Acha niwape experience yangu binafsi kuhusu kufall in love kwa kijana mdogo...ilikua balaa, ilibidi familia iingilie kati... Nilimzidi miaka nane....
Imepita miaka minne sasa, nilikutana na Gee wakati nafanya kazi deiwaka mahala, nilipokua nafanya kazi na ofisi ya Gee ni ofisi jirani, na pia alikua kijana mchangamfu sana, very humble ,very caring...
Kimuonekano alikua ana umbo kubwa , mtu wa mazoezi, kwahiyo haikua inasumbua sana, ni hadi uwe mfuatiliaji ndio utagundua utofauti wetu, ilikua tukitembea wote anapenda kunikumbatia yaani, na huu ushamba wangu wa kihehe ,woiii nikawa naona kama nimebeba dunia
Unapokua mgeni mahala lazma watatokea wawili watatu kukukaribisha, jinsia tofauti, kwaio wakati hao wakaribishaji wanapambana kunizoea Gee tried to stop it, si mnajuana tabia zenu wanaume mkiona pisi mpya mtaani, yaani aliingia kwa bifu na baadhi ya wanaume ofisi jirani. Hayo yakawa yanaendelea mimi muhusika sifahamu hata, taarifa zikaanza kuzagaa kua natoka na Gee, wachache wanaopenda kupata ubuyu ulio fresh toka kwa wahusika wakanifata kutaka kufahamu ukweli wa hiyo story, ikabidi nimfate huyo Gee Sasa maana sikuwahi kumzoea kiivo, ingawa yeye alikua anapambana kunizoea namkazia, nilikua nakachukulia katoto tu, kabishoo ivooo...
Nikawait lunch nikaomba kuongea nae, tukakutana kwa cafe mbali kidogo na hapo job, nikamuuliza nayoyasikia kama yana ukweli, akawa kama anataka kukataa baadae akakubali kua ni kweli alijipa iko kibarua, akanambia sister we mzuri sana watakutumia tu wakuache, nawajua wale majamaa mambo zao, so zikaanza story pale za hapa na pale, tukabadilishana namba, mazoea yakazidi, tunachart hadi usiku, tunaongozana karibu kila mahala ivooo....
Akanikaribisha kwake, alikua anakaa karibu na mahala tunafanya kazi, mimi nilikua naishi mbali kiasi, kwahiyo zilianza sleep over, naacha kagauni kwake, mara tishrt, mara bra , ghafla nikahamia kwake... Gee cooked for me, alikua ananifulia ,uwiii yale mahaba aiseee, sijawahi fanyiwa hizo mambo hata, we had a bond, vitu vilikua vinatokea kwa kasi na ilikua poa sana, never had that experience before, I can't tell how I fall in love but I surely did...
Kuna mistake aliifanya na ilifanya hadi familia waingilie, nilianza kufanya matumizi rough ya pesa kuliko inavyotakiwa, naweza sema alikua na jambo lake na alifanikiwa, alianza kunicontorl financially, and too bad sikua na kauli, I was okey ...just okey...nilihama home bila taarifa, home wakawa hawafahamu naishi wapi, naweza sema I was totally lost in his arms. Vipigo vikaanza pia, kaka anapiga kama Mandonga....wivu uliopitiliza daaah
Baada ya jitihada kubwa ya wanafamilia ikabidi nirudi nyumbani, bi mkubwa akawa anacontrol pesa yangu, Geee akaanza kujikataa mdogomdogo, si akipiga mzinga Sina hela, akaanza kunipiga matukio mfululizo yaani, hakuna rangi sikuona, ikafika mahala ilibidi na ile kazi niache, nilimblock kila mahala, nikapambana kumsahau and yes I won...ila Yule mkaka daah, hua namkumbuka na zile show zake aiseee, ni vile alinigeuza ATM machine...
All in all ,it was a beautiful experience....no regrets!