pCpCp RICH THINKER
Senior Member
- Apr 5, 2021
- 121
- 103
Habari wakuu
Maisha kwa sasa yanaenda kasi sana, Sisi vijana katika harakati za kutafuta pesa tunakutana na changamoto nyingi sana ,sasa kuna hii njia inaitwa "kupiga hela online ,ukiwa na simu yako na bando " Mimi nimeshafanya uchunguzi sana online businesses wanazosema ni zipi hizo au ni hizi ...
Cryptocurrency (sarafu za kidigitali)..
Forex ..
Betting ..
Nyingine ni network marketing ,huku utakutana na website zinatokea na kucollapse watu wanapigwa hela ,ila kutwa status kupost eti wanapiga hela eg ,pamafund ,smarthela ,global alliance ,qnet ,forever living ....
Kuna mengine mengi yanaibuka na kutoweka kwa kweli mpaka nabaki mdomo wazi na watu wanaweka hela huko ,wanapigwa ,ila ni full kujipa moyo et wanapiga hela ,wanasema wanapiga hela wakiwa wamelala kitandani ....
Hawa watu wa online wanawaona wauza mihogo ,machinga ,wauza migahawa ,wauza matunda ,chips ,washona viatu ,wapiga debe ,....hao wote wanawaona kama hawana akili ya kutafuta hela ,ila wao ndio wanajua hahaaaaaa....
Kusema kweli kama online business watu wanazosema ndio hizo hapo juu ,sina budi kusema kuwa ,watu wanaofanya hayo mavitu ni wavivu wa kufikili na "HAWATAKUJA KUFANIKIWA MPAKA MWISHO WA DUNIA"...
Yaani wanapigwa pesa mpaka akili ziwakae sawa, ..
Hakuna pesa za bure online, Fanya kazi kwa bidii, jitume, ndio njia ya kupata pesa ..
Forex ingekuwa biashara, serikali ingechukua $100,000 ikawaintrade na kutengeneza pesa ,...
Sarafu za kidigital zingekuwaa deal, hakuna tajiri ambaye angepoteza pesa kufungua kiwanda ,kulipa wafanya kazi, kodi, aridhi, na mabilion ya pesa wakati angeweza kununua hizo sarafu ..
Mh Raisi naamini atashauriwa vizur kuhusu hizo sarafu ..
Vijana tokeni nje, mkafanye kazi, ardhi ipo, mashamba yapo, mbegu zipo, hizo smart phone zinawadanganya,
• Tumegawanywa kisiasa tena siasa za ushabiki. Bado vijana wenzetu wengi wanaamini shilingi ina pande mbili. Katika siasa watafanya na kufikiri na kuyaona mambo yote kama 'daikotomi' fulani. Wanaowawakilisha wachache ili pengine waseme kwa niaba ya wengi kwa watu wenye maamuzi hawasemi, ama wanasiasa huingilia mchakato. Siasa za upande zinaaathiri sauti ya pamoja kama vijana. Wakiitishwa vijana waseme yanayowasibu wengi huja ki-UVCCM, ki-BAVICHA ama ki-NgomeYaVijana-ACT n.k, hoja za msingi haziguswi wanabaki kushindana. Hali hii inaanzia vyuoni mpaka huku. Tunashida!Vijana wanatakiwa kusimama wenyewe kupush agenda zao.
Sasa hivi kila mtu anaangalia maslahi yake.
Kama vijana tena wasomi kabisa hawajitambui usitegemee hata wanasiasa wakawaheshimu.
Sasa hivi serikali inaheshimu bodaboda, machinga, mama ntilie na wasanii kuliko "graduates" kwasababu graduates hawana effects.
Hawajui wanachotaka.
Kama vijana wangekuwa na agenda za pamoja, ingekuwa rahisi tu kusikilizwa. Tatizo hawana agenda, wanawekwa nyuma ya agenda zenye maslahi ya watu wengine
• Uchumi wa kidigitali. Kuna mwanaJamii forum humu aliwahi kusema “kwa sasa tuna aina tatu za ulimwengu: 1. Kimwili 2. Kiintaneti na 3. Kiroho”. Ulimwengu wa kidigitali unachukuliwa poa, kama kianasa, haupewi uzito unaostahili. Ni taasisi na kada chache ambazo zimevuna kwa ufanisi nafasi ya intaneti katika kuhudumia watu wa eneo lao k.v michezo. Sheria, sera zetu zimekuwa 'reactive' badala ya kuwa 'active' ama 'proactive'.
Eneo lakidigiti linasemwa tu nahisi kunaweza kuwa na sababu nyingi; mimi nitaje mbili. Mosi, tuna kizazi kinachoongoza ambacho ni kigeni cha teknoloji ya kidigitali. Tuna viongozi wengi ambao baada ya shule huacha kujifunza, kwa namna dunia inavokimbia hawa wanakuwa wajinga kadri siku zinavyosonga. Unyumbulifu ni mdogo, na si wepesi kuchangamkia fursa. Tuna sheria za kukomesha na kudhibiti, kwa sababu wanaoshikilia makali wanakuwa wajinga kadri dunia inavyosonga mbele kiteknolojia wao huendelea kijitutumua na vyeti vyao ili hali dunia imeawaacha.
•Umaizi wa kidigitali upo chini sana. Viongozi wengi ni wageni katika ulimwengu huu wakigitali, hususani waliokwenye nafasi. Intaneti na mitandao ya kijamii inachukuliwa katika uhasi ama ustarehe. Vijana mashuleni haaafundishwi mamboa ya twiter, facebook wala jamii forum; wameachwa wajifundishe wenyewe (wanajilindaje) lakini serikali imekuja nashiria kadhaa ili kudhibiti matumizi (inajilinda).
Kama dhima ya elimu ni kuwemwezesha mtoto kupambana na mazingira yake basi ijulikane kwamba kuna mazingira ya kimabile, kigitali na kiroho. Kwa sababu vitu vyote humwathiri mtu kwa namna moja ama nyingine ujuzi katika hayo mambo unahitajika.
•Jambo usilolijua huwa ni kama upuuzi tu. Kuna kizazi hapa ambacho kwa kweli ndo kina kontro nchi suala la mazingira ya kidigitali na TEHAMA kwa ujumla ni vitu vya kidhahania sana, halitilii maanani. Shule na taasisi vinajengwa na mahitaji ya mawasiliano ya intaneti hayapewi uzito.
•Biashara za mtandaoni ni biashara zinazohitaji mazingira mazuri ya kisera na sheria. Kwa mfano, unaweza kujifunza chochote mtandaoni na ukawa gwiji lakini ukashindwa kupata tenda sehemu fulani, wakikutaka leseni. Bado teknolojia imepewa taswira ya 'umasihara' fulani.
Kufanya 'forex' na biashara zingine sio kulala na kuamka tajiri. Shamba utalima mwaka wa kwanza, kama jipya, linaweza lisitoea mazao mengi ila mwaka wapili na watatu likaanza kuchanganya, ndivyo ilivyo mtaandaoni. Mtu anaefanya biashara mtandaoni anachukuliwa kama mvivu ama mtu ambae hajitbui na anapenda hela za mteremko. Hata hivyo, uzuri wa teknolojia huwa inajipigania, ni ngumu kushindana nayo. Pamoja na hayo hasara huwa nikuchelewa kuanza.
0759 170 823