Hivi Lazaro aliyefufuliwa na Yesu, alitoa ushuhuda gani kuhusu kuzimu baada ya kufufuka?

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
49,390
Reaction score
152,301
Mimi sio msomaji mzuri wa Bibilia, ila nimesikia habari ya Lazoro kufa na baadae kufufuliwa na Yesu wakati Yesu bado yuko hapa duniani na tena tunaambiwa alikuwa anatoa harufu.

Swali ni je, Lazaro alihadithia nini kuhusu kifio au hakusema chochote?

Kwa mfano, wakati anakata roho, nini hasa kilitokea?

Na je, alikufa mara ya pili au ilikuwaje?

Mwenye majibu tafadhali.
 
Maswali yako ni ya kijinga.
 
Hizo ni stori tu zisizo na kichwa wala miguu.

Lazaro hakuhadithia chochote kwa sababu hakukumbuka chochote kwa sababu hakukua na chochote.

Kuna miungu zaidi ya 3,000, stori nyingi tunazoambiwa ni kuhusu muungu mmoja wa kiyahudi. Hapo ndipo utapeli ulipo.

Mungu wa kwenye biblia ama quran hayupo.
 
Alikua anaogopa Nini Sasa na wakati alifufuka hata wangemuua si angefufuliwa tu!
Alikua anaogopa Nini kusema ukifa unaenda wapi?
Biblia imesema wayahudi walitaka kumuua sasa mimi ndio nimeweka assumption kwamba aliamua kukaa kimya. Anaweza kuwa aliwaambia watu lakini hakujawa na andiko au kumbukumbu ya hilo.

Besides, nani kakwambia kwamba unaweza ku-take advantage ya miujiza ya Mungu? Kwahiyo wewe hapo unaweza kuamka asubuhi na kuamua kuacha kazi kwasababu utapewa nyingine?
 
Mimi sio msomaji mzuri wa Bibilia, ila nimesikia habari ya Lazoro kufa na baadae kufufuliwa na Yesu wakati Yesu bado yuko hapa duniani na tena tunaambiwa alikuwa anatoa harufu...
Kupitia maandiko inaelezwa kua kabla ya yesu kufa na kufufuka, watu walikua wakifa wanaenda kuzimu wakisubiria kiama wakati wa hukumu, na kuzimu ni giza nene (huenda ni kwenye usingizi mzito).

Baada ya Yesu kufa alishuka kuzimu kuwachukua wafu (kwaajili ya hukumu) kuanzia hapo mtu ukifa moja kwa moja unaenda kupokea hukumu yako. Kwaiyo huenda lazaro alihisi ameamka kutoka usingizini kwakua alikua kuzimu.

Japo maandiko yanachanganya sana, yanasema yesu alipofufuka makaburi nayo yalipasuka na wafu wakatoka (wakafufuka). Hatujui kama walifufuka wachache au ni wote.

Tuishi humohumo tu, kama kuna sehemu nimenukuu vibaya nisamehewe sipo vizuri kwenye maandiko.
 
Mimi sio msomaji mzuri wa Bibilia, ila nimesikia habari ya Lazoro kufa na baadae kufufuliwa na Yesu wakati Yesu bado yuko hapa duniani na tena tunaambiwa alikuwa anatoa harufu.

Swali ni je, Lazaro alihadithia nini kuhusu kifio au hakusema chochote?

Kwa mfano, wakati anakata roho, nini hasa kilitokea?

Na je, alikufa mara ya pili au ilikuwaje?

Mwenye majibu tafadhali.
Huyu Lazaro anatuchanganya, niliwahi kuuliza hapa makuhani na manabii wote wa humu walikwepa kujibu
  1. Tunaambiwa Lazaro alikufa akaenda kustarehe mikononi na kifuani kwa Ibrahimu, je aliyemuona yuko na Ibrahimu ni nani? Alifikishaje hizo taarifa duniani?
  2. Lazaro alipokufa akafufuliwa na Yesu alikuwa amerudi lini toka kwa Ibrahimu?
  3. Tunaambiwa tajiri aliyemtesa Lazaro alimuomba Mungu amtume Lazaro duniani kuwaambia ndugu zake na tajiri watende mema, je hayo maneno yalishuhudiwa na nani?
 
Biblia imesema wayahudi walitaka kumuua sasa mimi ndio nimeweka assumption kwamba aliamua kukaa kimya. Anaweza kuwa aliwaambia watu lakini hakujawa na andiko au kumbukumbu ya hilo.

Besides, nani kakwambia kwamba unaweza ku-take advantage ya miujiza ya Mungu? Kwahiyo wewe hapo unaweza kuamka asubuhi na kuamua kuacha kazi kwasababu utapewa nyingine?
Maswali kama haya hatutayapatia majibu yake hata tukifa manake tutakua tumekufa!
 
Huyu Lazaro anatuchanganya, niliwahi kuuliza hapa makuhani na manabii wote wa humu walikwepa kujibu
  1. Tunaambiwa Lazaro alikufa akaenda kustarehe mikononi na kifuani kwa Ibrahimu, je aliyemuona yuko na Ibrahimu ni nani? Alifikishaje hizo taarifa duniani?
  2. Lazaro alipokufa akafufuliwa na Yesu alikuwa amerudi lini toka kwa Ibrahimu?
  3. Tunaambiwa tajiri aliyemtesa Lazaro alimuomba Mungu amtume Lazaro duniani kuwaambia ndugu zake na tajiri watende mema, je hayo maneno yalishuhudiwa na nani?
Umeniongezea maswali ndugu.
 
Back
Top Bottom