Hivi kwanini Wakenya walikataa kuungana na Tanzania ??

MALCOM LUMUMBA

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2012
Posts
21,113
Reaction score
65,124
Habari wakuu,
Hivi kwanini ndugu zetu Wakenya walimkatalia Hayati Mwalimu Nyerere kuunganisha Afrika Mashariki ??? Kikubwa zaidi alikubali kabisa kwa moyo mweupe Uraisi apewe Hayati Mzee Jomo Kenyatta, lakini kwanini mlikataa na miaka ya hivi karibuni mlikuja kuanza kupigia debe Shirikisho la Afrika Mashariki ???

Naomba nipate maoni na mtizamo wa Wakenya katika hili,
Naambatanisha hii video kahusiana an hili.

CC: JokaKuu
 
Kikubwa mkuu ni ulafi na ubinafsi wa Mzee Jommo Kenyatta na watu wake waliomzunguka. Alijua Nyerere atakuwa kikwazo kikubwa cha yeye na watu wake kujilimbikizia mali kama alivyofanya, alijua Nyerere ni muungwana sana hapendi dhuluma wakati yeye alipanga kuwauwa wale wote ambao walionekana kutishia utawala wake, na kweli aliwamaliza, kuanzia wenzake aliopigana nao vita vya mao mao hadi wasomi akina Tom Mboya,

Pia kwa sababu waingereza waliijenga sana Kenya Kuliko Tanzania kwa wakati ule wakenya wengi hawakutaka kushirikishwa umasikini na Tanzania, si unaelewa siasa na uchumi wa kibepari ulivyo, ni maslahi tu ndiyo yanayochagua rafiki, sasa hivi ukiona Kenya wanataka sana kuungana ujue kuna maslahi kwao, si vinginevyo, kumbuka Kenya ni "man eat man society"
 
Kumbe sababu ni:
1. Hofu ya Mwalimu Nyerere
2. Kulinda maslahi ya kikabila
3. Umasikini wa Tanzania

Sasa najiuliza maswali haya
1. Kwani sasa hivi Tanzania Umaskini umeisha ???
2. Kwani Kenye ukabila umeisha ???

Mbona wanang'ang'ania sana kuungana na Watanganyika na Wazanzibar ???
Unakumbuka kipindi cha Coalition of the Willing walitupa maneno kama The Laggard of East Africa mara Xenophobic.
Naumiza kichwa kutaka kujua kwanini muungano walioukataa Baba zao wenyewe wao wanataka kuulazimisha kwetu ???
 
Waliogopa kuwa koloni letu kama Zanzibar, sasa hivi zanzibar hawawezi kujitoa tena usicheze na ccm wewe
 
Hivi kweli Tanganyika ilikuwa hata na nguvu ya Kuifanya Kenya Koloni lake ndani ya Mfumo wa Shirikisho kweli ???
Haingii akilini kabisa na hata ukiangalia vizuri Mwalimu Nyerere alipendekeza huu Muungano hata kabla ya Tanzania kuwepo
 
Kwani Zanzibar tuliichukua kwa nguvu tulitumia mdomo tu, sisi hata kupata uhuru tulitumia mdomo tu
 
Kumbe sababu ni:
1. Hofu ya Mwalimu Nyerere
2. Kulinda maslahi ya kikabila
3. Umasikini wa Tanzania

Sasa najiuliza maswali haya
1. Kwani sasa hivi Tanzania Umaskini umeisha ???
2. Kwani Kenye ukabila umeisha ???

Mbona wanang'ang'ania sana kuungana na Watanganyika na Wazanzibar ???
Unakumbuka kipindi cha Coalition of the Willing walitupa maneno kama The Laggard of East Africa mara Xenophobic.
Naumiza kichwa kutaka kujua kwanini muungano walioukataa Baba zao wenyewe wao wanataka kuulazimisha kwetu ???
Kama ungesoma vizuri jibu langu la awali ungeelewa, yeye alitaka kujimilikisha mali na watu wake wa karibu, hilo alifanikiwa, leo hii watu wote aliokuwa karibu nao ni mtajiri wa kutupwa, pili alitaka kuhakikisha wapinzani wake wakubwa katika kuimarisha utawala wa kikabila anawamaliza na kuhakikisha nchi inakuwa na tabaka za kiuchumi na kikabila, hilo pia amefanikiwa, sasa hivi kama sio Mkikuyu, Kalenjin, Mjaluo au Mkamba, wala usijaribu hata kuchukuo form ya kugombea urais Kenya.

Sasa hivi Tanzania inafursa nyingi sana za kiuchumi kuliko Kenya, kumbuka Kenya ni nchi ndogo na ardhi kubwa ni jangwa, na hiyo ndogo yenye rutuba waligawana yeye Jommo Kenyatta na watu wake, kuingezeka kwa idadi ya watu Kenya, kunaifanya Kenya kutafuta maeneo mengine wakaishi, ni Tanzania pekee kati ya nchi zilizopakana na Kenya ndiko kwenye ardhi kubwa yenye rutuba na usalama wa nchi, na wakisikia kila kukicha kunagunduliwa gas, helium na madini ya kila aina, kunawafanya waitamani sana TZ
 
Hii mada inaweza ikajadiliwa vizuri bila ushabiki na kulaumiana kijinga maana wengi wetu hatukua hata tumezaliwa wakati ule.
Lilikua wazo nzuri, lakini pia muungano ni very complicated, binafsi nimeona mnavyolumbana kwenye kamuungano kenu na Wazanzibari, hivi tungewezaje kumudu huu wa mibabe wawili.
Binafsi nimeishi Zanzibari na pia Tanzania bara, nimeshuhudia tofauti zenu na jinsi kuna wengi sana hawautaki huo muungano wenu, hivyo kwa maoni yangu naona tungeishia full vurugu.
Nitarudi baadaye na analysis iliyotulia, kwa sasa nipo kwemye mikimbio ya kusaka tonge.
 
Hapo nimekuelewa sana mkuu,
Kwa hiyo wanalazimisha Muungano kwasababu wanataka watuletee matatizo yao kwetu!
Basi kweli tuna haki ya kuukataa kabisa kwa nguvu zote tulizonazo.

Halafu swali langu jingine,
Hivi hali ya Udini Kenya ikoje ???
Hivi Kenya ina wakristo wengi sana kihivyo ???
Mbona sijawahi kusikia Raisi, Makamu wa Raisi au Waziri Mkuu Muislamu kama ilivyo hapa Tanzania ???
Naomba nieleweshe mkuu wamewahi kuwepo au ni mimi tu nisiyejua ???
 
Kwanza kumbuka kwamba Kenya ni nchi ya kibepari sana, katika Africa, Kenya inaweza kuongoza kwa kufuata uchumi wenye misingi ya kibepari kuliko nchi zote kusini mwa jangwa la sahara, na ubepari ni unyama kama alivyotuambia Nyerere, kwa hiyo ukimuona bepari yoyote yule anakufuata kwa karibu, ujue lazima anataka kula nyama" man eat man"

Kenya waisilamu ni wachache ukilinganisha na huku Tanzania, sina uhakika kama hata wanazidi 15% ya watu wote, kibaya zaidi hawatoki kwenye hayo makabila makubwa, sidhani kama Kenya wanajali dini, kwao muhimu ni Kabila na zile koo teule, ya Kenyatta na Odinga
 
Hii mada inaweza ikajadiliwa vizuri bila ushabiki na kulaumiana kijinga maana wengi wetu hatukua hata tumezaliwa wakati ule.
Lilikua wazo nzuri, lakini pia muungano ni very complicated, binafsi nimeona mnavyolumbana kwenye kamuungano kenu na Wazanzibari, hivi tungewezaje kumudu huu wa mibabe wawili.
Binafsi nimeishi Zanzibari na pia Tanzania bara, nimeshuhudia tofauti zenu na jinsi kuna wengi sana hawautaki huo muungano wenu, hivyo kwa maoni yangu naona tungeishia full vurugu.
Nitarudi baadaye na analysis iliyotulia, kwa sasa nipo kwemye mikimbio ya kusaka tonge.

Umeonge kiushabiki sana bila kuangalia mambo kitaalamu;
Mosi, tatizo kubwa na la pekee ndani ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ni kuwepo na Mfumo Mbovu usioeleweka.
Haueleweki kama ni nchi moja au shirikisho. Hivyo kama tukiweza kumaliza hili Tatizo bila woga wowote ule basi nakuhakikishia hapa Afrika hakuna Muungano Imara na wenye faida kama ule wa Tanganyika na Zanzibar. Ulichokisikia wewe kule Zenji ni hisia tu ambazo zimejengwa zaidi na mihemko ya Kisiasa na kidini bila kuangalia uhalisi; ni sawa tu na kusema Tanzania kuna Baa la njaa, wengi waliamini na kuhisi kweli wanaumwa njaa kumbe hakuna kitu.

Pili, umesahau kwamba Tanganyika ilipendekeza kuwepo kwa Shirikisho (A Federal Republic) tofauti na Zanzibar ambako Karume alitaka kuwepo na nchi moja tu yenye iliyoungana katika kila kitu. Nadhani mfumo wa Shirikisho la Afrika Mashariki usingekuwa na Maneno mengi sana kwasababu tungeunganishwa tu kwenye mambo muhimu ya Shirikisho chini ya mwamvuli wa FEDERAL COMPACT. Kenya mngekuwa na yenu, vivyo hivyo Tanganyika, Zanzibar na Uganda wangekuwa na yao ya ndani kama nchi wanachama.

NB: Muhimi ni tufanye nini ili turudishe imani baina ya nchi hizi mbili ndugu ???
 
Kwanza kumbuka kwamba Kenya ni nchi ya kibepari sana, katika Africa, Kenya inaweza kuongoza kwa kufuata uchumi wenye misingi ya kibepari kuliko nchi zote kusini mwa jangwa la sahara, na ubepari ni unyama kama alivyotuambia Nyerere, kwa hiyo ukimuona bepari yoyote yule anakufuata kwa karibu, ujue lazima anataka kula nyama" man eat man"

Kenya waisilamu ni wachache ukilinganisha na huku Tanzania, sina uhakika kama hata wanazidi 15% ya watu wote, kibaya zaidi hawatoki kwenye hayo makabila makubwa, sidhani kama Kenya wanajali dini, kwao muhimu ni Kabila na zile koo teule, ya Kenyatta na Odinga

Sawa mkuu,
Kumbe tatizo kuu la kenya ni Ukabila.
Wakitoa huo basi wanaweza kujenga nchi yenye nguvu kuliko hii ya sasa.!

Maswali mengine mawili,
1. Tufanye nini ili kuweza kurudisha imani iliyovunjika baina ya mataifa haya ndugu ya Tanzania na Kenya ???
2. Nini mtazamo wako juu ya Ujio wa Rwanda na Burundi ndani ya Shirikisho la Afrika Mashariki ???
 
Kwanza kumbuka fikra za kuunganisha Afrika nzima zilianzishwa na Kwame Nkurumah na Nyerere, hata kabla ya Tanganyika kupata Uhuru, ila walitofautiana katika muundo wa jinsi gani ya kuungana, wakati Nkurumah, alitaka nchi zote huru wakati ule ziungane kwa pamoja, namkila nchi ikipata uhuru iwe automatikali imejiunga, Nyerere yeye alitaka tuanze kuungana kikanda kwanza, kama vile nchi za Magharibi ziungane kwanza, EAC, na kusini mwa Afrika, baadae hizo blocks ndiyo ziunganishwe, mawazo ya Nyerere ndiyo yaliyokubaliwa na wanachama wengi, ila Nkuruma alionya kwamba, hawa viongozi wa Afrika wakishalewa madaraka itakuwa ngumu sana kuja baadae kuwaambia watoke kwenye viti vyao kwa ajili ya kuunganisha hizi nchi, na ndicho kilichotokea, baada ya nchi nyingi za Afrika kupata Uhuru, viongozi wengi sana walikataa kuunganisha nchi zao japo kwenye kanda kama alivyopendekeza Nyerere, mzee Jommo Kenyatta ni miongoni mwa viongozi waliokataa pamoja na juhudi kubwa za kushawishiwa na Nyerere.

Kwa sasa hivi Kenya ina tatizo kubwa la utaifa, wananchi wenyewe hawana umoja, wamegawanyika sana, na kunauwezekano Kenya ikagawanyika ikawa nchi mbili, is too late kwa sasa Kenya kuwa kitu kimoja, njia pekee japo kuituliza Kenya ni kuwa na muungano kama alivyosema mwalimu Nyerere, kama si Muungano Zanzibar ingekuwa ilishagawanyika kati ya Upemba na Unguja, wazanzibar ni wabaguzi sana, ni sawa na wakenya au wamewazidi wakenya kidogo, kinachowafanya washindwe kuchinjana kama wanavyofanya wakenya, ni kwasabu wapo ndani ya muungano na serikali ya Jamhuri ya Tanzania imewashikilia kwelikweli, lakini pia Tanzania bara inatumika kama mapafu ya kupumua kiuchumi kwa wazanzibar, sheria ya kumiliki ardhi inamkataza mtanzania bara kumiliki ardhi Zanzibar, ila wao wanaruhusiwa kumiliki ardhi huku bara, ndiyo sababu utaona wazanzibar wengi wamejenga majumba na wanamashamba makubwa na wengi ni matajiri huku bara, wasingekuwa na uwezo wa kuja huku bara, ardhi kwao ni ndogo ndiyo ingekuwa chanzo cha wao kupigana

Tungeweza kuwasaidia wakenya kwa kuwaruhusu waje kumiliki ardhi kama tulivyowaruhusu wazanzibar kama tungeona ile ardhi kwao imegawanywa kwa usawa, ila kutokana na udogo wa ardhi wengine wamekosa, lakini kwa sasa hivi ardhi kubwa ya Kenya imekamatwa na wanasiasa na mabepari wasiojali wananchi wao, kwanini Tanzania ibebe mzigo ambao viongozi wao ndiyo wameusababisha?, Familia ya Kenyatta inamiliki zaidi ya ekari laki 5, kwa nchi kama Kenya ambayo eneo kubwa ni jangwa, hiyo ni ardhi kubwa sana, kwanini asibakishe laki moja nyengine awape familia masikini yeye afanye biashara zake za Bank, utalii na viwanda?.

Kuhusu ujio wa Rwanda na Burundi, mimi ninaunga mkono sana, kwa sababu hizi nchi zina matatizo ya msingi, ni nchi ndogo sana ardhi haiwatoshi, pili zina ukabila sana, tukiungana nao watafaidika kama Zanzibar, japo watapoteza political power za viongozi wao, lakini zitakuwa na amani kwa sababu serikali ya Tanzania ndiyo itakuwa inachunga usalama wao kama Zanzibar, na wataweza kuja huku na kupata ardhi na kutumia fursa nyingi za uchumi zilizopo Tanzania.
 
Watanzania 100 sawa na mkenya mmoja ukizijumuisha fikra zao ccm wapo madarakani toka 1961 maisha bado kama tupo chini ya mjerumani.
Sasa huo ni utani ina maana wakenya ni bora sana kuliko sisi, au sudi bado tupo karne ya 17/8 au tusemaje! Binafsi sioni utofauti maana suoni uspecial wao ni watu wa kawaida tu, mi niliokutana nao nawaona wa kawaida tu! Ila wewe ndo unawaogopa inferiority complex in you buddy! Achaaa hizo wa bongo tupo vizuri wewe ni wewe tu ndo zero kwa wakenya
 
Back
Top Bottom