Hivi makampuni ya simu za mkopo yana mpango gani na simu zinazoondolewa mkopo?

Mtaa wetu wa Nyampulukano umekuwa mtaa wa kidigitali ghafla bin vuu

Wazawa wamekopa simu kupitia makampuni ya simu za mkopo hasa hasa simu za WATU i.e samsung A05 na A06, kisha wanamtafuta Musa Mafyekeche! anatindua mikopo hiyo, watu wanaendelea kujimwaya mwaya kama kawaida

Swali linakuja, makampuni haya yana mpango gani na watu wa aina hiyo, wasiwe wanaandaa adhabu kali sana pasi na kuutaarifu ulimwengu tukaja kushangaa watu wanapotea kusikojulikana, akiwemo mwanangu! Na je, serikali imejipanga vipi kuwatetea watu wake pindi makampuni haya ya ovyo yatakapowasha hasira zao?

Kuepuka kuingia kwenye mkenge, nimeamua kujikopea zangu ka Itel A100C kwa sababu mkopp wake hauvunjiki ili hata nikiingiwa tamaa za kuvunja, usivunjike

Labda nivunje kioo!
Dah Nyampulukano ? Nilifika sengerema mjini kununua mpunga nitunze kwenye magahala yenu nikaibiwa mtoto wa mjini na wakala ,nikaambiwa niende kwa mganga Nyampulukano karibu na secondary ya nyampurukano nikaishia kulala na yule mama mganga nikarudi zangu Dar na maumivu
 
Inasikitisha Sana.

Kwanini ukope halafu uende kutoa Lock? Mnaua biashara za watu.
We unaweza kununua simu moja kwa pesa ya kununulia simu mbili

Hakuna mtanzania mwenye mpango wa kukopa simu. Ni ushawishi wao tu, kwani wasingetuwekea yale maspika ya simu za mkopo kwa gharama nafuu sie tungeshawishuka vipi kuingia mtegoni

Kuna mahali wanakopesha simu, wakati unafanya process unapatiwa futari na soda bure, huu sio ushawishi?
 
Mtaa wetu wa Nyampulukano umekuwa mtaa wa kidigitali ghafla bin vuu

Wazawa wamekopa simu kupitia makampuni ya simu za mkopo hasa hasa simu za WATU i.e samsung A05 na A06, kisha wanamtafuta Musa Mafyekeche! anatindua mikopo hiyo, watu wanaendelea kujimwaya mwaya kama kawaida

Swali linakuja, makampuni haya yana mpango gani na watu wa aina hiyo, wasiwe wanaandaa adhabu kali sana pasi na kuutaarifu ulimwengu tukaja kushangaa watu wanapotea kusikojulikana, akiwemo mwanangu! Na je, serikali imejipanga vipi kuwatetea watu wake pindi makampuni haya ya ovyo yatakapowasha hasira zao?

Kuepuka kuingia kwenye mkenge, nimeamua kujikopea zangu ka Itel A100C kwa sababu mkopp wake hauvunjiki ili hata nikiingiwa tamaa za kuvunja, usivunjike

Labda nivunje kioo!
Yani serikali ijipange kuwatetea wahalifu?

Mkopo wa simu ni mkopo kama mikopo mingine

Ukikopa simu na kukimbia wewe ni mwalifu kama wahalifu wengine ukikamatwa lazima uadhibiwe
 
Na wao ni wahalifu. Haiwezekani umkope mtu simu halafu arejeshe pesa ya kununulia simu mbili za aina hiyo. Halafu ni kwanini ukikaribia vibanda vyao wakuvute vute, huo si utekaji nyara?

Basi sawa, 80% ya watanzania waliokopa wamevunja, basi serikali iongeze magereza ya kutosha kukabili watanzania zaidi ya 5m yaani tuwe na ufungwaji huru na wa haki, wote tuozee jera, wote!

Hawa ni matapeli tu, serikali iwafukuzie mbali, hawana tofauti na kausha damu
 
Ninachojiuliza hizi simu wanazitoa wapi? Kwamba wanaenda samsung wanawambia tutengenezee simu ya Mkopo yani inakuaje na faida wanaipataje maana hawa wanaoztoa hizi simu walikuja moja ya maduka yangu kutaka kuniachia SIMU nikopeshe tumepga hesabu Brand nazotaka na zinazotoka Mzigo umekuja wa Mil.8

Na wamenambia wananletea sitoi hata sh tano.... hiii imekaaaje yani ananletea mzgo wa 8m

Yeye aliununua kwa cash au nae alikopeshwa..hii kitu sijaielewa kwakweli
 
Simu zinauzwa bei rahisi sana huko China, simu ya laki 2 dukani kkoo China unaweza kupata kwa elfu 20

Kwahiyo wanapata super normal profit

Hata hizo za mkopo wanaibia watu, simu ya 150000 keshi kwa mkopo unalipa mpaka 380k mpaka 400k ndiyo maana wahuni wanazitoa lock kuwakomoa

Shida ni hiyo namba yako ya NIDA wakiamua kukupata wanaweza
 
We unaweza kununua simu moja kwa pesa ya kununulia simu mbili

Hakuna mtanzania mwenye mpango wa kukopa simu. Ni ushawishi wao tu, kwani wasingetuwekea yale maspika ya simu za mkopo kwa gharama nafuu sie tungeshawishuka vipi kuingia mtegoni

Kuna mahali wanakopesha simu, wakati unafanya process unapatiwa futari na soda bure, huu sio ushawishi?
Kama bei kubwa jichange kwenye kibubu ikifikia kiwango halisi nenda kanunua dukani bila mkopo.

Vigezo na msharti vimezingatiwa lakin haukuona.
 
Hii nchi kila mtu ni mwizi, tapeli na muharamia. Ni ngumu sana kuendelea kama una raia wana akili za namna hii maana hata viongozi wanatoka kwenye jamii hii hii ya watu waovu. Acha mzungu aendelee kuitawala Dunia
Inasikitisha sana kwa kweli.
Tumekuwa taifa lenye watu wa hovyo sana.
 
Hii kitu sio hapa tu hata india nimekaa india miezi 7 niliyo yaona afadhali ya hapa kule sio powa kila mtu anatumia simu ambayo kavunja mkopo ila mie naona wenyewe hupata faida pale mtu anapotoa kianzio tu next ni balaa watu hawa malizi deni ni mwendo wa unlock tool mixer baypass sio powa afu na siku hizi zile app za ku unlock ni bei rahisi sana
🤣🤣Oyaaa weeee oya weeee mwanetu mwamba sana 🤣🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom