Kama unamtaji wa kutosha ama una mategemeo ya kupata ajira hivi karibuni chagua kazi. Ila kama huna kitu usichague cha kufanya fanya kitu chochote cha halali ambacho kinatoa pesa.
Mtu huna cha kupoteza, huna pesa why unaogopa?? Mimi hiyo hiyo forex na betting ndio nilikuwa nafanya wakati sina mtaji maana ndio sehemu za kupata au kupoteza pesa fasta fasta. Hizo sijui Apwork mpaka utafute kazi mtu akupe sio leo wala kesho.
Siwezi sema ni bahati ilianguka upande wangu nikapata mtaji hapana maana nilikuwa natumia akili na pesa niliwekeza ndio nikapata kitu. OOh mwingine atasema forex ni gambling yeah nikama gambling lakini sina kitu nifanye nini kama tuu kazi ya 150k unazunguka dar nzima hupati na unadegree ufanye nini.
Kwenye hizi kazi za kawaida napo nipagumu sana labda uwe na ujuzi mfano ufundi simu au tajiri akupe chombo uendeshe ,hata ukondakta uliouandika hapo kupata sio rahisi mpaka uwe na connection tena kali na dereva bila hivyo utaambulia manyoya
Mimi nina store ya nafaka kila kwenye kilo moja ya mchele faida ina range 200-300 ili uone faida lazima uuze kilo nyingi nyingi sana nahapo kodi ya fremu,tra tfda ,halmashauri,umeme ,zima moto ,mlinzi vyote vitoke humo . Bado kodi ya mimi niliko panga + usafiri ukipiga mahesabu unajikuta unafanyia tumbo.
Hao wanaopenda kukaa ofisini na kusubiri mishahara sio wajinga asee. Nikaona bora niongeze wigo wa biashara nilime mazao mfano maharage mimi mwenyewe niwe nakuja kuyauza, juzi tu hapa ndio nimetoka kuvuna msimu wa pili mfululizo naambulia hasara.
View attachment 1821683