Hance Mtanashati
JF-Expert Member
- Sep 7, 2016
- 20,137
- 26,189
Wakuu, hivi nyinyi ambao ni mashabiki wa mpira mnapenda nini haswa????
Mathalani mtu anaposema yeye ni shabiki wa timu fulani mfano Arsenal huwa anaangalia nini haswa mpaka anaamua kuwa shabiki wa timu hiyo???Kama ni aina ya mpira wanaocheza bila shaka mpira unabadilika kulingana na aina ya wachezaji ambao wapo katika hiyo timu pamoja na mbinu za kocha, sasa inakuwaje mtu ni shabiki wa timu hiyo hiyo miaka nenda miaka rudi ,tangu miaka ya 70 huko mpaka leo ,yeye anashabikia timu hiyo hiyo, wakati hata wachezaji tu huama tena unaweza kukuta kikosi kizima kikaondoka kwenda timu nyingine lakini shabiki akaendelea kushabikia timu hiyo hiyo?????
Tena mara nyingi timu inapofungwa wanaoumia zaidi ni mashabiki kuliko wachezaji, wachezaji mara nyingi huwa wanaangalia pesa zao tu timu ifungwe isifungwe wao wanaona poa tu ,tena wakati mwingine hao hao wachezaji husababisha kwa makusudi timu kufungwa kwa kula njama na timu pinzani.
Binafsi sielewi nyinyi mnapenda mpira mnapenda nini haswa kwenye mpira.