Hivi kweli kuna watu wanapiga hela online? Mimi naona kama uzushi tu!

Kwa ujumla wake kufanya Youtube inaitwa Vlogging kwa maana ya kutengeneza videos na kuweka YouTube
Ahsante mkuu, nilikuwa nafikir ni specific content, mm ni Youtuber na youtube ina ela mno, lakin sio Kazi ndogo,inaitaj uwekezejaj wa muda, nguvu na ela, Kazi yangu ni Youtube,nalipa kodi nakula navaa sina shughuli nyingine zaidi ya Youtube na Blogging, uyo anaesem Online we specifi ni online gan anayosema maana online kuna Vijiwe vingi sana, kama aliingia kijiwe cha wanywa kahawa ambao wanastory za uongo lazima aseme online hamna ela[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Wengi wanaosema online hakuna pesa ni wale wanaotegemea kupata pesa kwa kubofya tu na kushare scams mtandaoni.
 
Wengi wanaosema online hakuna pesa ni wale wanaotegemea kupata pesa kwa kubofya tu na kushare scams mtandaoni.
Siyo kila kazi au business inayofanyika online lazima kila mtu aiweze/aifanye. Kila mtu afanye anachoona anaweza. Kuna options nyingi sana za kufanya na kupata fedha online tatizo tutataka kuforce kufanya mambo ambayo siyo interest/hobby/profession yetu kisa tu umesikia kuna hela. Na hii siyo tu kwenye online business hata mtaani wengi biashara wanafanya kwa kuiga au kukurupuka kisa kasikia hiyo biashra inalipa (matikiti maji, kuku, nguruwe, mayai ya kwale etc). Hakuna hela rahisi kuipata online au mtaani ni lazima ufanye kazi kwa kujituma kama zilivyokazi nyingine.
 
[emoji16][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mkuu fanya unaloweza kama wewe huwezi jambo wapo wanaoweza. Huwa sipendi watu wanao generalize mambo kwa sababu tu yeye kashindwa basi ana assume dunia nzima hakuna anayeweza. Kila jambo hapa duniani liwe zuri au baya wapo wanaweza kulifanya na wakafaidika na pia wapo wasioweza. Tafuta unachoweza kufanya kama online business zimekushinda waachie wanaoweza wapambane.
 
Online hakuna hela wewe ,mbona unataka kutuaminisha kuwa watu wanapiga helaa sanaa
 
Yaaah kama ni hizi ,basi hela ipo ....

But mimi nafuatilia rafiki zangu wote kutwa status wanajimwambafi wanafanya online business ....

Fuatilia sasa uone ,utasikia forex,smart hela ,pamafund ....

Daa unabaki unashangaa ....
Kwa hiyo wewe unajaji business kwa kusikia tu kwa watu wengine? Ndio maana biashara nyingi zinafail kwa sababu hazina msingi mzuri. Watu wanaanzisha biashara kwa hearsay za watu wengine siyo kwamba wafanya research/survey wakajua kwamba kweli hiki kitu kina faida. Kwa mentality za namna hii kamwe kupigwa kutaendelea tu iwe online au manualine.
 
Ndugu pesa ipo.

Nakushauri pata ujuzi wa kutosha (knowledge and skills) hela ipo.

Nina uzoefu na hivyo vitu
 
Nothing is easy.
Cryptocurrency- yenyewe ni investing ya muda mrefu kwa mfano if you bought Bitcoin last year ikiwa USD 3000 leo hii ni dollar 36000 kama ulinunua ya dollar 100 now una dollar 3600. Though its not easy Kuna ups and downs inahitaji uwe na mishe zingine za kufanya and you invest for fun.

Though kiukweli technology behind crypto ni convincing halaf bado ipo in very early stages Kuna uwezekano in the future ikatengenza millionaires wengi kama kukiwa na massive adaptation. The opposite is true pia.

Cryptocurrency kama XRP unaweza ukamuhamishia mtu sehemu yoyote within seconds kwa makato almost zero. Hizi crypto ni medium of exchange kama zilivyo pesa au dhahabu, silver pia price zake zinacontroliwa na demand na supply tofauti na currency za kawaida ambazo price zake zinacontroliwa na governments au Central banks.
Yaani Thamani ya dollar moja itabaki kuwa hivyo hivyo sana sana itapungua value miaka kadhaa nyuma ukiwa na dollar moja ungeweza pata sukari hata kilo ila Leo hii hata robo hupati. Tofauti na cryptocurrency ambazo thamani zake zinapanda with time kulingana na demand.

Forex trading yenyewe pia ni currency exchange pia ukiwa na right knowledge you can make good income. Wapo watu wengi wanatengeneza income kupitia forex.

Wabongo tunapenda mteremko unataka uweke pesa yako kwenye forex ubonyeze buy or sell udownload pesa sio rahisi kihivyo.
Unaweza ukalima vitunguu , nyanya na ukapata hasara kuliko hata anayefanya forex. Watu wangapi wanafunga maduka yao.

Unaweza ukajenga nyumba yako mil 100 ukaipangisha Kodi laki 3 kwa mwezi itakuchukua takribani miaka 3 ili uanze kupata faida lakini unataka uweke laki 1 forex halafu uwe unaingiza laki 4 kwa mwezi immediately. Laki 1 inatakiwa ikuingizie walau elfu 10000 per month and it's very possible ukiwa na good stratergy. Sema greediness ndo inafanya watu wafeli kwenye forex.
 
Ndugu.

Hivi vitu forex na crypto vyote ni vigumu na vyote ni virahisi ukiwa na knowledge.

Tofauti ni kwamba.
Forex ukipoteza unapoteza kabisa, Crypto huwezi poteza kabisa unless uwe na tamaa au upate changamoto.
Nawashauri tuwekeze sana kwenye cryptocurrency sababu bado n changa sana.

Baada ya miaka mitano hivi tutaona jinsi itakavyojipambanua.

Knowledge is wealth!
 
YouTube nayo watu walidharau leo hii wakiwaona wakina milard ayo walipofikia wanajutia.

Hizo affiliate pia utashangaa baadaye ndo watu wanashtuka then itakuwa too late.

Bitcoin humu JF ilianza kuongelewa ikiwa hata haijafika dollar 100 leo hii ipo dollar 36000. Utasikia ni scam or utapeli.

Wanawadharau wanaofanya forex kwa kuwa wao walipata hasara wanadhani watu wote wanapata hasara.

Wanataka Kila mtu alime vitunguu, afungue Banda la chipsi, aendeshe boda nk. Dunia inakuwa lazima kuwe na diversites.

Wenzetu unakuta dogo wa miaka 7 anaingiza milions kwa kucheza games YouTube. Mtu akiingia kwenye mtandao anaingiza pesa tu. Huku bongo asilimia nyingi tunatumia mitandao kuangalia udaku insta.

Unakuta mtu ni daktari, lawyer, engineer lakini Ana channel yake YouTube anafanya vlogging kama part time or anacreate educational contents. Wengine wanaimba wanafanya covers za nyimbo na wanapata extra income. Wengine wanapromote bidhaa mbalimbali instagram. Wanatumia mitandao productively.

Huku sisi tunafatilia udaku tu, habari za kina uwoya unakuta mtu amefollow wasanii tu home page nzima wakati huo wasanii wanatumia page zao kuingiza pesa, kujitangaza, wanafanya matangazo wanaingiza pesa. Wewe unabaki kusema hakuna pesa online.
 
Kinachowatafuna wengi leo n Lack of Information
Wengi hatuna taarifa sahihi kuhusu hii kitu.

Baadhi wameingizwa mkenge na Scams mbalimbali ambazo zilijificha chini ya mgongo wa Bitcoin. (Bitcoin) ikatumika kama njia ya malipo hivyo inaonekana n utapeli.

Kumbe mtu angeamua kufatilia ni asset nzuri sana.

Hata hivyo Bado ni mapema sana mtu anaweza pata maarifa haya vizuri akaanza kuwekeza polepole.

Uzuri ni kwamba haikuchukulii muda au nafasi.
Maana kila kitu kinafanyika kwenye simu yako.
 
Taja online busines tofauti na nilizotaja hapo juu ....

Mkuu tafadhari naomba unitajia hizo online business tofauti na hayo makundi nimeyoweka hapo juuu ...

Online kuna pesa sehemu tofauti sana. Asilimia 95 ya pesa nilizowahi kupata mimi basi nilizitoa online.
Online kuna category mbali za kufanya

Kuna kutoa huduma
Kuna kuudha bidhaa.

Unasema huamini online kuna pesa na wakati kila siku unamwona Diamond anajisifu kufikisha viewers milion 1?


Hizo ulizotaja kuna watu wametajilika hapo.

Mfano hiyo ya Sarafu za kidigitali

Mwaka 2018 ilikuwa kama laki 3(Bitcoin 1) hivi ya kibongo.
Kuna watu walikuwa nazo kama 4 hivi.

2021 Bitcoin imefikia Usd 47,000+ zaidi ya milion 120Tsh.

Kwenye kelele za sijui tunapiga hela online ni tabia tu ya wabongo.
Yaani kama alipata laki moja basi inakuwa story ya miaka miwili kwamba tunapiga hela na mbwembwe kama hizo.
Siku wakipoteza kwenye hizo mambo zao hawasemi kwamba hii bizz za online kuna lisk ya kupoteza pia.

Kwahiyo kelele zinazokuwa zaidi ni hizi za tunapiga hela achaa.

Pesa online zipo nyingi. Cha msingi elewe zipo sehemu gani?
Kwa kufanya nini?
 
 
Hiyo kauli yako ya mwisho inaonyesha bado upo gizani.....pole sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…