc. na anaweza kutoa mchango fulani katika kuboresha program au system fulani.

Software engineer ni mtu anayedesign software na kuifanya, mfano akadesign software kama mobile app, au web application, na anauwezo wa kuifanyia repair and advancement. Hawa wao wanadeal na softwares tu.

Kwa ujumla watu hawa watatu wote wanatakiwa kuwa na ujuzi wa programming au kuandika program. (Programming ni msingi wa software engineering. Hivyo basi, programmer ni software engineer lakini pia ni developer
 
Causes of poverty???? ENZI ZILE SASA MAJIBU YA KUKARIRI KILA FANI YALIKUWA NI
LACK OF CAPITAL
LACK OF TECHNOLOGY
 
Lectures wenyewe wako vizuri... Hapo bado hujawagusa wanaojifunza kila siku hawana kazi nyigine wao ni kujifunza tu
 
Nitajie Lugha zinazoingia kwenye Coding
Zipo nyingi, kuna Python, JavaScript, Java, C++, C#, PHP, Ruby, Kotlin, pia HTML na CSS Lakini hizi wanaziterm kama Structuring languages au markup language kwa ajili ya kudesign web interfaces
 
Yaan kwa ninavyoelewa, coding ni part ya programming, programming inajumuisha kuanzia utambuzi wa tatizo mpaka mtu anamaliza kuandika program ya kutatua hilo tatizo, kwahiyo ndani yake kuna kipengele cha coding (write a program) ambayo huwa ni hatua ya 3 katika hatua za kudevelop a program
 
Kwanini usiconnect direct bila http proxy mkuu?
 
Project kufika mbali au kutokufika mbali sio tatizo la programmers ila mazingira shawishi bado hayawekwa kwaajiri ya watu wenye good ideas kuwakilisha of coz buni ipo ila bado haihamasishi kiasi hiko.

And kwenye kipengele cha copy and pesting hii ni skills ambayo kila programmer mwenye akili timamu duniani anakua nayo coz sheria namba moja ya programming Google is your best friend and second make sure unacode kitu ambacho hakijawahi kusolviwa anywhere but kama problem unayoicode ilishawahi kusolviwa somewhere why upoteze muda kujichosha kuandika codes while ukiingia stack overflow unakuna snippets zipo? The goal ni kumake sure end results inatokea kama inavyotakiwa na code zimeandikwa katika mfumo unaoeleweka yaani ile flow inaonekana vizuri.

NB: Kitendo cha kujua tu code ipi nikiicopy nikiiweka sehemu hii nitapata result ninayo ihitaji basi wewe tayari ni programmer.
 
Nenda kwenye File -> settings ->appearance &behavior ->system settings -> http proxy then click kwenye sehemu iliyoandikwa no proxy then bonyeza OK kisha build project yako uone kama bado inaleta error icopy hiyo error ipest hapa tuione.
 
Programmers wapo ila hakuna software industry so hakuna sababu ya kulundikana ni kutafuta unemployment.

Kuna NALA nadhani unaijua ilianza hapa wakakimbilia Kenya, kuna Ramani, kuna ile software ya POS siikumbuki jina, najua kuna software za kufanya reconciliation benki ni za bongo, kulikuwa na app ya kununua tiketi za maonyesho/matamasha etc kuna wakati Voda walikuwa na mashindano ya kuandika apps walikuwa wengi tu, ila industry haikushika moto kwa vile nchi yetu ni ngumu, nina wasiwasi ni too late now.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…