Zanzibar-ASP
JF-Expert Member
- Nov 28, 2013
- 11,550
- 40,697
Shida iko kwenye tafsiri ya mtu sahihi, utulivu kabla ya kuamua kuingia kwenye mahusiano na tamaa kutangulia mbele.
Kabla ya kujiuliza huyo mtu sahihi unayemtaka wewe, je yeye naye anakuona wewe ni mtu sahihi kwake?
Kuna tofauti kati ya mtu sahihi na mtu mzuri. Kama wewe huna pesa na maisha yako yana mtazamo wa kuhitaji pesa zaidi ili kuwa yenye furaha basi mtu sahihi kwako huenda akawa ni yule mwenye pesa lakini hiyo haimaanishi huyo mtu atakuwa mzuri kwako kimaisha.
Yote kwa yote, mpaka watu wanaamua kuoana basi ujue wazi wamekutana na kujiridhisha kuwa wao ni watu sahihi waliokutana. Simamia hapo hapo.