Nadhani Tanzania bado ni darasa na shule kuu ya kipekee mno ya demokrasia barani Africa. Ni nchi pekee ya wananchi wasiozingatia ukabila, ukanda wala rangi ya mtu kwenye uchaguzi.
Shukrani za kipekee ni kwa Baba wa Taifa Mw.J.K Nyerere kutujengea kama Taifa, utamaduni, mila na desturi hii ya kutokubaguana kulingana na misingi isiyofaa, iliyotuepusha na ubaguzi wa aina zote na kuchochea utu, heshma, haki na usawa kwa binadamu wote...
Kama Taifa, hatuna budi kuitunza na kujivunia tunu hii muhimu sana, iliyokijita ndani ya mioyo ya waTanzania na inayotufanya kijilikana na kufahamika duniani kama kisiwa cha amani.
La muhimu ni AMANI na kwamba kasoro na dosari katika uchaguzi haziepukiki.
Mungu Ibariki Tanzania