Hivi kweli kuna cha kujifunza kutokana na uchaguzi wa Afrika Kusini kama taifa?

Hivi kweli kuna cha kujifunza kutokana na uchaguzi wa Afrika Kusini kama taifa?

Kwenye Press iliyopita ya EFF, Kiongozi wa EFF Julius Malema kadai wapo tayari kushirikiana na ANC. Shida ya huu Muungano wa ANC na EFF ni kwamba wote ni rejects. ANC kashuka mpaka asilimia 40, na huku EFF kashuka mpaka asilimia 9. Hivyo wakiungan itakuwa Muungano wa mabwege. Labda ANC aungane na MK hapo kidogo nguvu itarudi.

Pia Kwa taarifa za Chini Chini zinadai ya kwamba ANC na DA wapo kwenye maongezi ya awali ya kuunda serikali ya mseto ingawa itakuwa ngumu kidogo kwa wa ANC wenye msimamo mkali.
ANC atapendelea zaidi aungane na mwenye kuchangia kidogo tu ili atimize ile simple majority ya wabunge 200+1 ili Ramaphosa aingie muhula wa pili, lakini ili pia kwenye makubaliano ya kuunda serikali asitoe share kubwa zaidi kwa mshirika wake 🐒

MK party wametoa sharti kwamba ili wangune na ANC Lazima Ramaphosa angatuliwe kwanza....

Kwahivyo naona uwezekano mkubwa ni EFF na huenda chama kingine lakini sio DA🐒
 
Ni kama Nigeri wanavyohangaika kwa Sasa. Imebakia urais ni Kwa watu wa kaskazini maana ndio wengi. Wale wa kusini walipotaka kujitenga na kuanzanisha nchi ya Biafra Chini ya Dudumeju Ojwuku walishugulikiwa na jeshi la Nigeria. Mpaka Leo Nigeria haija settle wanawaona wa Igbo kama sio wanaigeria.
dah ukabila ni dhambi mbaya mno aise 🐒
 
Wewe hushangai chama Cha kibaguzi kuwa Cha pili kwenye nchi ya waeusi asilimia 80 na zaidi?. Tafakali Hilo kwanza.
Ukiangalia mijadala ya wasouth wameanza kuiona DA Kama suluhisho la matatizo yao. Halafu kumbuka kinavhofanya DA isipate asilimia hamsini ni ile chuki ya ubaguzi hapo tu.
Kwanza tuweke sawa kumbukumbu: Democratic alliance sio kile chama cha kibaguzi kilichotawala South africa mpaka 1994. Kile kilikuwa kinaitwa National party. Soma hapa chini:

"The New National Party (NNP) was a South African political party formed in 1997 as the successor to the National Party, which ruled the country from 1948 to 1994. The name change was an attempt to distance itself from its apartheid past, and reinvent itself as a moderate, mainstream conservative and non-racist federal party. The attempt was largely unsuccessful, and in 2005 the New National Party voted to disband itself" (hii ndio 7% unayoisema) Hiki chama hakikusamehewa kabisa na wa-south Afrika mpaka umauti ukakikuta licha ya kubadili jina.

DA kinajitambua kama chama cha ki- Liberali. Matokeo ya safari hii si ya kushangaza sana kwani chaguzi za nyuma kilipata kama ifuatavyo 2009 (16.66), 2014 (22.23%), 2019(20.8%).

Kwa faida ya msomaji ili asikichanganye hiki chama na kile cha makaburu soma hapa chini:
"The Democratic Alliance (DA; Afrikaans: Demokratiese Alliansie) is a South African political party and the official opposition to the ruling African National Congress (ANC). The party is broadly centrist,[3][4] and has been attributed both centre-left[5] and centre-right[6] policies. It is a member of Liberal International and the Africa Liberal Network. The DA traces its roots to the founding of the anti-apartheid Progressive Party in 1959, with many mergers and name changes between that time and the present. The DA ideologically shows a variety of liberal[7] tendencies, including neoliberalism,[8] social liberalism,[9] classical liberalism,[9] and conservative liberalism" Source Wikipedia.
 
Nadhani Tanzania bado ni darasa na shule kuu ya kipekee mno ya demokrasia barani Africa. Ni nchi pekee ya wananchi wasiozingatia ukabila, ukanda wala rangi ya mtu kwenye uchaguzi.

Shukrani za kipekee ni kwa Baba wa Taifa Mw.J.K Nyerere kutujengea kama Taifa, utamaduni, mila na desturi hii ya kutokubaguana kulingana na misingi isiyofaa, iliyotuepusha na ubaguzi wa aina zote na kuchochea utu, heshma, haki na usawa kwa binadamu wote...

Kama Taifa, hatuna budi kuitunza na kujivunia tunu hii muhimu sana, iliyokijita ndani ya mioyo ya waTanzania na inayotufanya kijilikana na kufahamika duniani kama kisiwa cha amani.

La muhimu ni AMANI na kwamba kasoro na dosari katika uchaguzi haziepukiki.

Mungu Ibariki Tanzania :whatBlink:
DEMOCRASIA YA WIZI WA KURA? ACHA UJINGA
 
Kikubwa tunachojifunza katika uchaguzi huu na safari ya ANC toka 1994 ni mambo matatu makubwa:
1) Umaarufu wa chama cha siasa hutokana na ukali wa mbwembwe/propaganda, lakini thamani ya chama cha siasa hutokana na utendaji wa kazi katika kutatua matatizo ya wananchi.
2) Kugombania madaraka katika chama ni dalili mbaya ya uhai wa chama.
3)Wananchi ndio mwisho wa siku ndio wanaoamua nani awaongoze, japo inaweza kuchukua muda miaka 30 au 60 au zaidi lakini mwisho wa siku wakikuchoka wanakutosa.
 
Mambo ya kujifunza ni mengi.
Hakuna wizi wa kula,tume ya uchaguzi ipo vizuri.
Pili Matarajio ya kuanguka kwa ANC kumetimia watahitaji ubia na vyama pinzani ili kuunda serikali.
Tatu wananchi walio wengi wamechoka na ahadi hewa,rushwa,uzembe wa serikali ya ANC.
Nne usalama wa raia na mali zao ni mdogo.Vikundi vya kiarifu vinatishia maisha ya watu.
Tano kadiri uchumi unavyozidi kuyumba,wawekezaji wamehamisha mitaji yao na kuipeleka nchi nyingine hivyo kuleta uhaba wa ajira kwa mamilioni ya watu.
Sita wahamiaji haramu na wakimbizi wamefurika kulemea huduma za msingi kumesababisha ugumu wa maisha kwa wananchi wa Africa kusini.
Mategemeo ya wananchi weusi kumiliki njia kuu za uchumi kwa zaidi ya miaka 30 toka wapate uhuru imegonga mwamba.
 
Nadhani Tanzania bado ni darasa na shule kuu ya kipekee mno ya demokrasia barani Africa. Ni nchi pekee ya wananchi wasiozingatia ukabila, ukanda wala rangi ya mtu kwenye uchaguzi.

Shukrani za kipekee ni kwa Baba wa Taifa Mw.J.K Nyerere kutujengea kama Taifa, utamaduni, mila na desturi hii ya kutokubaguana kulingana na misingi isiyofaa, iliyotuepusha na ubaguzi wa aina zote na kuchochea utu, heshma, haki na usawa kwa binadamu wote...

Kama Taifa, hatuna budi kuitunza na kujivunia tunu hii muhimu sana, iliyokijita ndani ya mioyo ya waTanzania na inayotufanya kijilikana na kufahamika duniani kama kisiwa cha amani.

La muhimu ni AMANI na kwamba kasoro na dosari katika uchaguzi haziepukiki.

Mungu Ibariki Tanzania :whatBlink:
Cha kujifunza hapa ni jinsi chama cha ukombozi kinaweza kubakia madarakani licha ya kua kimesaliti malengo na itikadi yake kutokana na ulaghai uroho na ubinafsi wa viongozi wake. Chama kilikua kinaanguka taratibu ila kutokana na fisadi mkabila zuma kuwatoa wazulu kuiunga mkono ANC basi tena ndio mwisho wa utawala wake. Mjue nyuma ya pazia makaburu wana nguvu kubwa ndio maana uchumi bado wanamiliki pia ubaguzi wa rangi bado upo japo sio ule wa apartheid.
 
Nadhani Tanzania bado ni darasa na shule kuu ya kipekee mno ya demokrasia barani Africa. Ni nchi pekee ya wananchi wasiozingatia ukabila, ukanda wala rangi ya mtu kwenye uchaguzi.

Shukrani za kipekee ni kwa Baba wa Taifa Mw.J.K Nyerere kutujengea kama Taifa, utamaduni, mila na desturi hii ya kutokubaguana kulingana na misingi isiyofaa, iliyotuepusha na ubaguzi wa aina zote na kuchochea utu, heshma, haki na usawa kwa binadamu wote...

Kama Taifa, hatuna budi kuitunza na kujivunia tunu hii muhimu sana, iliyokijita ndani ya mioyo ya waTanzania na inayotufanya kijilikana na kufahamika duniani kama kisiwa cha amani.

La muhimu ni AMANI na kwamba kasoro na dosari katika uchaguzi haziepukiki.

Mungu Ibariki Tanzania :whatBlink:
Ndio, Mwisho wa vyama "VIKONGWE" umekaribia, wajitayarishe kisailolojia soon nao wataitwa vyama vya "UPINZANI"
 
ni vizuri kujipanga hasa na kua na consistency katika kupigania mambo muhimu, vinginevyo ikiwa leo unadai hile kesho jingine, utafika umechoka sana 🐒
Katiba mpya na tume huru ya uchaguzi imepaganiwa kwa miaka zaidi ya 30 Sasa. Je zimepatikana? Sema utakavyo bado uchaguzi wa Africa kusini umekuwa na utabaki kuwa bora kuliko huu upuuzi unaoendelea hapa nchini.

Huko Africa kusini uchaguzi wao mshindi anapatikana kwa sera zake, hapa kwetu mshindi anapangwa na genge linalojiita system, na uchaguzi ni kiini macho ili kuhadaa umma kuwa Kuna uchaguzi/demokrasia.
 
uko sahihi ila ungwana ni zero...

inafaa ifanyike bidii ya ushawishi na kubadili mindset za wengi kua upande wako, kuliko kubeza anachoamini mwingine kwenye chama au taasisi yake....

mi naona, hii ya sijui habari nyumbu au sijui chawa ni useless kabisa, haisaidii wala kubadili kitu. Lazima kuwepo na content za maana za kumshawishi na kuvutia wengi 🐒

kwamba uungwe mkono wasababu ya uhodari wa kumuita mwingine chawa au nyumbu au kabila lako?🐒
Kwani uchaguzi wa hapa mshindi anapatikana kwa nguvu ya ushawishi, au matakwa ya chama kilichopo madarakani? Ingekuwa ni ushawishi Wala ccm isingekuwa madarakani, ama kuwa na wingi usioakisi ushawishi wao halisi.
 
Ndio, Mwisho wa vyama "VIKONGWE" umekaribia, wajitayarishe kisailolojia soon nao wataitwa vyama vya "UPINZANI"
Ccm bado iko madarakani sio kwasababu ya kukubalika kwake, bali ni kutokana na uoga wa wananchi wa nchi hii, uwepo wa tume isiyo huru ya uchaguzi na katiba hii ya mfumo wa chama kimoja.

Ni aidha machafuko ama mapinduzi ya kijeshi ndio tutapata mabadiliko ya kweli, lakini kuendelea kushiriki hizi chaguzi za kishenzi, ni kuipa uhalali ccm isiostahili.
 
Back
Top Bottom