Hivi kweli Rais Samia umedhamiria kuleta maendeleo nchini?

Huna hoja ya msingi.
 
Jamani tumekuwa vigeugeu,tulikuwa tunalia kuwa vijana hawapati nafasi leo tumepewa nafasi tena ya heshima kama hii bado tunapondana,ulitaka akae nani ndo huone kama Rais anataka kuleta maendeleo.Mkuu usihukumu kitabu kwa jalada la nje!
 
Wakati utaongea.
 
Kwa tuliyoyasikia huko Kisarawe, kama ni ya kweli basi alipobebwa, alibebeka na anastahili kama zile tetesi za kumhusisha na mtuhumiwa zitakuwa nullified and vo

Kwa tuliyoyasikia huko Kisarawe, kama ni ya kweli basi alipobebwa, alibebeka na anastahili kama zile tetesi za kumhusisha na mtuhumiwa zitakuwa nullified and void
Si kweli,madame alijitahidi kwa nafasi yake na inawezekana anayevaa viatu vyake visimtoshe,kawilaya kagumu kale
 
Kufahamiana kuhusiana vip ndugu??
Punguza kujihisi dhaifu binadamu wote ni sawa.
 
Kwa hivo mlitaka watu wa aina gani?
 
Ni kweli lakini unaangalia uadilifu wa vijana wenyewe walioteuliwa unabaki mdomo wazi!
 
Si kweli,madame alijitahidi kwa nafasi yake na inawezekana anayevaa viatu vyake visimtoshe,kawilaya kagumu kale
Nadhani nimeeleweka ni vibaya; binti Mwegelo alipopewa nafasi, kimsingi ilikuwa ni mbeleko, hakuwa wa upande huo. Mimi siko Kisarawe kujua haswa alichokifanya kwa uhalisia LAKINI kwa tunayoyasikia na zile movements za waungwana kwenda kutembelea vivutio kule, jinsi suala la zero zilivyotawanywa, ni wazi BINTI kapiga kazi na anastahili kuwepo alipo.

Imani inaanza kwa kusikia, nadhani ni huku huku JF, walisema pengine alijihusisha na bwana yule, sasa kama ikawa kweli, juhudi zake zitafifishwa na ubinaadamu wake huo.

Na mwisho, amefanya vizuri Kisarawe, ama angeendelea pale mpaka hapo ambapo tungeona amefikia bar, kisha tumpeleke sehemu nyingine remote ambapo atatupigia kazi mujarabu kama hiyo, sio mbaya akipewa special incentives kwaajili hiyo; kumleta Dar ni kumharibu, anao ujinga ujinga ambao hapa utakuwa amplified na kumpotezea umakini, lakini ukweli kwamba miamba yote iko hapa, itamuwia ugumu kutekeleza majukumu yake kwakuwa yeye si MWANASIASA.
 
Dira ya maendeleo iko na DISTRICT EXECUTIVE DIRECTOR siyo DC. DC majukumu yake ni kuhamasisha utendaji kazi, kuratibu shughuli za kiserikali kama mapokezi ya viongizi, kuzuia migogoro ya kivikundi. Ni majukumu ambayo yanaweza kuwa embedded kwa DED.

DC ni nafasi iliyorithiwa kutoka mfumo wa kikoloni wa indirect rule. Katiba mya ya wananchi rasimu ya Warioba ilipendekeza nafasi kama hii kufutwa. Viongozi wa watu wanapaswa kutokana na watu wenyewe kama walivyo kwenye nchi jirani ya Kenya.

Kwangu mimi na watu makini nafasi hii imekuwa ikitumika kama shukrani kwa baadhi ya watu ambao wamemsaidia Mteuzi au Chama Tawala.

Ningeona vizuri tupaze sauti KUFUTA nafasi za ma DC kuliko kuanza kuangalia nani kapewa u- DC.
 

Tulivyokua tunawaambia awamu hii hatuna raisi tunaishi kwa matumaini mlikua hamtuelewi? Sie wengine tumeshachoka Na hii awamu tayar
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…