Hivi, kweli kabisa Vyombo vya Ulinzi na Usalama waliamini Polepole yuko Tanzania?

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
376,316
Reaction score
871,876
Majira ya saa tano usiku wa jana walivamia kwa dadaake na Polepole kwa kile kinachosemwa kusaka taarifa! Uhalisia ni kwamba "walipangwa" wakapangika wakaingizwa cha city kwamba muhuni yuko nchini

Nina hakika walishakagua entries zote na kujiridhisha kwamba muhuni hajazitumia.. Ila kwakuwa hawaaminiani "wakadhani" muhuni kapitishwa njia ya panya..

Na kule nyumbani kwa dadaake walikovamia kumbe inasemekana kulikuwa na concealed cameras hivyo wamejulikana wote

Only professionals can act professionally... Wamebug big time?
 

Wengine wanasema yupo miami USA banda ya kupewa ile namba.

Nilichogundua tuiombee nchi yetu Amani idumu milele .
 
Wanaendeshwa kwa mihemko, maagizo. Hawawezi kufanya kama kazi yao inavyowataka. Iwe Idara au policcm. Ukiangalia ni sheria ipi Polepole amevunja, mpaka wanamtafuta?

Hawataki watu waseme ukweli, wanachotaka kusikia sasa hivi, ni kusifia tu!!! Hawezi kutenda mabaya, watu wasiseme, watasema tu. If you can't stand the heat, get out of the kitchen.
 
naamini walitaka kuchukua ndugu zake kama ramsom ili asiongee, wamekosa nini sasa? ndio hao kosa la gwajima adhabu wanapewa waumini. kosa la polepole,mange au maria sarungi (kama kweli wangekuwa na kosa) lakini adhabu wanapewa watanzania wote kwa kufunga mitandao. hawajui humo kwenye mitandao wengine ndio wanapata pesa ya kula, wanahubiri wanafanya yote. mfano, wakifunga youtube leo au facebook, sisi tunaosali tutapata shida kwa sababu tunapata mahubiri humo, tunapata na nyimbo. imagine taifa kubwa lenye vyombo vyote vya ulinzi wanaweweseka kwa viwatu vinna au kumi tu hadi kufungia mitandao yote, nadhani wanataka watanzania wasijue wala kuona chochote, waishi gizani tu ili wao wawafanye wapendavyo.
 
Mkuu Mshana Jr . Hivi unadhani ''hawa watu'' wana akili? Tukiona wanavyoteka na kuua vijana wadogo kabisa wasio na hatia tunaweza kudhani wana akili hata za kuvukia barabara? Ukiona wanapiga picha eti wakifuatilia ''kesi'' ya Lissu unadhani kuna ubongo hapo? Yaani kwangu mimi nadhani kuna kikundi cha watu wajinga kabisa, na possibly kinasimamiwa na wajinga wenzao (may be mzee wa mapete na Abdul?) kufanya operation. Hivi hata kuzima mitandao leo ilikuwa ni lazima?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…