Hivi kweli Azam FC timu iliyokuwa inategemewa kuleta mapinduzi ya soka inazidiwa point 23 na Yanga inayoongoza ligi?

Hivi kweli Azam FC timu iliyokuwa inategemewa kuleta mapinduzi ya soka inazidiwa point 23 na Yanga inayoongoza ligi?

Tatizo la Azam ni uongozi,benchi la ufundi na wachezaji,

viongozi-hawa ndio wanaua timu hawana malengo ya kimaendeleo na timu ukilinganisha na viongozi wa hizi timu kongwe zinajipanga kuwa na mafanikio ya kuchukua ubingwa au kufika hatua flani katika mashindano ya kimataifa.wangekuwa na malengo na wakayatekeleza timu hii ingekuwa tishio hapa nchini na nje ya nchi,lakini viongozi wanaonekana hawana malengo ya dhati kufikia kuwa timu tishio nchini na afrika kwa ujumla,nadhani viongozi wengi ni mamluki wa hizi timu kongwe.

Benchi la ufundi- naona hawa hawana njia yeyote ya kuifikisha timu katika mafanikio.......kwani hawasajili wachezaji wanaoweza kuleta ushindani wa hali ya juu katika kukabiliana na timu zilizokuwa na benchi la ufundi imara kama Simba au Yanga,unaona kabisa usajili wa azam ni wa kawaida wanasajili wachezaji wa level za timu kama polisi Tz au coastal union au wengine wanauwezo mdogo kuliko wachezaji wa timu tajwa,pengine labda timu ibakuwa na bajeti ndogo kwa mwaka kuweza kusajili wachezaji wenye madaraja ya juu kama wanaosajiliwa na hizi timu kubwa,maana kuna mechi Azam Fc inafungwa kutokana Quality ya wachezaji iliyo nao..mfano mechi ya juzi ya Yanga.

Wachezaji- Hawana morali na ni wachezaji wa hali ya chini kabisa kucheza pale Azam fc ukilinganisha na ukubwa wa Azam na uwekezaji waliofanya kwenye soka kwa kuwa na miundo mbinu na vifaa bora vya mchezo wa soka,lakini bado wanaokota wachezaji ambao upambanaji wao si wa kuiletea timu chochote,ingekuwa vizuri timu ikaboresha uchezaji kwa wachezaji wao walio nao kwa kuweka ushindani wa namba sio mtu anabweteka anajua tu lazima mechi hii nitacheza,timu iwe na quality player wanaoweza kukupa kitu kwa asilimia mia wanapokutana na hizi timu kubwa na timu yeyote ile,wajenge heshma ya uwanja wa nyumbani kwa kutokutoa pointi tatu kizembe zembe,Timu iweze kushindana katika soko la usajili ijengwe timu inayoweza kutunishiana misuli na Pyramid fc na sio timu inayopigwa bao na polisi au Coast Nyumbani.

#Mimi niliamua kuwa shabiki wa Azam fc kama mwana mabadiliko katika soka ,sio kila siku Simba mara Yanga....Mashabiki wa kweli kama sisi tunaumia sana kushabikia timu ambayo haibebi chochote haina dira haina tamaa ya kufika mbali.
Litimu la hovyo sana hilo unashabikia timu inafukuza wachezaji waliowapa ubingwa mna akili nyinyi
 
Ukitaka kujua ushindi wa yanga huwa umepangwa mezani,subiri waende kimataifa ndio utajua tunachoongea.

Kifupi huo ni ubingwa wa GSM na siyo wa yanga.
Utaona jinsi atakavyoumbuka kimataifa
Ukweli ni kwamba Yanga hii imevizidi sana hv vilabu vingine hapa nchini. huu ubora wao si wa kubahatisha.. Yanga ni club pekee ambayo inaweza kutanguliwa kufungwa BAO na Mashabiki wakaendelee kuwa na furaha.

Refer mechi nying za nyuma za Yanga.. ukiona Yanga katanguliwa goli moja basi hiyo mechi itaisha kwa ushindi wa Yanga 2-1 au 3-1.

So mpaka Yanga atamaliza ligi atakuwa amemuacha Azam zaidi ya points 30
 
Ukitaka kujua ushindi wa yanga huwa umepangwa mezani,subiri waende kimataifa ndio utajua tunachoongea.

Kifupi huo ni ubingwa wa GSM na siyo wa yanga.
Utaona jinsi atakavyoumbuka kimataifa
Kwani nyie Makolo huko kimataiga mmechukuwa kombe gani zaidi ya kulitia Taifa letu aibu kwa vipigo vikali..
Yanga tunaweza dadeq Dunia yote inafahamu hvyo.. Timu pekee ambayo haijafungwa kwenye ligi, nyie Makolo mnaweza haya..?
 
Back
Top Bottom