Uzi tayari!
Kiasi gani cha matumizi unachomwachia mkeo ili kukidhi mahitaji ya kutwa na maandalizi ya chakula cha jioni?
Ambao hatujaoa njooni tujifunze hapa!
Ninachofanya! Wanapanga bajeti ya mwezi mzima (mke akishirikiana na dada wakazi au waliopo home), kwamba nyama watakula kwa wiki mara ngapi? Maharagwe? Samaki? Kuku au vyovyote vile ila mboga za majani ni lazima kila mlo!!N afaka pia unga wa ugali, mchele, ngano,makande, ndizi, na n.k. zinalika kiasi gani kwa siku/wiki/mwezi. Dharura isikosekane, wageni wamo.
Hii inafanya kunakuwa na urahisi kujua kwa wiki ni kiasi gani cha mlo, na kwa mwezi vinahitajika bila kusahau mahitaji mengine kama gesi, mafuta, umeme, mkaaa,maji na n.k.
Wakishapata bajeti kuu ya mwezi mzima katika mlo, wanapiga bajeti ya vitu vidogo vidogo kama nyanya, vitunguu, mayai, mikate, maandazi kwa siku wanatumia kiasi gani na kisha wanaijumlisha kwa mwezi.
Mwisho bajeti kuu ya mlo inajumlishwa na ya matumizi ya siku inapatikana gharama ya mwezi mzima. Nampa wife hiyo hela kinachobaki kinakwenda kwenye maendeleo na mambo mengine!!
Hii mbinu inasaidia kuhakikisha mlo kamili unalika nyumbani na unaweza kufuatilia vyema ili kuimarisha malezi!!
Mi nikiamka asubuhi sina ninachouliza wala kuulizwa lakini hata katikati ya mwezi ukifulia, home uhakika upo. Hakuna kinachokosekana.
Pia, utajua kipato chako kwa mwezi kinakwenda vipi na namna gani ufanye kuleta maendeleo.
NB: Mambo ya kutoa hela kila siku utaona maisha magumu na mtagombana tuu!! Mjenge mkeo katika bajeti ya kila mwezi, mwanzoni inatesa ila akizoea na mwenyewe atafurahi.