Uchaguzi 2020 Hivi mgombea wa CCM atafikisha hata 40% ya kura kweli?

Uchaguzi 2020 Hivi mgombea wa CCM atafikisha hata 40% ya kura kweli?

Unamzungumzia Lisu atayekuwa na kura elfu mbili.
 
Nimeamini na huu ndio ukweli kwamba mgombea wa CCM atapoteza kiti chake siyo kwamba hajafanya kitu laahasha, shida kubwa ni mipangilio isyokua na mfumo ulionyooka. Ameshikilia kufanya mambo makubwa kwa wakati mmoja huku akiacha mambo madogo madogo yanayoigusa jamii. Hii kitu itamwangusha vibaya sana na walimshauri siyo wazoefu wa siasa za vyama vingi.

Unakimbilia kujenga mabarabara, mabwawa ya umeme, kununua mandege na kuhamisha mji kwenda Dodoma kwa wakati mmoja huku huduma zinazoingiza jamii moja kwa moja hutekelezi, watumishi wa umma umewaacha, ajira kiduchu kwa vijana,mikopo ya elimu ya juu shida tupu,huduma za afya bado ni tatizo, shida kwenye biashara mzunguko mgumu wa pesa mtaani, uhuru wa kujieleza ni shida. Haya yote yanachochea chuki, watu hawaangalii miundombinu hii wanataza maisha yao yanakwenda vipi.

Nataka niseme kwamba, kwa mwendo anaokimbia nao Tundu Lissu na hoja zake zenye mashiko na ngumu, ndiyo maana wananchi wengi wanakimbilia kwenye mikutano yake wakidhani kua huyu ndio mtu atakayewania shida zao badala ya yule anayetengeneza vitu kwa ajili ya mtaji wa kisiasa.

Kuna uwezekano CCM hata kura 40%% kisipate. Lissu anaweza kupewa 60% kama pumzi ya waliochoma. Swali ni je, Mgombea wa ccm anaweza kupata kura hata 40% kweli?
mkuu unaonaje matokeo,pole ndugu
 
Haya matokeo yameonyesha watanzania wengi bado wana imani na chama cha mapinduzi. Hata hivyo uchaguzi huu uligubikwa na hujuma kwa mawakala, na wagongea wa vyama vya upinzani
 
Wapinzani inabidi wachukue familia zao ili waandamane kwa kuzunguka nyumba zao. Walianza kuzunguka pale ufipa walipopanga kwa kuwaonyesha wanachama wao kwamba uwezo huo wanao. Aibu kubwa hii, Mlevi wa konyagi na genge lake chali. Hata wale vibaraka waliojaa humu JF kwisha habari yao. Walijinadi hadi kumwalika sara kuku lakini wapi? Tanzania iko imara mwedo mdundo hadi kieleweke. 2025 CCM na Serikali itaangalia imewafikisha Watanzania wapi na inataka kuwapeleka wapi. Hongera sana Chama ChaMapinduzi kwa ushindi mnono chini ya Jemedari John Pombe Magufuli.
 
Back
Top Bottom