Sawa mkuu,
Kumbe tatizo kuu la kenya ni Ukabila.
Wakitoa huo basi wanaweza kujenga nchi yenye nguvu kuliko hii ya sasa.!
Maswali mengine mawili,
1. Tufanye nini ili kuweza kurudisha imani iliyovunjika baina ya mataifa haya ndugu ya Tanzania na Kenya ???
2. Nini mtazamo wako juu ya Ujio wa Rwanda na Burundi ndani ya Shirikisho la Afrika Mashariki ???
Kwanza kumbuka fikra za kuunganisha Afrika nzima zilianzishwa na Kwame Nkurumah na Nyerere, hata kabla ya Tanganyika kupata Uhuru, ila walitofautiana katika muundo wa jinsi gani ya kuungana, wakati Nkurumah, alitaka nchi zote huru wakati ule ziungane kwa pamoja, namkila nchi ikipata uhuru iwe automatikali imejiunga, Nyerere yeye alitaka tuanze kuungana kikanda kwanza, kama vile nchi za Magharibi ziungane kwanza, EAC, na kusini mwa Afrika, baadae hizo blocks ndiyo ziunganishwe, mawazo ya Nyerere ndiyo yaliyokubaliwa na wanachama wengi, ila Nkuruma alionya kwamba, hawa viongozi wa Afrika wakishalewa madaraka itakuwa ngumu sana kuja baadae kuwaambia watoke kwenye viti vyao kwa ajili ya kuunganisha hizi nchi, na ndicho kilichotokea, baada ya nchi nyingi za Afrika kupata Uhuru, viongozi wengi sana walikataa kuunganisha nchi zao japo kwenye kanda kama alivyopendekeza Nyerere, mzee Jommo Kenyatta ni miongoni mwa viongozi waliokataa pamoja na juhudi kubwa za kushawishiwa na Nyerere.
Kwa sasa hivi Kenya ina tatizo kubwa la utaifa, wananchi wenyewe hawana umoja, wamegawanyika sana, na kunauwezekano Kenya ikagawanyika ikawa nchi mbili, is too late kwa sasa Kenya kuwa kitu kimoja, njia pekee japo kuituliza Kenya ni kuwa na muungano kama alivyosema mwalimu Nyerere, kama si Muungano Zanzibar ingekuwa ilishagawanyika kati ya Upemba na Unguja, wazanzibar ni wabaguzi sana, ni sawa na wakenya au wamewazidi wakenya kidogo, kinachowafanya washindwe kuchinjana kama wanavyofanya wakenya, ni kwasabu wapo ndani ya muungano na serikali ya Jamhuri ya Tanzania imewashikilia kwelikweli, lakini pia Tanzania bara inatumika kama mapafu ya kupumua kiuchumi kwa wazanzibar, sheria ya kumiliki ardhi inamkataza mtanzania bara kumiliki ardhi Zanzibar, ila wao wanaruhusiwa kumiliki ardhi huku bara, ndiyo sababu utaona wazanzibar wengi wamejenga majumba na wanamashamba makubwa na wengi ni matajiri huku bara, wasingekuwa na uwezo wa kuja huku bara, ardhi kwao ni ndogo ndiyo ingekuwa chanzo cha wao kupigana
Tungeweza kuwasaidia wakenya kwa kuwaruhusu waje kumiliki ardhi kama tulivyowaruhusu wazanzibar kama tungeona ile ardhi kwao imegawanywa kwa usawa, ila kutokana na udogo wa ardhi wengine wamekosa, lakini kwa sasa hivi ardhi kubwa ya Kenya imekamatwa na wanasiasa na mabepari wasiojali wananchi wao, kwanini Tanzania ibebe mzigo ambao viongozi wao ndiyo wameusababisha?, Familia ya Kenyatta inamiliki zaidi ya ekari laki 5, kwa nchi kama Kenya ambayo eneo kubwa ni jangwa, hiyo ni ardhi kubwa sana, kwanini asibakishe laki moja nyengine awape familia masikini yeye afanye biashara zake za Bank, utalii na viwanda?.
Kuhusu ujio wa Rwanda na Burundi, mimi ninaunga mkono sana, kwa sababu hizi nchi zina matatizo ya msingi, ni nchi ndogo sana ardhi haiwatoshi, pili zina ukabila sana, tukiungana nao watafaidika kama Zanzibar, japo watapoteza political power za viongozi wao, lakini zitakuwa na amani kwa sababu serikali ya Tanzania ndiyo itakuwa inachunga usalama wao kama Zanzibar, na wataweza kuja huku na kupata ardhi na kutumia fursa nyingi za uchumi zilizopo Tanzania.