Hivi kwanini watu sahihi hawakutani kwenye mahusiano

Hata wazazi wako hawakuwa sahihi kweny e mahusiano yao ?

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 

Na wenyewe watu sahihi hawakutani kwenye mahusiano sababu wanataka watu sahihi​

 
........factors zonazowaweka watu pamoja ni nyingi si moja, so even if you are descent kitabia you need to be attractive, usawa kidini, kikabila nk mf kuna baadhi ya mahusiano yanavunjwa na wazazi hata kama walimatch kwa vitu vingi.....
 
Nadhani ni mfumo wa muumba mwenyewe au ni wivu wa shetani!

Ingelikuwa ni rahisi kumpata mtu wa 'size' yako, dunia hii tungeliishi kwa raha sana.

Cha ajabu kabla ya kuingia kwenye mahusiano, watu wanaweza kuigiza tabia njema kuvutia wenza, lakini tabia hizo njema kuziendeleza ama kujirekebishia, huwa haiwezekani.

Mkishaoana, tabia mbofu mbofu zile zile zinarudi na mnaanza kusumbuana!

Dunia hii siyo fair kwa kweli.
 
Tatizo linaanziaga hapa👇

Unayempenda, kampenda mwingine
Huyo mwingine naye ana mwingine
Mwingine naye kapendwa na mwingine
Kupendwa na mwingine infinitively siyo tatizo, tatizo lipo hivii?:

Ukimpenda mtu kwa dhati, yeye huwa hakupendi kwa kiwango unachompendea wewe na huo ni mfumo!

Kwa hiyo ukimpenda mtu sanaa, elewa yeye hawezi na hakupendi kwa kiwango hicho, kwa hiyo mkifanikiwa kuanzisha mahusiano, lazima wewe utakuwa ni 'slave' katika penzi hilo.

Nadhani hali hiyo iliumbwa ili kulipa thamani penzi, awepo wa kuringa na awepo wa kubembeleza.

Kungelikuwa na 50/50 katika penzi ku break up ingelikuwa ni rahisi sana maana pasingelikuwepo wa kujali.
 
kwasababu mnaoa haraka amna subira, mimi bado namtafuta ☺。
Mfumo wa dunia hauwezi kurekebishwa na wewe mtu mmoja.

Tena usipoangalia kwa chagua chagua yako hiyo, utajanasa kwenye 'tundu bovu' mpaka ushangae.

Chagua chagua, peleleza peleleza yako hiyo haitakusaidia sana zaidi ya kupoteza muda na wakati.

Tumia mila na tamaduni kuchagua mchumba wa kuoa na uoe, lakini kusema utamchunguza tabia mwanamke na umjue kabla ya kumuoa na kuishi naye, unajinganya, tabia zote mbovu hufichwa mchumba usizielewe.
 
Kuna binti mmoja aliwahi kumuuliza mama yake, kwani ulimtoa wapi huyu baba. Akiangalia alivyo na mama na baba yake hawaendani kabisa. [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Yote ni bure tu, mapenzi yanaimarika popote penye heshima, kujitoa na uaminifu. Hayo yakikosekana tu yanabakia mazoea ama maslahi tu.

Kwakuwa binadamu wengi tuna unafiki na ubinafsi matokeo yake ndo inakuwa ngumu sana kukutana mkadumu. Interests zinapishana mapema tu. We umefata hela mwenzio amekuja kukuenzi na kukupa huba. Unafikiri nini kitafata ukishazipata hela zake? Utaendelea kuishi kinafiki hadi lini na unajua dhahiri kilichokupeleka ni pesa zake tu.
 
Kufupisha tu mtu hawezi kuwa perfect kwa 100% lazma kuna room ya corrections. Ishu inakuja kwamba unakutana na mtu perfectionist ambaye yeye hataki kufanya corrections ina maana upande mmoja utapaswa kuishi kwa kuvumilia udhaifu wa upande mwengine. Kwa vijana wa kileo hilo haliwezekani kwao solution ni replacement.
 
Mkuu mimi nadhani tatizo hapa sio kiwango cha upendo

Kumpenda sana mtu hakufanyi muwe couple sahihi kama na yeye atakupenda kwa kiwango kilekile
Mnaweza mkapendana sana lakini issue ikawa ni tabia tu, ulevi, hasira, wivu, kuchepuka nk nk
 
Ni kweli mkuu

Na hii uvumilivu wa upande mmoja huwa unawa favor sana wanaume wanao oa mama wa nyumbani ambao 100% anamtegemea mumewe kwa kila kitu na anaona ni kama ndoa ikifa atakwenda wapi na ana watoto na umri umesogea
Sasa couple kama hii ukiiona Jumapili wanakwenda kanisani wamependeza wanacheka na watoto unaona hii ndio couple sahihi ina miaka 20 na wako poa
Kumbe nyuma ya pazia ni balaa

Ila vijana wa 2000 hawaogopi kabisa usingle mother mkizinguana kidogo hakuna kuvumilia anasepa
 
Eeh vitoto vya buku 2 havijui uvumilivu. As long as hapati anachotaka atakitafta kwengine tu mwisho ni kufumaniana na kuachana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…