Hivi kwanini wahitimu wa Udom wanapata ajira sana

Hivi kwanini wahitimu wa Udom wanapata ajira sana

Mujumba

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2011
Posts
853
Reaction score
306
Niseme tu wazi mimi nimesoma UDSM, Ila sifurahishwi na jinsi ambavyo wahitimu wa udom wanavyopewa upendeleo ktk soko ajira kwasasa kuliko vyuo vingine au upendeleo?

Hivi karibuni nilikuwa nchini Botswana na Korea, nilibahatika kukutana na vijana wa Kitanzia wanaofanya kwenye mashirika ya USAID na UN respectively, kwenye maongezi yetu nikawahoji mmesoma vyuo gani wakasema Udom.

Nilishtuka sana maana sikutegemea chuo kipya kama hiki kinaweza kutoa graduates makini, wakaniambia tatizo Tz tumekariri kwamba kusoma chuo fulani basi wewe ndio unajua kumbe waajiri wanaangalia competency.

Pia juzi kulikuwa na interview ya kazi kwenye ofisi zetu katika vijana 24 waliokuwa shortlisted kwa ajiri ya Oral 9 walikuwa UDOM, 5 udsm, 5 SAUT, 3 IFM, MZUMBE 1, MUCCOBS 1, na waliofanikiwa kupata ajira na wanaripoti kazini jumatatu ni watano, udom 3, saut 1 na Muccobs 1.

Wale wazungu waliokuwa wakifanya interview walisifu sana uwezo wa vijana wa udom.

Pia nimesikia watu wakilalamika kuwa si kweli udom wapo vizuri bali wanapendelewa tuu ili kuuza jina la chuo, je haya madai ni ya kweli wadau?
 
Unamfahamu Dr. Goebble? alikuwa waziri wa habari wa Germany wakati wa Hitler, Naye alikuwa anapost thread kama hizi.
 
Nani alijua kwamba Azam inaweza kuwa timu bora kuliko Simba na Yanga? Sasa hivi waajiri hawa angalii mbwe mbwe wanaangalia utendaji kazi, nidhamu na uwezo. Wewe kaa kujisifu kuwa umesoma chuo kikuu kikongwe kumbe huna competence kama utadaka ajira labda baba yako au kwenye NEC
 
niseme tu wazi mimi nimesoma UDSM, Ila sifurahishwi na jinsi ambavyo wahitimu wa udom wanavyopewa upendeleo ktk soko ajira kwasasa!
hivi karibuni nilikuwa nchini Botswana na Korea, nilibahatika kukutana na vijana wa Kitanzia wanaofanya kwenye mashirika ya USAID na UN respectively, kwenye maongezi yetu nikawahoji mmesoma vyuo gani wakasema Udom nilishtuka sana maana sikutegemea chuo kipya kama hiki kinaweza kutoa graduates makini, wakaniambia tatizo Tz tumekariri kwamba kusoma chuo fulani basi wewe ndio unajua kumbe waajiri wanaangalia competency.
-pia juzi kulikuwa na interview ya kazi kwenye ofisi zetu katika vijana 24 waliokuwa shortlisted kwa ajiri ya Oral 9 walikuwa UDOM, 5 udsm, 5 SAUT, 3 IFM, MZUMBE 1, MUCCOBS 1, na waliofanikiwa kupata ajira na wanaripoti kazini jumatatu ni watano, udom 3, saut 1 na Muccobs 1
-wale wazungu waliokuwa wakifanya interview walisifu sana uwezo wa vijana wa udom
-pia nimesikia watu wakilalamika kuwa si kweli udom wapo vizuri bali wanapendelewa tuu ili kuuza jina la chuo, je haya madai ni ya kweli wadau??

uongo unakusaidia nini mkuu?
 
FRANSIS THE DON mbona wanakupinga ulisema ulikuta masharti ili uajiriwe sharti usiwe umemaliza udom? nani muongo?
 
Last edited by a moderator:
Nani alijua kwamba Azam inaweza kuwa timu bora kuliko Simba na Yanga? Sasa hivi waajiri hawa angalii mbwe mbwe wanaangalia utendaji kazi, nidhamu na uwezo. Wewe kaa kujisifu kuwa umesoma chuo kikuu kikongwe kumbe huna competence kama utadaka ajira labda baba yako au kwenye NEC
 
Udom wako vema sana...kama huamini nenda World Vision..USAID..KOICA..ofisi ya waziri mkuu na n.k...uulizie utendaji wao...nyie endeleeni kubaki na majina ya vyuo kwa sifa za enzi za mwalimu
 
Huu ni uongo wa wazi wazi...na kujitangazia udhaifu wako mleta uzi.
 
niseme tu wazi mimi nimesoma UDSM, Ila sifurahishwi na jinsi ambavyo wahitimu wa udom wanavyopewa upendeleo ktk soko ajira kwasasa!
hivi karibuni nilikuwa nchini Botswana na Korea, nilibahatika kukutana na vijana wa Kitanzia wanaofanya kwenye mashirika ya USAID na UN respectively, kwenye maongezi yetu nikawahoji mmesoma vyuo gani wakasema Udom nilishtuka sana maana sikutegemea chuo kipya kama hiki kinaweza kutoa graduates makini, wakaniambia tatizo Tz tumekariri kwamba kusoma chuo fulani basi wewe ndio unajua kumbe waajiri wanaangalia competency.
-pia juzi kulikuwa na interview ya kazi kwenye ofisi zetu katika vijana 24 waliokuwa shortlisted kwa ajiri ya Oral 9 walikuwa UDOM, 5 udsm, 5 SAUT, 3 IFM, MZUMBE 1, MUCCOBS 1, na waliofanikiwa kupata ajira na wanaripoti kazini jumatatu ni watano, udom 3, saut 1 na Muccobs 1
-wale wazungu waliokuwa wakifanya interview walisifu sana uwezo wa vijana wa udom
-pia nimesikia watu wakilalamika kuwa si kweli udom wapo vizuri bali wanapendelewa tuu ili kuuza jina la chuo, je haya madai ni ya kweli wadau??

Swali limeka kimkakati zaidi.
 
tatzo watu wanapenda kuish kwa propaganda uchwara, hakuna chuo kscho na mapunguf, lakn kuhusu udom hiv sasa wamepga hatua kubwa sana, last year ofisin kwetu tulifanya interview ndio tukajua udom wapo smart sana kuanzia kujieleza kufikir nidham na kiutendaj, tulitoa case study moja then tukawaweka watu ktk makund huez amin udom walikua mstar wa mbele kugundua mbinu zote tulizoweka kujua tulichokua tunaktaka walipokua eneo husika, this year somewhere tumefanya interview pia udom wameonyesha wanatechnics nzur sana wanapopata fursa ya kuajiriwa, tumewajir weng japo wapo na vyuo vngne ila wao ndio wamekua mfano.. wew unaekaa kupga porojo kuhusu udom endelea
 
Mimi mwenyewe ni product ya Udom, nilipata kazi kwa kuwashinda hao graduates mnaosema wanatoka vyuo vikongwe, ngoja niwambie kwa sasa kinachohitajika kwenye taasisi nyingi ni unajua nini na sio umesoma wapi, chuo hakimbebi mtu bali yeye mwenyewe
 
Mkuu kama ulikuwa Korea kuna washkaji wengi wako pale toka Udom, kuna wengine wameajiliwa kama wahadhiri na wanajiendeleza kimasomo.
 
Back
Top Bottom