Hivi mashabiki wa mpira huwa mnashabikia nini haswa?

HONGERA SANA Utakuwa ni mtu wa kipekee sana, lazima una akili kubwa pia
Ni watu wachache sana wanagundua hilo, ni kweli michezo kwa ujumla ina faida nyingi sana
hasa kwa wale wadau husika mmoja kwa moja , mchezaji, waajiriwa wa tasisi za michezo,
mapato ya kodi, kiuchumi kama advertisements, washabiki kama burudani na kutumika kisiasa kuwapumbaza vijana n.k

Lakini ebu tuangalie upande wa pili:
1. Ulevi mbaya sana unagharimu pesa na muda hasa muda wa kazi /uzalishaji watu wanabishana kuhusu mpira na hapati pato lolote.

2. Ukanda wa pwani tanga ,Dar, Moro n.k watoto wa kiume wanashindwa kabisa ku concentrate masomo madarasani kisa ushabiki na mpira kila mtoto ana ndoto ya kuwa mchezaji bora, hii ni moja ya sbb wasichna kuongoza madarasani kuliko wavulana mtoto anakariri wachezaji ulaya yote darasani ZERO, na ukiangalia ajira zitokanazo na mpira ni 0.0002%ya ajira zote kwa ujumla

3. Mpira -USHABIKI ni chanzo cha umaskini , uzembe , mjini mageneni wapo watu kazi yao ni mdomo tu ushabiki wa mpira tena kibaya zaidi timu za ulaya, wazee hata wamama na watoto wanachinda njaa magengeni lakini maneno hayakaki mdomoni KAZI ZERO

4. Ushabiki wa mpira usio na tija ni janga la JAMII hasa pwani ni ulevi sawa kabisa na VIROBA, BANGI , GONGO na kwa kuutumia kisiasa kwa kuwalewesha jamii hasa vijana

5. Kwa TZ ushabiki huu wa mpira umeshamiri sana kwenye jamii ambayo ipo nyuma kielimu.

MWISHO NAOMBA RADHI KWA WALE WOTE NITAKAOWAKWAZA SIJASEMA TUSISHABIKIE MPIRA KBS HAPANA "KUNYWA ILA USIWE MLEVI"
Nina uhakika 90% wewe unatokea kilimanjaro au Arusha

Tabia zenu za majivuno huwa hazijifichagi hata mara moja
 
Shukran sana kwani sisi binadamu hatukamiliki, nitashukuru tena zaidi kama utanionyesha kosa langu au kunikosoa ili nisije kulirudia tena kwa mwingine

Bahati mbaya mm sio wa maeneo hayo uliyoyataja kabisa, naomba kujua kiashilia kinachoonyesha MAJIVUNO au DHARAU, Samahani tena kama nitakukwaza.
 
Kifupi mkuu hua hatushabikii mpira bali tunashabikia timu (logo ya timu).
Hata wachezaji wote pamoja na kocha wao wakiondoka halafu tukasajili wachezaji wa timu pinzani pamoja na kocha wao bado tutaendelea kushabikia timu ileile, kiufupi ni starehe ambayo imechanganyika na ka uwehu fulani hivi ( yaani ni kama vile tumelishwa ndele) huku wajanja fulani wakiendelea kupiga pesa.

Mkuu katika wachangiaji wote wewe ndio nimekuelewa zaidi. Mimi binafsi ushabiki wa mpira umenishinda kabisa. Nafikiri watu walioanzisha hii michezo akili zao ni sawa na za wale walioanzisha dini.. Yaani mtu unapumbazwa akili kiasi kwamba timu iko ulaya huko lakini ikifungwa wewe huku unakosa raha mpaka kushindwa kula na kununa siku nzima..! Wengine mpaka wanajiua kisa ushabiki wakati hakuna hata senti tano unayolipwa kwa kushabikia mpira. Cha kusikitisha zaidi ni kwamba ukimuambia mtu mimi sishabikii huo upumbavu anaanza kukushangaa na kukuona wewe ndio wa ajabu!
 
Wakuu, hivi nyinyi ambao ni mashabiki wa mpira mnapenda nini haswa????

Mathalani mtu anaposema yeye ni shabiki wa timu fulani mfano Arsenal huwa anaangalia nini haswa mpaka anaamua kuwa shabiki wa timu hiyo???Kama ni aina ya mpira wanaocheza bila shaka mpira unabadilika kulingana na aina ya wachezaji ambao wapo katika hiyo timu pamoja na mbinu za kocha, sasa inakuwaje mtu ni shabiki wa timu hiyo hiyo miaka nenda miaka rudi ,tangu miaka ya 70 huko mpaka leo ,yeye anashabikia timu hiyo hiyo, wakati hata wachezaji tu huama tena unaweza kukuta kikosi kizima kikaondoka kwenda timu nyingine lakini shabiki akaendelea kushabikia timu hiyo hiyo?????

Tena mara nyingi timu inapofungwa wanaoumia zaidi ni mashabiki kuliko wachezaji, wachezaji mara nyingi huwa wanaangalia pesa zao tu timu ifungwe isifungwe wao wanaona poa tu ,tena wakati mwingine hao hao wachezaji husababisha kwa makusudi timu kufungwa kwa kula njama na timu pinzani.

Binafsi sielewi nyinyi mnapenda mpira mnapenda nini haswa kwenye mpira.
timu asiyoipenda kufungwa na timu yake kupata magoli mengi kuliko pinzani Mimi naona ni ishara ya roho mbaya ndio maana sipendi kuangalia Wala kushabikia soka
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mkuu katika wachangiaji wote wewe ndio nimekuelewa zaidi. Mimi binafsi ushabiki wa mpira umenishinda kabisa. Nafikiri watu walioanzisha hii michezo akili zao ni sawa na za wale walioanzisha dini.. Yaani mtu unapumbazwa akili kiasi kwamba timu iko ulaya huko lakini ikifungwa wewe huku unakosa raha mpaka kushindwa kula na kununa siku nzima..! Wengine mpaka wanajiua kisa ushabiki wakati hakuna hata senti tano unayolipwa kwa kushabikia mpira. Cha kusikitisha zaidi ni kwamba ukimuambia mtu mimi sishabikii huo upumbavu anaanza kukushangaa na kukuona wewe ndio wa ajabu!
mashabiki wa mpira ni wa ajabu sana.
 
Kuna mchungaji fulani alisema kucheza mpira ni dhambi kwa sababu mchezaji anapopiga chenga huwa anadanganya mchezaji mwenzake kuwa anapita kulia kumbe anapita kushoto kwa hiyo wanaoangalia watenda dhambi nao wanatenda dhambi indirectly
 
Aisee
 
Kwa Hali hii messi naona Hana ndoto kabsaa za kuingia mbinguni kashajikatia tamaa zake
 
HONGERA SANA Utakuwa ni mtu wa kipekee sana, lazima una akili kubwa pia
Ni watu wachache sana wanagundua hilo, ni kweli michezo kwa ujumla ina faida nyingi sana
hasa kwa wale wadau husika mmoja kwa moja , mchezaji, waajiriwa wa tasisi za michezo,
mapato ya kodi, kiuchumi kama advertisements, washabiki kama burudani na kutumika kisiasa kuwapumbaza vijana n.k

Lakini ebu tuangalie upande wa pili:
1. Ulevi mbaya sana unagharimu pesa na muda hasa muda wa kazi /uzalishaji watu wanabishana kuhusu mpira na hapati pato lolote.

2. Ukanda wa pwani tanga ,Dar, Moro n.k watoto wa kiume wanashindwa kabisa ku concentrate masomo madarasani kisa ushabiki na mpira kila mtoto ana ndoto ya kuwa mchezaji bora, hii ni moja ya sbb wasichna kuongoza madarasani kuliko wavulana mtoto anakariri wachezaji ulaya yote darasani ZERO, na ukiangalia ajira zitokanazo na mpira ni 0.0002%ya ajira zote kwa ujumla

3. Mpira -USHABIKI ni chanzo cha umaskini , uzembe , mjini mageneni wapo watu kazi yao ni mdomo tu ushabiki wa mpira tena kibaya zaidi timu za ulaya, wazee hata wamama na watoto wanachinda njaa magengeni lakini maneno hayakaki mdomoni KAZI ZERO

4. Ushabiki wa mpira usio na tija ni janga la JAMII hasa pwani ni ulevi sawa kabisa na VIROBA, BANGI , GONGO na kwa kuutumia kisiasa kwa kuwalewesha jamii hasa vijana

5. Kwa TZ ushabiki huu wa mpira umeshamiri sana kwenye jamii ambayo ipo nyuma kielimu.

MWISHO NAOMBA RADHI KWA WALE WOTE NITAKAOWAKWAZA SIJASEMA TUSISHABIKIE MPIRA KBS HAPANA "KUNYWA ILA USIWE MLEVI"
Well said. ....Nimeicopy as it is, nitaenda kuipest sehemu fulani.
 
Pana siku humu ulianzisha uzi kuulizia taarab flan kuwa nani anao huo wimbo au nani kapiga sasa hayo mahaba ulonayo penye tasnia hiyo jua wenzio tuna mahaba hayo hayo na soka au kabumbu
 
Back
Top Bottom