Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 301,577
- 754,412
Waliosema maisha sio leo ni kesho walifunuliwa unabii mkubwa mno.. Ni maono ya aina yake ambayo kila anayepata nafasi ya kuwa juu ya wengine anapaswa kuyakariri vema
Maisha kamwe hayana formula .. Nimemkumbuka Gadafi na Saddam Hussein na mwisho wao ulivyokuwa.. Maisha ya ukwasi, ubabe, ulinzi na kuwa juu ya sheria..lakini wakaishia kuwa kama digidigi na ndezi.. Wakiwa hawana kikao maalum na kuishi maisha ya hofu na kuiificha
Mtu aliyewahi kujitangaza kama mla bata namba moja duniani leo hii hajulikani alipo kakimbia mkono wa sheria na mahakama imetoa kibali atangazwe kwenye vyombo vya habari kwamba anatafutwa akajibu kesi inayomkabili
Waliokuwa chawa wake, wapambe wake marafiki zake ni muda sahihi wa wao kujitokeza hadharani na kumpigania kwa namna yoyote ama la kumpa walau faraja kwamba kiongozi tuko nawe hadi mwisho.
Tulifurahi pamoja, tutalia pamoja.
Paulo Makonda kawa mkimbizi kwenye nchi yake mwenyewe! Kawa mkimbizi wa hiari.