Hivi kwanini ukimueleza mtu mafanikio yako anakasirika?

Hivi kwanini ukimueleza mtu mafanikio yako anakasirika?

Bwana kazanazo watu wanalalamika eti mafuta ni ghari sana, mimi sijui sasa nikasema ngoja nijionee mwenyewe, nikaenda kuweka mafuta na msaidizi wangu, kuangalia receipt hata dola Mia mbili haifiki, nilishangaa sana nikamuuliza msaidizi wangu sasa hawa watu wanalalamikia nini
Ila yamepanda kweli mkuu😀
 
Kuongea mafanikio ndio kuji-proud mbona tafsiri inakuwa hivyo!
Mkuu,
Mpaka hapa ilitakiwa uwe umesha pata jibu na sio kuendelea kubishana na wachangiaji,

Umeshajua kua hao watu wako hawapendi uwaelezee mafanikio yako,sasa kwanini uendelee kuwaelezea mafanikio yako?

Acha kuwaelezea mafanikio yako hao watu wako au badilisha marafiki,hao sio marafiki/watu wema kwako.
 
Ni kweli mafanikio yako inabidi yawe Siri ,

Ukitaka kuongeza maadui tangaza mafanikio yako au malengo yako

Binadamu wame umbiwa mashindano kila mtu anataka awe juu ya mwenziye

Tunza Malengo yako uta tunza Amani yako.
Kwanini jamii imejengwa kwa fikra kama hizo
 
Kwanini shida sio tatizo kwahiyo watu tuwe na shida tu muda wote
Una umri gan kijana? .mbona kama bado unabalehe? Hiv hii hesabu si ndogo kabisa kwa mtu mzima mwenye akili fimamu?

Kama mtu ukimuelezea raha zako anafurahi, ukimueleza shida zako si atahuzunika? Je nn kitatokea endapo itakuwa vice versa? Hapo jibu hupati hata kama huna digrii mathalan
 
Mkuu,
Mpaka hapa ilitakiwa uwe umesha pata jibu na sio kuendelea kubishana na wachangiaji,

Umeshajua kua hao watu wako hawapendi uwaelezee mafanikio yako,sasa kwanini uendelee kuwaelezea mafanikio yako?

Acha kuwaelezea mafanikio yako hao watu wako au badilisha marafiki,hao sio marafiki/watu wema kwako.
Bado sijapata jibu zaidi naona hata wachangiaji ni sawa na marafiki zangu wote hawataki kuambiwa mafanikio ya mtu zaidi ya shida, swali ni kwanini jamii imejengeka namna hiyo
 
Hii ni hatari sana kwa kweli yaani usijaribu
Mimi nilianza kufuga kuku 100 wake delea kuongezeka Hadi tukuku mia mbili alipo jua tu amegoma kuniuzia chakula kwakweli mafanikio hata yawe madogo kiasi Gani furahia peke Yako tu
 
Bado sijapata jibu zaidi naona hata wachangiaji ni sawa na marafiki zangu wote hawataki kuambiwa mafanikio ya mtu zaidi ya shida, swali ni kwanini jamii imejengeka namna hiyo
Ukiuliza swali "Ni kwanini jamii imejengeka hivyo?"

Mwingine atauliza Kwanini watu wanatapeli wenzao? Kwanini watu wanakula rushwa? Kwanini watu wanaiba mali za uma? Kwanini kuna Wanawake wanajiuza?

Hizo ni hulka za Binadamu tu,sio Binadamu wote watachukia mafanikio ya mtu mwingine,

Huwezi kumbadili binadamu tabia yake ikiwa yeye mwenyewe hayupo tayari kubadilika,

Kama umejua kua watu hawapendi ukiwaelezea mafanikio yako,acha kuwaelezea, simple tu,

Usipoelewa na hapa basi utakua na tatizo kubwa ambalo wewe mwenyewe hujalijua bado.
 
Mafanikio hayana kipimo ila kila mtu na mafanikio yake kulingana na malengo aliyojiwekea

Sasa jamii yetu ya kibongo ukimuelezea mtu mafanikio yako yawe makubwa au madogo hujawa na makasiriko na laana juu, kwanini?

Mara ooh! Pesa ni za shetani tafuta ufalme wa Mungu, mara sijui pesa kazipata kwa magendo na njia za mkato alooh!!!?
Zaidi ninyi weusi, mnakuwa weusi mpaka wa roho🤣
 
Hii ni hatari sana kwa kweli yaani usijaribu
Mimi nilianza kufuga kuku 100 wake delea kuongezeka Hadi tukuku mia mbili alipo jua tu amegoma kuniuzia chakula kwakweli mafanikio hata yawe madogo kiasi Gani furahia peke Yako tu
Ukimuuliza hawezi kuwa na sababu ya msingi ya kuchukia maendeleo yako
 
Mafanikio hayana kipimo ila kila mtu na mafanikio yake kulingana na malengo aliyojiwekea

Sasa jamii yetu ya kibongo ukimuelezea mtu mafanikio yako yawe makubwa au madogo hujawa na makasiriko na laana juu, kwanini?

Mara ooh! Pesa ni za shetani tafuta ufalme wa Mungu, mara sijui pesa kazipata kwa magendo na njia za mkato alooh!!!?
Ukitaka akufurahie mweleze mafanikio yako huku ukionesha kuwa na yeye atanufaika na mafanikio yako.

Hebu tuulizane, nini lengo la kumueleza mtu mafanikio yako ikiwa hata hanufaiki na wewe na unakuta ana njaa! Je, ni kumrusha roho au kumuhamasisha?

Kwa mfano ukisema, aisee mwaka jana nimefanikiwa kufanya 1,2,3 na wewe naweza kukusaidia katika 1,2,3 unahisi kuna mtu atakasirikia mafanikio yako? Sasa wewe ni kujitapa tu mbele ya maskini kwa kuonesha mafanikio yako lakini ukiombwa msaada hutaki! Kwani ukikaa kimya na mafanikio yako kuna shida gani huku watu wakiona vitendo tu?
 
Tazamia unamweleza naaani au na wewe una wenge la mafanikio yako ko kila mtu unaona
ni wa kumwambia tuu!!!?
Mwamba au haujatoka badoo!
 
Back
Top Bottom