kukariri
Fuatilia nyimbo zao za kwaya na vitabuni utaelewa kuwa biblia yote iko kichwaniKila mwaka huwa tunashudia mamia ya watoto wanaoshindana kwa kuhifadhi kitabu kitakatifu cha Quran.Hufanyika ngazi ya misikiti mpaka kimataifa kwenye viwanja vikubwa vya kitaifa,
Wako kama mimi wanaoweza kukariri juzuu moja yenye sura 36 fupi fupi.Wako juzuu 2,,3..4 mpaka 30.Tena ukariri huo ni lazima ufuatane na hukumu za kusoma kwa usahihi bila kukatisha herufu au kupunguza.
Yako mengi,lakini kwa hili masheikh wanasema huo ni moja ya muujiza wa Qur'an kwa vile ni maneno ya Mungu (Allah) mwenyewe.
Sijui kama wengine wanaofuata vitabu tofauti na Quran wamewahi wao wenyewe au viongozi wao kujaribu angalau ukurasa mmoja tu.
Kukalili ndiyo nini wewe mkubwa?Alafu unarudia mara mbili,jaribu kusema kukariri.Usituharibie lugha yetu pendwa ya kiswahili.Kukalili maandiko bila kuacha dhambi ni kazi bure. Umeambiwa usizini acha kuzini. Usiibe acha kuiba. Usiue basi usipoteze uhai we mwenzio. Wapo wanaokalili maandiko kuanzi mwanzo lakini ndio wauaji na wenye kila aina ya unyama na ufedhuli. Narudia tena,muhimu ACHA DHAMBI FANYA MATENDO YA UPENDO.
Hebu nitajie mstari unaotaja ukitoka chooni uoshe mikono kuaondosha uwezekano wa maambukizoKukariri ili iweje ?
Kwanza hiyo Quran yenu imeandikwa kwa mfumo wa mashairi ,hata Waimba singeri wanaikariri
Quran ni fupi sana ,huwezi linganisha na biblia ,biblia imejaa kila kitu kuanzia historia za mitume na manabii ,matukio ,Ina Vitabu vitano vya Torati, Zaburi ,injili ,nyaraka za mitume,matendo ya Mitume ,
Agano jipya tu ni kubwa kuliko Quran
Yaani ile Quran Ina maneno machache sana haifikii Agano jipya tu ambalo kwa asilimia kubwa aliandika Mtume Paulo ,
Quran ni mashairi hata Mzee wa bwax ,Manfongo ukiwapa siku 2 wanaikariri
Hii kukariri kwa Quran ni kama utangulizi.Tafsiri zake ndio ni ndefu sana kwa sababu zinaendana na hadithi za Mtume saw.Mtu anayependa Kukariri ni mpuuzi.
Mtu makini huwa anapenda kuelewa kitu, ila sio kukariri