Hivi kweli kuna cha kujifunza kutokana na uchaguzi wa Afrika Kusini kama taifa?

Hivi kweli kuna cha kujifunza kutokana na uchaguzi wa Afrika Kusini kama taifa?

Kwani uchaguzi wa hapa mshindi anapatikana kwa nguvu ya ushawishi, au matakwa ya chama kilichopo madarakani? Ingekuwa ni ushawishi Wala ccm isingekuwa madarakani, ama kuwa na wingi usioakisi ushawishi wao halisi.
No,
hupaswi kukata tamaa hata kidogo wala kulalamika katika kutafuta mabadiliko 🐒
 
Ccm bado iko madarakani sio kwasababu ya kukubalika kwake, bali ni kutokana na uoga wa wananchi wa nchi hii, uwepo wa tume isiyo huru ya uchaguzi na katiba hii ya mfumo wa chama kimoja.

Ni aidha machafuko ama mapinduzi ya kijeshi ndio tutapata mabadiliko ya kweli, lakini kuendelea kushiriki hizi chaguzi za kishenzi, ni kuipa uhalali ccm isiostahili.
hicho cha kufanya mapinduzi kiko wap?🐒

majeshi yetu yako cultured, yako disciplined mno hakuna wa kuweza kuthubutu hata kuskiza tu wenyewe mentality kama yako 🐒
 
No,
hupaswi kukata tamaa hata kidogo wala kulalamika katika kutafuta mabadiliko 🐒
Usichanganye kukata tamaa na kupuuza chaguzi za kishenzi. Ndio maana nasema machafuko ama mapinduzi ya kijeshi ndio yataleta mabadiliko.
 
ANC atapendelea zaidi aungane na mwenye kuchangia kidogo tu ili atimize ile simple majority ya wabunge 200+1 ili Ramaphosa aingie muhula wa pili, lakini ili pia kwenye makubaliano ya kuunda serikali asitoe share kubwa zaidi kwa mshirika wake 🐒

MK party wametoa sharti kwamba ili wangune na ANC Lazima Ramaphosa angatuliwe kwanza....

Kwahivyo naona uwezekano mkubwa ni EFF na huenda chama kingine lakini sio DA🐒
Sijui kama watawezana . Maana EFF hawatabiriki. Pia EFF wanataka kurudi kwenye mstari hivyo kuwa sehemu ya serikali kutawa boost Sana.
 
hicho cha kufanya mapinduzi kiko wap?🐒

majeshi yetu yako cultured, yako disciplined mno hakuna wa kuweza kuthubutu hata kuskiza tu wenyewe mentality kama yako 🐒
Kama 1982 walitaka kupindua tena chini ya Nyerere, itakuwa kwa Hawa wagawa bandari?
 
Kikubwa tunachojifunza katika uchaguzi huu na safari ya ANC toka 1994 ni mambo matatu makubwa:
1) Umaarufu wa chama cha siasa hutokana na ukali wa mbwembwe/propaganda, lakini thamani ya chama cha siasa hutokana na utendaji wa kazi katika kutatua matatizo ya wananchi.
2) Kugombania madaraka katika chama ni dalili mbaya ya uhai wa chama.
3)Wananchi ndio mwisho wa siku ndio wanaoamua nani awaongoze, japo inaweza kuchukua muda miaka 30 au 60 au zaidi lakini mwisho wa siku wakikuchoka wanakutosa.
Kweli kabisa mkuu
 
Nadhani Tanzania bado ni darasa na shule kuu ya kipekee mno ya demokrasia barani Africa. Ni nchi pekee ya wananchi wasiozingatia ukabila, ukanda wala rangi ya mtu kwenye uchaguzi.

Shukrani za kipekee ni kwa Baba wa Taifa Mw.J.K Nyerere kutujengea kama Taifa, utamaduni, mila na desturi hii ya kutokubaguana kulingana na misingi isiyofaa, iliyotuepusha na ubaguzi wa aina zote na kuchochea utu, heshma, haki na usawa kwa binadamu wote...

Kama Taifa, hatuna budi kuitunza na kujivunia tunu hii muhimu sana, iliyokijita ndani ya mioyo ya waTanzania na inayotufanya kijilikana na kufahamika duniani kama kisiwa cha amani.

La muhimu ni AMANI na kwamba kasoro na dosari katika uchaguzi haziepukiki.

Mungu Ibariki Tanzania :whatBlink:
Kichwa cha habari na mchango wako ni vitu viwili tofauti kabisa! Kwani ulilenga nini!?!
 
Kwanza tuweke sawa kumbukumbu: Democratic alliance sio kile chama cha kibaguzi kilichotawala South africa mpaka 1994. Kile kilikuwa kinaitwa National party. Soma hapa chini:

"The New National Party (NNP) was a South African political party formed in 1997 as the successor to the National Party, which ruled the country from 1948 to 1994. The name change was an attempt to distance itself from its apartheid past, and reinvent itself as a moderate, mainstream conservative and non-racist federal party. The attempt was largely unsuccessful, and in 2005 the New National Party voted to disband itself" (hii ndio 7% unayoisema) Hiki chama hakikusamehewa kabisa na wa-south Afrika mpaka umauti ukakikuta licha ya kubadili jina.

DA kinajitambua kama chama cha ki- Liberali. Matokeo ya safari hii si ya kushangaza sana kwani chaguzi za nyuma kilipata kama ifuatavyo 2009 (16.66), 2014 (22.23%), 2019(20.8%).

Kwa faida ya msomaji ili asikichanganye hiki chama na kile cha makaburu soma hapa chini:
"The Democratic Alliance (DA; Afrikaans: Demokratiese Alliansie) is a South African political party and the official opposition to the ruling African National Congress (ANC). The party is broadly centrist,[3][4] and has been attributed both centre-left[5] and centre-right[6] policies. It is a member of Liberal International and the Africa Liberal Network. The DA traces its roots to the founding of the anti-apartheid Progressive Party in 1959, with many mergers and name changes between that time and the present. The DA ideologically shows a variety of liberal[7] tendencies, including neoliberalism,[8] social liberalism,[9] classical liberalism,[9] and conservative liberalism" Source Wikipedia.
Asante mkuu. Nilikuwa namjibu jamaa hapo juu aliyedai DA ni chama Cha kibaguzi. Nikamwambia kwanini hashangai DA kuwa chama Cha kibaguzi halafu kikawa Cha pili?. Yani watu wachague chama Cha kibaguzi kiwe Cha pili?. Ila DA ndio suluhisho la South Africa.
 
Kweli. Kwa Sasa coalition politics ni muhimu hasa kwa vyama vya upinzani.
that's it,
binafsi nahitaj opposition inayochallenge the ruling party to expand its plans and efforts wanainchi wapate development, otherwise ipigwe chini but through issues 🐒
 
Acha kabisa mkuu. Ukabila ndio unaitesa Kenya mpaka Sasa, inabidi ukitaka kuwa Rais lazima uende kwa Wakikuyu kwanza au wakalenjin. Hivyo urais umebaki kwa Wakikuyu na Wakalenjin basi.
aise ni hatari,
kama saivi vita ya deputy president RigGy na Boss wake Rais Ruto hadi huruma 🐒
 
Kama 1982 walitaka kupindua tena chini ya Nyerere, itakuwa kwa Hawa wagawa bandari?
hakuna ambacho kingefanikiwa hata chembe. By the way mapinduzi attempts zilifanyika zaidi ya hiyo but ilikua ngumu na itakua ngumu mno as we go on 🐒
 
Back
Top Bottom