Kila mwaka huwa tunashudia mamia ya watoto wanaoshindana kwa kuhifadhi kitabu kitakatifu cha Quran.Hufanyika ngazi ya misikiti mpaka kimataifa kwenye viwanja vikubwa vya kitaifa,
Wako kama mimi wanaoweza kukariri juzuu moja yenye sura 36 fupi fupi.Wako juzuu 2,,3..4 mpaka 30.Tena ukariri huo ni lazima ufuatane na hukumu za kusoma kwa usahihi bila kukatisha herufu au kupunguza.
Yako mengi,lakini kwa hili masheikh wanasema huo ni moja ya muujiza wa Qur'an kwa vile ni maneno ya Mungu (Allah) mwenyewe.
Sijui kama wengine wanaofuata vitabu tofauti na Quran wamewahi wao wenyewe au viongozi wao kujaribu angalau ukurasa mmoja tu.
Nyie mnakariri Quran. Unaweza kunionesha aya kwenye Quran inayotaka Waislam wakakariri Quran?
Wakristu na Wayahudi wanafuata kile kilichoandikwa kwenye Biblia. Katika kitabu cha Deuteronomy 6:6 inasema hivi:
6 "Na maneno haya ninayokuamuru leo, yatakuwa katika moyo wako;"
Wayahudi Wanaita Sehemu hii ya Biblia kwa jina la "
Shema Yisrael au Sh'ma Yisrael" au wengine wanaita tu "
Shema". Wakristu wote wanaita
"Amri Kumi Za Mungu"
Hii "Shema" Musa aliwambia Wayahudi kuwa lazima waijue kwa moyo. Na hii ni sehemu pekee ya Biblia ambayo Wayahudi na Wakristu wote wanaijua kwa moyo, akili na roho.
"Shema" inapatikana kwenye vitabu vya
Kumbukumbu la Torati 6: 4-9
Kumbukumbu la Torati 11: 13- 21
Hesabu 15: 37-41
Mkristu yoyote au Myahudi anajua sehemu hii ya Biblia kwa sababu Musa aliamuru tuijue kwa moyo (siyo tukariri). Kufaulu Sunday school lazima ujue sehemu hii pamoja na Amri 10 za Mungu kwa ujumla
Nakuwekea hapa portion zima ya "Shema" ili uielewe:
4 Sikiza, Ee Israeli; BWANA, Mungu wetu, BWANA ndiye mmoja.
5 Nawe mpende BWANA, Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote.
6 Na maneno haya ninayokuamuru leo, yatakuwa katika moyo wako;
7 nawe uwafundishe watoto wako kwa bidii, na kuyanena uketipo katika nyumba yako, na utembeapo njiani, na ulalapo, na uondokapo.
8 Yafunge yawe dalili juu ya mkono wako, nayo yatakuwa kama utepe katikati ya macho yako.
9 Tena yaandike juu ya miimo ya nyumba yako, na juu ya malango yako.
13 Mche BWANA, Mungu wako; ndiye utakayemtumikia, na kuapa kwa jina lake.
Yesu anarudia "Shema" katika kitabu cha Marko 12: 29-31