Hivi kwanini Wakristo na Wayahudi wanashindwa kukariri angalau ukurasa mmoja wa vitabu vyao?

Quran ina aya 6300, Biblia ina aya 31,102. Biblia ni kubwa mara tano zaidi ya Quran.
Sawa.Lakini hizo aya zote ni maneno ya Mungu ?
Kwa sababu Mungu ambaye ndiye muumba wa lugha huwa hatumii maneno mengi kufikisha ujumbe .
 
Imekuwaje basi hata mtume Paulo akatia maneno yake.Shida imeanzia hapo.
 
Quran imetokana na simulizi za mtu mmoja akisumulia kile anachoamini kilitokea au ameambiwa na Allah, Biblia imeandikwa na kutokana na waandishi zaidi ya 40.
Sio simulizi.Ni maneno ya Allah ambayo Mtume Muhammad aliyakariri kwa maswahaba hata kama hakujua maana yake wakati huo.
Na baadae Allah aliporidhika kila kitu kiko sawa akasema humo humo kwenye Quran kama Muhammad angethubutu kubadili angalau herufi moja basi angemkatila mbali mshipa wa kulia wa moyo.
 
Maandiko hayatambui kitabu kinachoitwa Biblia wala hakuna andiko lililotaja biblia kwahiyo ni kitabu cha ujanja ujanja
 
Ikiwa vitabu vya kisheria watu wanakariri...
Ili utilie maanani jambo inategemea how vslue it is....kuna mtu ukimwambia kuna andiko ndani ya BIBLE inakataza nguruwe atang'aka....andiko YESU sio MUNGU atang'aka...
Huku ni matendo kwa imani tu....hata wakikaa viongozi waka edit vifungu...hii ni dini ya imani tu utaingia mbinguni
 
Waislam wapo na aman saana
 
Watu wanakariri chand iwe biblia?,ni vile tu Haina ulazima au maana yoyote Ile kuriri kitu ambacho unaopition ya kukisoma.Biblia imeandika "yasomeni na kutafakari mchana na usiku",na sio habari za nkukariri.So acha ujinga,huo sio muujiza ni ujinga tu wa mashekhe na sio vinginevyo!!!
 

Systematic Embecilization...
 
Key word hapa ni elewa siyo kariri. What is the point of kukariri, itakusaidia nini? Kwa tofauti hii tu, you can't convince me eti tunamwambudu Mungu mmoja, the difference is too much.
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ Ila Allah ana mikwara Sana kwamba mshipa wa kulia wa Moyo sio
 
Na alikufa katika maumivu kana kwamba mshipa wa moyo wake ulikuwa unakatiliwa mbali. Nyie, Mungu ni wa kuogopwa
 
Nyie mnakariri Quran. Unaweza kunionesha aya kwenye Quran inayotaka Waislam wakakariri Quran?

Wakristu na Wayahudi wanafuata kile kilichoandikwa kwenye Biblia. Katika kitabu cha Deuteronomy 6:6 inasema hivi:
6 "Na maneno haya ninayokuamuru leo, yatakuwa katika moyo wako;"

Wayahudi Wanaita Sehemu hii ya Biblia kwa jina la "Shema Yisrael au Sh'ma Yisrael" au wengine wanaita tu "Shema". Wakristu wote wanaita "Amri Kumi Za Mungu"

Hii "Shema" Musa aliwambia Wayahudi kuwa lazima waijue kwa moyo. Na hii ni sehemu pekee ya Biblia ambayo Wayahudi na Wakristu wote wanaijua kwa moyo, akili na roho.

"Shema" inapatikana kwenye vitabu vya
Kumbukumbu la Torati 6: 4-9
Kumbukumbu la Torati 11: 13- 21
Hesabu 15: 37-41

Mkristu yoyote au Myahudi anajua sehemu hii ya Biblia kwa sababu Musa aliamuru tuijue kwa moyo (siyo tukariri). Kufaulu Sunday school lazima ujue sehemu hii pamoja na Amri 10 za Mungu kwa ujumla

Nakuwekea hapa portion zima ya "Shema" ili uielewe:

4 Sikiza, Ee Israeli; BWANA, Mungu wetu, BWANA ndiye mmoja.
5 Nawe mpende BWANA, Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote.

6 Na maneno haya ninayokuamuru leo, yatakuwa katika moyo wako;

7 nawe uwafundishe watoto wako kwa bidii, na kuyanena uketipo katika nyumba yako, na utembeapo njiani, na ulalapo, na uondokapo.

8 Yafunge yawe dalili juu ya mkono wako, nayo yatakuwa kama utepe katikati ya macho yako.

9 Tena yaandike juu ya miimo ya nyumba yako, na juu ya malango yako.
13 Mche BWANA, Mungu wako; ndiye utakayemtumikia, na kuapa kwa jina lake.

Yesu anarudia "Shema" katika kitabu cha Marko 12: 29-31
 
Kipindi nasoma mafundisho pale St Peter, nilikua nimezikariri Sala zote za Kanisa katoliki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…