Hivi kweli Azam FC timu iliyokuwa inategemewa kuleta mapinduzi ya soka inazidiwa point 23 na Yanga inayoongoza ligi?

Hivi kweli Azam FC timu iliyokuwa inategemewa kuleta mapinduzi ya soka inazidiwa point 23 na Yanga inayoongoza ligi?

Noti bandia

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2020
Posts
2,684
Reaction score
4,315
Viongozi wa Azam ni kama walifanikiwa kuingizwa kwenye mtego wa U Yanga na U Simba hususani kulalamikia hujuma timu inayofanyiwa dhidi ya mabeberu hao wa soka hapa nchini na kupelekea wao kutokufanya vizuri.

Wakati mwingine wakaenda mbali zaidi na kuhisi pia chama cha soka kimewakumbatia zaidi huyo Kurwa na Doto Jambo ambalo ukilitazama vizuri ni kama linaukweli. Lakini licha ya hayo yote nimejaribu kufuatilia mechi za Azam hususani mechi ya karibu dhidi ya Yanga.

Hivi kweli game kama ile utajiuliza kweli kunahujuma au Azam imefikia kikomo na imebaki na tabia za Kurwa na Doto ambapo msimu Kurwa anashinda Doto anawaaminisha washabiki zao kuwa Kurwa anabebwa na yeye anahujumiwa same to Doto akishinda Kurwa naye hulalama the same.

Azam kwa hatua mliyofikia haiendani na matokeo yenu, nilitegemea muwe mnatoa ushindani kwa hizi timu mbili lakini sio leo mmecheza mechi 19 sawa na Yanga lakini tayari mnatofauti ya point 23.
 
Tatizo la Azam fc ni viongozi wao kwa kikosi walicho nacho kingekuwa ni Cha Yanga ama Simba ingekuwa hatari zaidi pia timu imekosa nguvu ya Mashabiki hivyo machezaji wanavheza kifaza zaidi kwavile wachezaji wao hawatukanwi na Mashabiki wakifanya vibaya
 
Ukweli ni kwamba Yanga hii imevizidi sana hv vilabu vingine hapa nchini. huu ubora wao si wa kubahatisha.. Yanga ni club pekee ambayo inaweza kutanguliwa kufungwa BAO na Mashabiki wakaendelee kuwa na furaha.

Refer mechi nying za nyuma za Yanga.. ukiona Yanga katanguliwa goli moja basi hiyo mechi itaisha kwa ushindi wa Yanga 2-1 au 3-1.

So mpaka Yanga atamaliza ligi atakuwa amemuacha Azam zaidi ya points 30
 
Ukweli ni kwamba Yanga hii imewazidi sana hv vilabu vingine hapa nchi.. huu ubora wao si wa kubahatisha.. Yanga ni club pekee ambayo inaweza kutanguliwa kufungwa BAO na Mashabiki wakaendelee kuwa na furaha.. refer mechi nying za nyuma za Yanga.. ukiona Yanga katanguliwa goli moja BAO sio mechi inaisha kwa ushindi wa Yanga 2-1 au 3-1.
So mpaka Yanga atamaliza ligi atakuwa amemuacha Azam zaidi ya points 30
agiza mihogo hapo ukaandae futali jioni nakuja kulipia😄😄😄
 
Azam walitakiwa wawe kama asec MIMOSA au pyramid maana ndio wapo kama wao ila cha ajabu nje hawapo na ndani tia maji tia maji.
Asec ni timu kongwe labda pyramid .......hela hazitumiki ipasavyo.
 
Tatizo la Azam ni uongozi,benchi la ufundi na wachezaji,

viongozi-hawa ndio wanaua timu hawana malengo ya kimaendeleo na timu ukilinganisha na viongozi wa hizi timu kongwe zinajipanga kuwa na mafanikio ya kuchukua ubingwa au kufika hatua flani katika mashindano ya kimataifa.wangekuwa na malengo na wakayatekeleza timu hii ingekuwa tishio hapa nchini na nje ya nchi,lakini viongozi wanaonekana hawana malengo ya dhati kufikia kuwa timu tishio nchini na afrika kwa ujumla,nadhani viongozi wengi ni mamluki wa hizi timu kongwe.

Benchi la ufundi- naona hawa hawana njia yeyote ya kuifikisha timu katika mafanikio.......kwani hawasajili wachezaji wanaoweza kuleta ushindani wa hali ya juu katika kukabiliana na timu zilizokuwa na benchi la ufundi imara kama Simba au Yanga,unaona kabisa usajili wa azam ni wa kawaida wanasajili wachezaji wa level za timu kama polisi Tz au coastal union au wengine wanauwezo mdogo kuliko wachezaji wa timu tajwa,pengine labda timu ibakuwa na bajeti ndogo kwa mwaka kuweza kusajili wachezaji wenye madaraja ya juu kama wanaosajiliwa na hizi timu kubwa,maana kuna mechi Azam Fc inafungwa kutokana Quality ya wachezaji iliyo nao..mfano mechi ya juzi ya Yanga.

Wachezaji- Hawana morali na ni wachezaji wa hali ya chini kabisa kucheza pale Azam fc ukilinganisha na ukubwa wa Azam na uwekezaji waliofanya kwenye soka kwa kuwa na miundo mbinu na vifaa bora vya mchezo wa soka,lakini bado wanaokota wachezaji ambao upambanaji wao si wa kuiletea timu chochote,ingekuwa vizuri timu ikaboresha uchezaji kwa wachezaji wao walio nao kwa kuweka ushindani wa namba sio mtu anabweteka anajua tu lazima mechi hii nitacheza,timu iwe na quality player wanaoweza kukupa kitu kwa asilimia mia wanapokutana na hizi timu kubwa na timu yeyote ile,wajenge heshma ya uwanja wa nyumbani kwa kutokutoa pointi tatu kizembe zembe,Timu iweze kushindana katika soko la usajili ijengwe timu inayoweza kutunishiana misuli na Pyramid fc na sio timu inayopigwa bao na polisi au Coast Nyumbani.

#Mimi niliamua kuwa shabiki wa Azam fc kama mwana mabadiliko katika soka ,sio kila siku Simba mara Yanga....Mashabiki wa kweli kama sisi tunaumia sana kushabikia timu ambayo haibebi chochote haina dira haina tamaa ya kufika mbali.
 
Azam inasikitisha sana.imekua ni timu ambayo imebaki jina tu badala yakutoa ushindani unaoeleweka.Nadhani tatizo liko kwenye uongozi wa timu kwa ujumla.
 
Binafsi nilitaka Azam FC iwe kama Mamelodi Sundown, masandawana hapo SA, hizi timu zinafanana mno kuanzia owners wake, facilities zao ila Azam fc politics zimewakamata mno,sad
 
Azam wanaumiza sana wana kila kitu shida sijui hata niniukute pia viongozi wapo chamazi ila mapenzi yapo kariakoo tukiwa na Azam bora na Simba bora na Yanga bora itasaidia kimataifa hamna kitu kinatia wivu kama wamisri na wamorroco ona misri timu zao msimu huu mpaka saivi zote zipo quarter final kasoro zamalek njoo Morroco watu waache ubabaishaji tupambane ila one day tu tutakuwa kama wao
 
Viongozi wa Azam ni kama walifanikiwa kuingizwa kwenye mtego wa U Yanga na U Simba hususani kulalamikia hujuma timu inayofanyiwa dhidi ya mabeberu hao wa soka hapa nchini na kupelekea wao kutokufanya vizuri.

Wakati mwingine wakaenda mbali zaidi na kuhisi pia chama cha soka kimewakumbatia zaidi huyo Kurwa na Doto Jambo ambalo ukilitazama vizuri ni kama linaukweli. Lakini licha ya hayo yote nimejaribu kufuatilia mechi za Azam hususani mechi ya karibu dhidi ya Yanga.

Hivi kweli game kama ile utajiuliza kweli kunahujuma au Azam imefikia kikomo na imebaki na tabia za Kurwa na Doto ambapo msimu Kurwa anashinda Doto anawaaminisha washabiki zao kuwa Kurwa anabebwa na yeye anahujumiwa same to Doto akishinda Kurwa naye hulalama the same.

Azam kwa hatua mliyofikia haiendani na matokeo yenu, nilitegemea muwe mnatoa ushindani kwa hizi timu mbili lakini sio leo mmecheza mechi 19 sawa na Yanga lakini tayari mnatofauti ya point 23.
Azam ina vionhozi wadwanzi,waswahili,wana majungu ya hatari
 
Ukweli ni kwamba Yanga hii imevizidi sana hv vilabu vingine hapa nchini. huu ubora wao si wa kubahatisha.. Yanga ni club pekee ambayo inaweza kutanguliwa kufungwa BAO na Mashabiki wakaendelee kuwa na furaha.

Refer mechi nying za nyuma za Yanga.. ukiona Yanga katanguliwa goli moja basi hiyo mechi itaisha kwa ushindi wa Yanga 2-1 au 3-1.

So mpaka Yanga atamaliza ligi atakuwa amemuacha Azam zaidi ya points 30
Yanga ambayo kimataifa hawana lolote
 
Back
Top Bottom