Hivi kwanini Wakristo na Wayahudi wanashindwa kukariri angalau ukurasa mmoja wa vitabu vyao?

Mkuu we hujawahi ona wahubiri au mkristo akiwa anazungumza pasipo kuwa na bible anatoa reference ya mstari, kifungu na kuutaja ulivyo pasipo kutumia kitabu au wewe unasema kuclaim kwa muda gani? Tena kwa anachokizungumzia anaweza kurefer zaidi ya kifungu kimoja kutoka vitabu tofauti vya biblia
 
There you go, mnakariri, si kuelewa. Kukariri hakukufanyi kulijua neno pa Mungu, kulielewa
 
Huu ndio ukweli
 
Ukristo sio ubishoo wa kujionesha. Mambo ya ndani ya kania utajuaje wewe usiye mkristo? Watoto wa kikristo wanakariri kitabu kizima lakini pia ujue Neno la Mungu sio kukariri tu bali kuliishi ndiko kuliko na muujiza. Hivyo Acha kulinganisha ukristo na watu wengine.
 
Biblia ni nafsi inayo ishi kama radi tu,
Ukikariri utasogea ila kuna mahali hautafika
 
Lazma ukariri ukikumbuka ahadi ya ahera ya kuvunja mabikra 72 bikra zao,alaf Wana macho mithili ya vikombe Kwa nn usikariri??
 
Sion sbb ya kukariri au kushindania vitabu vya kidini nachoona ni kuvisoma na kuvielewa na kuyaishi yanayoshairiwa humo.
 
Wayahudi wamekariri Na Ni lazima Kukariri Torati Yote..
Ukiwa Kijana na Ukikariri Unapewa huwa Wanavaa Tefilin shel yad (תפילין של יד) – Hufungwa kwenye mkono wa kushoto (au wa kulia kwa mtu wa mkono wa kushoto), na kamba ya ngozi (retzuot) huzungushwa juu ya mkono na vidole. Na pia huvaa Tefilin shel rosh (תפילין של ראש) – Huvaliwa kwenye kichwa, katikati ya paji la uso, na kamba hupita kuzunguka kichwa.

Ukimuona myahudi kavaa Hizo kamba Au utepe Ujue Amekariri Torati yote na Kuielewa Na Anaweza Kuitamka..

Kama Maelekezo Ya Biblia (TANAKH) Yanavyowataka..


Kumbukumbu la Torati 6:6-8...

"Na maneno haya ninayokuamuru leo yatakuwa moyoni mwako; nawe uwafundishe watoto wako kwa bidii, na uyanene ukiwa umeketi nyumbani mwako, uendapo njiani, ulalapo, na uamkapo. Nawe uyafunge yawe dalili juu ya mkono wako, nayo yatakuwa kama utepe katikati ya macho yako."

Na Pia Soma!

Kumbukumbu la Torati 11:18

"Yawekeni maneno yangu haya mioyoni mwenu na rohoni mwenu, myafunge kama ishara juu ya mikono yenu, nayo yawe kama utepe katikati ya macho yenu."


Sasa Sijui wewe Unawasemea Wayahudi Gani?

Au hujui Hata Torati kwa Wayahudi Ziko za Aina Mbili?

Torati Iliyoandikwa yaani Torah Shebichtav –na hii ni sehemu tu ya maandiko matakatifu ya Kiyahudi na ndo ipo Kwenye Biblia ikiwa na vitabu vitano vlvya Musa au unaweza kuita Pentateuch Mwanzo, Kutoka, Mambo ya Walawi, Hesabu, na Kumbukumbu la Torati.

Na torati nyingine ni Torati ya Mdomo yaani Ya Masimulizi Torah Shebe'al Peh – Hii ndo ina mafundisho, tafsiri, na maelekezo yaliyopitishwa kwa mdomo kutoka kizazi kimoja hadi kingine kutoka kwa Musa Mwenyewe na baadaye yaliandikwa katika Talmud na Midrash...


So Kindly Kama Hujui Kitu Uliza Kwa Moyo wa Dhati Kuliko Kukileta Kwa Mlengo wa Chuki Na HASAD..

Shukrani
CC: Webabu
 
Sion sbb ya kukariri au kushindania vitabu vya kidini nachoona ni kuvisoma na kuvielewa na kuyaishi yanayoshairiwa humo.
Hilo ndio lengo kuu la waislamu,Huwa wanafanya hivyo kujikumbusha na kukumbushana.
AlhamduLillaah ,sehemu Qur'an ilipohifadhiwa nyoyoni na kukaririwa basi pana na amani sana na baraka kutoka kwa Allah.
 
Tunashukuru kwa kutoa uzi wenye hamasa za KIROHO zaidi ni jambo jema sana
Kwanza nianze kwa kusema umeandika uzi bila kufanya utafiti kwa kina maana umebase kwenye uislamu na kuuinua juu mno hadi viwango vya stratosphere, kwa upande wako katika hili upo sahihi.
Pili, tambua ya kwamba wakristo wengiiii Imani zao sio za kujionesha kile wafanyacho, tambua kuna wakristo wanafunga siku hadi 40 bila matangazo kwenye social mediaz
Wakristo wamejaza mafungu ya Biblia kwa umaji wa kimya kimyaaaaa kwa mfano wafuatilie Wasabato utaelewa nisemacho hapa.

Tatu, Dini sio kukariri tu Vitu ambavyo huvitumii maishani ,Maana mnakaririsha watoto Dini alafu ndio wanaongoza kwa matusi mitandaoni, mfano mdogo Waislamu wakifunga kwenye mitandao kuna kuwa kutulivu saaaana, mkifungua virugu nyingiii kama kunguru aliyeachiliwa baada ya kukamatwa😄😄 Don't take it seriously.

La nne na la mwisho Tuache Udini na huu pia unarudisha nyuma maendeleo ya Taifa maana kuna mahali nilikusa Ajira kwa kuwa ni Mkristo So sad...
 
Anafanya vitu kama vitu huyo Yehova.Naona kama ni huyo huyo Allah.ni mbadiliko wa lugha tu
Siyo kweli Allah siyo Yehova.
Kiarab na Kiebrania ni lugha zinazofanana sana. Maneno mengi ya Kiebrania yanafana na Kiarab sitegemi Yehova ibadilike kuwa Allah.

Ndiyo maana hata Wakristu Waarab Yesu au Yeshua kwa Kiarab anaitwa Yasu na siyo Isa
 
Wote ambao nimewasikiliza mimi huwa wanatoa yao ya moyoni na waliyokutana nayo jana njiani.hao ambao wamefanikiwa kufanya hivyo hebu nielekeze niende nikawafuatilie.
 
Umenikumbusha Mbali sana Kuhusu Shema Yisrael..

Na Ndo hutumika Mfanano wa Adhana kwa Wayahudi ambao waislam walichukua Huko..
Webabu
Your browser is not able to display this video.
 
Sawa.Lakini hizo aya zote ni maneno ya Mungu ?
Kwa sababu Mungu ambaye ndiye muumba wa lugha huwa hatumii maneno mengi kufikisha ujumbe .
Lete ushahidi bila shaka kuwa Quran ni neno la Mungu.
 
Wote ambao nimewasikiliza mimi huwa wanatoa yao ya moyoni na waliyokutana nayo jana njiani.hao ambao wamefanikiwa kufanya hivyo hebu nielekeze niende nikawafuatilie.
Kweli watu husikia na kuamini kile wanachokiamini. Wakristo hasa walokole huwa wana refer mistari ya biblia, atakwambia mathayo sura ya 3 mstari fulani unasema hivi, ataenda kwingine ata quote kifungu kingine chenye ujumbe sawa na huo wakati akieleza jambo fulani. Mbona ni jambo la kawaida hilo sana mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…